MKURUGENZI WA WIKICHA AFUNGUKA KUHUSU UVUNJAJI WA BAA

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Wikicha Estate Development Agency inayosimamia na kumiliki shughuli zote zinazofanywa kwenye kiwanja namba 48766 kilichopo Ukonga eneo la Banana jiini Dar  es Salaam mzee Wilson Kiguha Chacha afunguka kuwa vijana wake hawakuhusika na uvunjaji wa baa ya Big Mountein.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini kwake Banana Ukonga jijini Dar es Salaam Chacha amesema anasikitishwa na kitendo cha mmiliki wa baa hiyo aliyekuwa  mpangaji wa sehemu ndani ya kiwanja hicho kukamata vijana wake kwa madai kuwa walihusika kuvunja baa hiyo.

“Mimi nilikuwa Marekani kwa matibabu nikapata taarifa kuwa baa hiyo imevunjwa na aliyevunja ni mmiliki mwenyewe ili asilipe kodi yangu niliyokuwa na mdai kwa kipindi kirefu na tayari mahakama ya Ardhi ilimwamuru aondoke mara moja katika eneo hilo,”amesema Chacha.

Ameongeza kuwa “Hukumu ya Mahakama hiyo iliyotolewa Desemba 19, 2022 ilimtaka mpangaji huyo wa baa ya Big Mountein aondoke na alipe malimbikizo yote ya kodi ya pango aliyokuwa anadaiwa na kampuni yangu ya Wikicha”.

Chacha amesema mpangaji huyo ameleta usumbufu mkubwa kwa vijana wake kwani sasa kazi hazifanyiki wanashinda kituo cha polisi kuripoti kila siku, ndipo alipoamua kurudi Tanzania kutoka Marekani alikokuwa anapatiwa matibabu ingawa bado hajapona vizuri ili kushughurikia suala hilo.

“Nimerudi nchini ingawa hali yangu ya kiafya haijaimalika ili kushungulikia jambo hili la uonevu wanalofanyiwa vijana wangu la kukamatwa hovyo na mpangaji wangu kwa taarifa za uongongo kwa lengu la kukwepa kulipa malimbikizo ya kodi ninayomdai.

“Vijana wangu hawajahusika katika uvunjaji wa  baa hiyo kama inavyoelezwa na kwamba mwezi Desemba wafanyakazi wangu wote niliwapa likizo na hata huyo Godfrey Chacha anayedaiwa kutokomea kusiko julikana naye alikuwa likizo, kwa sasa kampuni imempangia majukumu mengine nje ya Dar es Salaam wala hajajificha,  Polisi wakimhitaji nitamleta mara moja.” 

Amesema mmiliki wa baa ya Big Mountain anaeneza taarifa za uongo ndiyo maana hadi sasa jeshi la polisi limeshindwa kupeleka kesi  Mahakamani kwani hakuna ushahidi wa jambo hilo, hivyo vijana wake wanaonewa kuwekwa ndani mara kwa mara.

Mzee Wilson Chacha amewataja vijana wake waliokamatwa na Polisi kuwa ni Joseph Nyagare, Michael Julius Chacha, Amosi Chacha na  Elizabeth Kiguha.

Alipotafutwa mmiliki wa baa ya Big Mountain ambaye alielekeza atafutwe wakili wake, na alipotafutwa wakili wake Frenk Chundu amesema wao wanasubili maamuzi ya jeshi la polisi kupeleka kesi Mahakamani kwani mteja wangu hawezi kujihujumu mwenyewe kwakuwa alifanya uwekezaji wa fedha nyingi kwenye biashara hiyo.

“Uwekezaji uliofanywa na mteja wangu ulikuwa ni wazaidi ya shilingi milioni 100, hivyo si kweli kwamba kavunja yeye tusubili vyombo vya sheria vifanye kazi yake,”amesema Wakili Frenk Chundu.

Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages