WADAU WAKOSHWA NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA BENKI YA TCB

01

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangassa (kulia), akizungumza na wafanyakazi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), alipotembelea kwenye banda la lao, wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika viwanjani hapo leo. ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali,

02
Mkurugenzi Mtendaji wa banki ya biashara Tanzania (TCB)   Sabasaba   Mushingi akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika viwanjani hapo leo. ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali,
03
Meneja Masoko wa Benki ya Biahara ya Tanzania TCB Gloria Mutta (kushoto), akitoa maelezo kwa mteja alietembelea banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika viwanjani hapo leo. ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, katikati ni Meneja Mahusiano wa Benki ya TCB Geace Majige 04Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangassa (kulia), akipokea zawadi kutoka kwa Meneja uwendeshaji Matawi wa Benki ya Biashara ya Tanzania (TCB), alipotembelea kwenye banda  lao, wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika viwanjani hapo leo. ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, wengine ni Maofisa wa Benki hiyo.

05Mkurugenzi wa Masoko na ukuzaji biashara wa Benki ya Biashara ya Tanzania TCB Deo Kwiyukwa (kulia), akizungumza na Meneja Masoko wa kampuni ya simu ya Vodacom kitengo cha Mpesa Noel Mazoya  wakati alipotembelea banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika viwanjani hapo leo. ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, kushoto ni Meneja Mahusiano wa Benki ya TCB Geace Majige

06
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangassa (kulia), akisaini kwenye kitabu cha wageni  alipotembelea banda la Benki ya Biashara Tanzania (TCB), wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika viwanjani hapo leo. ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali,

 

Wadau  pamoja na  wataalam wa huduma za fedha nchini  wamesema Tanzania ipo miongoni mwa nchi zilizopo kwenye  jangwa la sahara  ambazo zina  idadi  ndogo sana ya wananchni wanao tumia huduma za  kifedha   licha ya ujio wa huduma  za simu banki na wakala wa banki  kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma hizo  asilimia 42 kutoka asilimia 23 katika kipindi cha miaka  miwili iliyopita lakini baado kunakazi kubwa ya kutoa elimu ili kukuza ulewa kwa watanzania   kuhakikisha wanafaidika na utumiaji wa huduma  za kifedha.

 

Ambapo Benki ya Biashara ya Tanzania TCB imejipanga kimkakati kwaajili yakutoa elimu ya kifedha nchi nzima ili kuleta tija na hamasa kila mtanzania aweze kutumia huduma hizo kwa urahisi ili kukuza uchumi wa nchi kupitia huduma za fedha.


 Akitoa taarifa hiyo  wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mkurugenzi Mtendaji wa banki ya biashara Tanzania (TCB)   Sabasaba   Mushingi amesema tanzania ni miongoni mwanchi ambazo zipo kusini mwa jangwa la sahara ambazo utafiti uanonyesha  inakazi kubwa ya kutoa elimi kwa   wananchi wake kuelewa umuhimu wa  kutumia huduma za fedha  licha ya ujio Taasisi nyingi za kifedha pamoja na mawakala wa Benki mbalimbali kuongeza idadi ya watumiaji wa uhuduma za kifedha

 

 ameongeza kwakusema kwa asimilimia 42 kutoka asilimia 23 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita bado idadi hiyo  ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine ambazo  hazipo kwenye ukanda huo  kwa hiyo ni muhimu kwa wadau wa fedha kuendelea kutoa elimu hiyo kwakuzingatia mahitaji ya watumiaji. 

 

 Aidha  mushingi ameongezea kuwa utafiti uanonyesha  suala la uelewa  mdogo wa masuala ya uhuduma za kifedha  ndio sababu inayopelekea wananchini wengi  wanaoishi kusini mwajangwa la sahara ikiwemo Tanzania  kuogopa kutumia huduma za kifedha   kwa kuamini sio huduma zinazoweza kumkomboa mtu wa kipato cha chini  lakini kupitia juhudi zilizoanza kuchukuliwa na serikali anaamini wananchi wengi watapata muamko wa kutuia huduma hizo ikiwemo huduma za bima.

 

Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango yameanza toka Novemba 08 hadi Novemba 14 mwaka huu yanalenga wadau mbalimbali wakiwemo; watumishi wa umma, wanafunzi, wakufunzi, wanawake, vijana, watu wenye mahitaji maalumu; wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs); asasi za kiraia; Wahariri na waandishi wa vyombo vya habari; watoa huduma za fedha; na umma kwa ujumla.

 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Zanzibar, Jamal Kassim Ali amesema Serikali imepanga kutumia Fedha kwenye mitaji ya wajasiriamali wadogowadogo ambao wanatoa huduma za kifedha kwenye Mpango wa Maendeleo ya sekta ya Fedha hapa nchini.

 

Amesema Elimu ijikite kwenye huduma za Fedha ili waweze kukuza kipato cha mtu mmojamoja na kuongeza mapato kwa taifa hivyo ni vyema kujipima ipasavyo ili kuongeza ufanisi kwenye huduma za kifedha hapa nchini.

 

kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko na ukuzaji biashara wa Benki ya Biashara ya Tanzania TCB Deo Kwiyukwa amesema Benki hiyo imeshiriki katika maonesho hayo ili kuweza kitangaza huduma wanazozitoa ili kuweza kupanua wigo kwa wananchi hasa wajasiriamali wadogowadogo.

 

Pia amesema TCB wanatoa huduma za kifedha kama vile kufungua akaunti, huduma ya benki kwa njia ya wakala, bima pamoja mikopo pamoja kuinua Biashara zinazowahusu wanawake hii yote ikiwa ni kuwafikia wananchi wote na kutoa huduma iliyobora

Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages