Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB), akihutubia wageni waalikwa wakati wa kumpongeza na kumuaga Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka, ambaye amemaliza muda wake wa utumishi katika chama hicho. Hafla hiyo iliandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka, akizungumza wakati alipokuwa akiwaaga wafanyakazi wa chama hicho pamoja na wadau mbalimbali baada ya kumaliza muda wake wa utumishi katika chama hicho, katika hafla hiyo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama. Hafla hiyo iliandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) wamefanikisha tukio kubwa na la kihistoria katika utaratibu wake wa kupokezana uongozi wa ngazi za juu, ambapo Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu Mtendaji Dk. Aggrey Mlimuka anastaafu na kutoa fursa kwa awamu mpya ya uongozi chini ya mrithi wake, Suzanne Ndomba.
Pamoja na mabadiliko hayo ni jambo la kujivunia kwamba katika uwepo wake, ATE imefanikiwa katika kupevuka kishughuli kiasi cha malengo yake kupanuka zaidi ya lile la kudumisha uhusiano kazini, na sasa ni mdau thabiti katika kuhakikisha mazingira ya kufanya biashara Tanzania yanaboreshwa.
Pamoja na hayo, ATE kama taasisi mama inayounganisha waajiri imefanikiwa kuongeza idadi ya wanachama, na vilevile imekuwa ikiibua miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikitekelezwa kwa kushirikian na wadau nawashirika mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake Dk. Aggrey Mlimuka alisema : “ Mafanikio yaliyofikiwa katika awamu yangu ya uongozi yamewezekana kutokana na ushirkiano wa uongozi wa sasa na uliopita, pamoja na bodi, na nina wiwa kuona nao pia wanapokea shukurani zao zinazostahili”
Dk.Mlimuka alibainisha kuwa ATE inazo changamoto zake zandani ya taasisi, mojawapo na kubwa zaidi ni ulipaji mdogo wa ada za wanachama. “ Tunatakiwa kufanya mabadiliko makubwa kwenye vyanzo vyetu vya fedha na kuondoa hali ya sasa ambapo pamoja na kwamba ATE ni chama chenye wanachama matajir ilakini chenyewe kinabakia kuw nimasikini” alisema Dk Mlimuka.
Kama taasisi inayojihusisha na ajira, ATE inaona haya ya sheria za nchi kuhusiana na maswala ya ajira kufanyiwa mabadiliko ili kuendana na hali halisi ilivyo duniani, hasa kutokana na mabadiliko yaliyoletwa na utandawazi. “ Sheria zetu zimepitwa na wakati na hazishabihiani na haliiliyopo. Baadhi ya sheria zilitungwazaidi ya miaka 17 iliyopita na zina mapungufu. Sheria za ajira hazina budi kuendana na hali halisi ya kisiasa na kiuchumi”, alisema Dk. Mlimika.
“ Nina matumaini kuwa Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini itafanyiwa marekebisho yapasayo ili kuboresha na kuleta ulinganifu katika wajibu na haki za waajiri na wafanyakazi. Natumaini vilevile kuwa ATE itashiriki ipasavyo na kutoa mchango ili kurekebisha hali hiyo na hivyo kusaidia kupanua ajira. Waajiri hawana budi sasa kuitambua ATE.”
Taasisi ya ATE bado itaendelea kuimarisha uhusiano kati yake na serikali na wafanyakazi. Maboresho hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukuza ufanisi kazini, kuongeza kipato cha wafanyakazi na kwa upande wao wafanyakazi watazalisha zaidi, kodi itaongezeka na kufanya hali ya kifedha ya serikali iimarike. Kuboresha uhusiano kutasaidia kuwepo kwa ajira endelevu na ya uhakika. Wafanyakazi wote katika sekta zote bila kubagua watafaidika na mahusiano mazuri maeneo ya uzalishaji.
Alisema Dk Mlimuka : “ Hadi sasa uhusiano na serikali umekuwa ni mzurisana, kwa kuwa ATE imekuwa ikifanya kazi kwa karibu zaidi na wizara mama, viongozi wa ngazi za juu wa serikali na muungano wa wafanyakati yaani TUCTA. Kwa mfano, ATE ni mjumbe wa bodi mbalimbal I za taasisi za umma.”
Kwa upande wa miradi, ATE imekuwa ikiendesha program za kuzuia ajira za watoto kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya watoto, yaani UNICEF. Vilevile ATE imekuwa ikishiriana na vyama visivyokuwa vya kiserikali ili kuongeza tija kwa walemavu na kuwaandaa wawe na sifa za kuajirika. Eneo lingiine limekuwa ni katika kuwawezesha wanawake kushika nyadhifa za uongozi, ambapo mafunzo mbalimbali yamekuwa yakiendeshwa kwa lengo la kuwapa wanawake sifa zitakazowawezesha kukwea hadi ngazi za juu kabisa za uongozi.
Alisema Mlimuka, “ Kwa siku za usoni, tunategemea kupanua wigo wa mradi huu wa wanawake kujumuisha wanasiasa, ambapo tumepanga kuendesha mafunzo kwa Wabunge wanawake kwa upande wa Tanzania Bara na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa upande wa Visiwani.”
Hivyo basi, ikiwa imejipanga vyema kutekeleza malengo yake, ATE leo inastahili kuwa na fahari wakati inamkaribisha Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu Mtendaji mpya, Suzanne Ndomba, ambaye ni matokeo ya program hiyo ya ATE ya kuwawezesha wanawake na kuwaweka tayari kushika nyadhifa za juu za uongozi.
“ ATE imefanya kwa vitendo falsafa yake kwa kutumia mafunzo hayo vyema. Nikiwa moja wa waliofaidika na program hiyo, itoshe kusema tuna uwezo, weledi, uzoefu na sifa ambavyo vinatuwezesha kushika nyadhifa za juu za unongozi vyema,” alisema Suzanne Ndomba. “ Nina msimamo wangu na nina uwezo wa kufanya maamuzi, hata hivyo ninakaribisha maoni na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali. Uongozi unahitaji ushirikiano, na kiongozi si lazima awe anafahamu kila kitu.”
Akigusia kuhusu dira ya ATE, Suzanne alisema dira hiyo imebeba azma ya ATE ya kuhakikisha inatoa mchango kwenye kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania. “ Tutahakikisha tunatekelzea dira hiyo, na nichukue fursa hii kuwahakikishia wadau ya kuwa ATE itaendelea kuwa sauti ya waajiri Tanzania,” alisema.
“Tutaendeela kufanya kazi kwa karibu zaidi na serikali katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini. Kwa Upande wetu, ATE tunaridhishwa na hatua ambazo zimekwisha chukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania.”
Kuhusiana na kupanua wigo wa wanachama, Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu Mtendaji mpya Suzanne Ndomba amesisitiza haja ya waajiri kujiunga na ATE. Alisema kama taasisi mama inayounganisha waajiri wote, shughuli za ATE zinazaa manufaa yasiyobabu ambayo mwisho siku yananufaisha waajiri wote katika sekta zote.
“ Hivyo basi, natoa wito kwa waajiri wasio wanachama kujiunga na ATE na kuongeza nguvu kwenye utakelezaji wa malengo yake. Ili ATE ifanikiwe, inatakiwa waajiri wote wawe wanachama wa taasisi hii,” alisema Suzanne. “ Mimi kama Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu Mtendaji mpya nitahakikisha kuwa naongeza idadi ya wanachama kwa kuhakikisha kila mwajiri anakuwa mwanachama wa ATE.”