WIKI YA AZAKI 2021 KUFANYIKA JIJINI DODOMA, WADAU WAKUTANA KUFANYA UZINDUZI RASMI DSM

  

Mbunge Neema Lugangira (kushoto) akipiga makofi mara baada ya kufanyika uzinduzi rasmi wa wiki ya Azaki uliofanyika Jijini dar es Salaa, (wa kwanza kulia) ni Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo Msajili wa Asasi za Kiraia nchini, Vickness Mayao (katikati yake) ni Rais wa The Foundation for Civil Society (FCS) Dkt. Stigmata Tenga, na (wa tatu kulia) ni Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Asasi za Kiraia Nchini, NACONGO, Lilian Badi.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Wiki ya AZAKI Msajili wa Asasi za Kiraia nchini, Vickness Mayao Akizungumza wakati alipokuwa akitoa hotuba yake ya ufunguzi.

 
Mkurugenzi Mtendaji wa (FCS) Francis Kiwanga Akizungumza na wadau kwenye uzinduzi huo kwa kwa kutoa utangulizi kuelezaea maudhui ya wiki ya AZAKI na umuhimu wake.
Mbunge anawakilisha Asasi za Kiraia Bungeni kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Neema Lugangira akitoa Salamu zake mapema asubuhi ya leo kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Asasi za Kiraia Nchini, NACONGO, Lilian Badi akitoa Salamu za Baraza wakati alipokuwa Akizungumza na wadau mbalimbali kwenye uzinduzi huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Wadau mbalimbali wa na Baadhi ya Viongozi wa Asasi za Kiraia wakifuatilia hotuba za viongozi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Wiki ya AZAZI uliofanyika leo Dar es Salaam.
Rais wa The Foundation for Civil Society (FCS) Dkt. Stigmata Tenga akitoa neno la Shukrani na kufunga rasmi hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa (FCS) Francis Kiwanga akiwa na wadau wengine wakifuatilia hotuba ya Rais wa (FCS), Dkt. Stigmana Tenga.


Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM | MSAJILI wa Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs)Vickness Mayao amezindua rasmi Wiki ya AZAKI inayotarajiwa kufanyika Oktoba 25 hadi Oktoba 29 mwaka huu huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza viongozi wapya wa Baraza la Kitaifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali kupitia Mwenyekiti na timu yake yote.

Akizungumza leo Julai 29,2021 jijini Dar es Salaam wakati akizindua wiki hiyo ya AZAKI,Mayao amesema hiyo ni mara yake ya pili sasa kupata nafasi ya kukutana na wakuregenzi wa Asasi za kiraia nchini pamoja na wadau wengine wa maendeleo, baada ya mkutano wa kikao kazi uliofanyika Januari mwaka huu.

"Ama kwa hakika fursa hizi za kukutana nanyi zimeendelea kuwezesha uimarikaji wa mahusiano na mashirikiano kati ya asasi za kiraia na Serikali kupitia Ofisi ya Msajili na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini. Nichukue nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa mara nyingine tena kwa uongozi mpya wa Baraza la Kitaifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali, kupitia Mwenyekiti na timu yake yote."

"Wizara Pamoja na ofisi yangu tulipata faraja kubwa kuona kuwa sasa uongozi na uratibu wa sekta ya asasi za kiraia nchini umerejea mahali pake. Sote ni mashahidi wa madhara yaliyojitokeza kutokana na ukosefu wa uongozi na uratibu wa sekta ya asasi za kiraia nchini kwa miaka kadhaa.Nipende kuwaahidi kuwa ofisini yangu iko tayari kushirikiana nanyi kwa karibu sana kuhakikisha ustawi na usimamizi dhabiti wa sekta ya asasi za kiraia nchini," amesema.

Aidha ametoa pongezi kwa Kamati ya uchaguzi wa NaCoNGO chini ya Mwenyekiti wake Flaviana Charles wakili msomi na uratibu makini wa mchakato mzima kupitia Mkurugenzi wa Foundation for Civil Society Francis Kiwanga."Hakika mmedhihirisha bayana nguvu ya umoja na mshikamano ambayo ikiendelea kutumika vizuri itapelekea mapinduzi na maendeleo ya hali ya juu kwa sekta hii ya Asasi za kiraia nchini."

Kuhusu Wiki ya AZAKI , Mayao amefafanua wamekutana kwa ajili ya tukio muhimu kwa wadau wa maendeleo nchini ikiwemo Asasi za kiraia, sekta binafsi, pamoja na Serikali ambayo ndio mdau mkubwa wa maendeleo katika taifa letu. "Sote ni mashahidi wa umuhimu na matokeo chanya ya Wiki ya AZAKI toka uzinduzi wake mwaka wa 2018, ikiwemo kuongezeka kwa umoja na mshikamano miongoni mwa wadau wa maendeleo".

"Kuimarika kwa mshikamano kati ya Asasi za kitaifa na za ngazi ya jamii/mashinani, asasi za wazawa na mashirika ya Kimataifa, wakala wa sekta binafsi pamoja na taasisi za serikali na vyombo vya maamuzi.Tunashuhudia pia kuimarika kwa ushiriki wa Asasi katika masuala ya kisera kwa kujiamini zaidi na kwa kushirikiana na vyombo vya serikali pamoja na Bunge katika misingi ya kuaminiana," amesema.

Aidha kupitia Wiki ya AZAKI, wameona kuongezeka kwa ushirikishanaji taarifa na upashanaji habari miongoni mwa wadau wa maendeleo. Pia kuongezeka kwa uelewa miongoni mwa Jamii ya Watanzania kuhusu kazi na huduma zitolewazo na Asasi za kiraia na wadau wa maendeleo, sambamba na mchango wao katika ujenzi wa Taifa.

Kwa miaka miwili mfululizo 2018 na 2019, Wiki ya AZAKI ilifanyika Jijini Dodoma na kuwaleta kwa pamoja wadau muhimu wa maendeleo. Zaidi ya Asasi 1,000 kutoka mikoa yote nchini zimeshiriki katika jukwaa hili tena kwa kujigharamia ushiriki wao katika warsha na maonesho ya kazi za Asasi za kiraia. Kauli mbiu ya Wiki ya AZAKI kwa mwaka 2018 ilikua "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Watu, Sera na Utekelezaji". Ambapo kwa mwaka 2019 kauli mbiu ilikua "Ubia kwa Maendeleo: Ushirikiano kama Nguzo ya Maendeleo nchini Tanzania.

Ameongeza kauli mbiu ya mwaka huu ni mchango wa sekta ya Asasi za kiraia katika maendeleo ya nchi, kwa ufupi AZAKI na maendeleo huku akisisitiza Wiki hiyo ya AZAKI inatarajiwa kufanyika mwezi wa Oktoba 25 - 29 Jijini Dodoma, ikitanguliwa na maonesho ya kazi za Asasi za kiraia nchini Oktoba 23 na Oktoba 24 mwaka huu.

Amesema Wiki ya AZAKI ya mwaka 2018 ilileta mwamko mkubwa miongoni mwa wadau wa sekta kuonesha na kuudhihirishia umma wa watanzania mchango wa AZAKI katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. Miongoni mwa jitihada zilizochukuliwa ni kutoa ripoti ndogo ya mchango wa AZAKI katika uchumi wa Taifa.

"Niwahakikishie kuwa ofisi yangu, kwa kushirikiana na NaCoNGO pamoja na wadau wa kamati ya maandalizi itahakikisha ripoti hii inakamilika kwa wakati na kuwasilishwa katika wiki ya AZAKI mwezi Oktoba mwaka huu 2021," amesema.

Aidha amesema toka kuanzishwa kwa Wiki ya AZAKI Ofisi ya Msajili imekuwa ikishiriki kikamilifu katika maandalizi na utekelezaji wa shughuli hii muhimu, kama mshauri mkuu kwa kamati ya maadalizi. "Mwito wangu kwa kamati ya maandalizi ni kuendelea kuboresha ushirikiano wao kuhakikisha AZAKI zinakua imara na zinaleta mchango unaostahili katika maendeleo ya nchi".

Kwa upande wake Mwenyekti wa Bodi wa Baraza la Uratibu wa NGOs Taifa Lilian Badi amesema ni mara yake ya kwanza kukutana na wadau hao tangu yeye na wenzake 29 wachaguliwe kutoka mikoa 26 na wawakilishi wanne wa makundi maalum kuwa wajumbe wa baraza la uratibu wa NGOs Tanzania.

Aidha amesema ni muhimu kutambua kwa miaka mingi sasa Foundation for Civil Society imekuwa kinara katika kuzijengea uwezo NGOs kupitia ruzuku na hata kuwapatia mafunzo mbalimbali na kuwaunganisha kwa njia kadhaa."Na leo hii tunapozindua wiki ya AZAKI ni ushahidi tosha kuhusu ufanisi na dhamira yetu ambayo haijawahi kupwata na tunajua tukio hili mmekuwa mkilifanya kila mwaka."

Ametumia nafasi hiyo kutoa mwito kwa Foundation for Civil Society na wadau wengine waendelee kuunga mkono chombo hicho muhimu kilichoundwa kisheria kwa kuhakikisha sio tu kinafanya kazi zake kwa ufanisi bali NGOs zinaelewa majukumu na nafasi ya NaCoNGO kisheria na kiuendaji ili kuepuka chombo hicho kujikuta kwenye migogoro ya mara kwa mara na isiyo na tija au kudhoofika.

Awali Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) anayewakilisha Asasi za kiraia amesema ameshauri vitu vya tatu, cha kwanza wakati umefika fedha za ufadhili ambazo zinakuja kwa ajili ya ASASI za kiraia zitekeleze mipango iliyopo kwani takwimu zinaonesha fedha hizo zinapoingia ni asilimia moja tu ndio inakwenda kwenye NGOS za ndani na iliyobakia inakwenda kwenye mashirika ya kimataifa, hivyo umefika wakati ASASI za kiraia nchini kushiriki kikamilifu kwenye maendeleo.

Amesema eneo la pili ambalo ameshauri ,amesema sekta ya AZAKI mara nyingi inahesabiwa kama sehemu ya sekta binafsi, lakini sekta binafsi ni tofauti ambayo inawafanyabishara zaidi na anapokwenda kuongea mwakilishi wa seta binafsi hawezi kuwa anawakilisha sekta ya AZAKI, hivyo ni vema AZAKI nao wakatambula na mwisho amesema bado kunachangamoto katika kufanya kazi wao kama sekta hasa katika kutekeleza matakwa ya kisheria hasa sheria za kodi.

"Kuna mkanganyiko mkubwa kwa mfano unakuta mimi ni mkurugnzi natumia vijana wanaojitolea lakini unapowalipa posho TRA anahesabu wale kama wafanyakazi kitu ambacho sio sahihi, kwa hiyo bado kuna mkanganyiko wa uelewa wetu katika sheria ya kodi kwa mashirika ambayo sio ya kiserikali na hiyo inachangia sisi kukwama."


Share:

BENKI YA SERIKALI YA BIASHARA TCB YAZINDULIWA RASMI

 25Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt.  Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).  wa pili (kushoto), akibonyeza ripoti kuashiria uzinduzi rasmi wa Muonekano  mpya wa jina na Nembo mpya ya Benki mpya ya  Serikali ya Biashara Tanzania Commercial Bank (TIB) ambayo ni muunganiko wa  Benki mbili TIB pamoja na  Benki ya Posta TPB zenye lengo la kuleta ushindani wa kibiashara. Wengine pichani ni Afisa Mtendaji Mkuu wa  Benki ya TCB  Sabasaba Moshingi, Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo  Edmund Mndolwa pamoja na viongozi wengine kutoka Serikalini.3

Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt.  Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Muonekano  mpya wa jina na Nembo mpya ya Benki mpya ya  Serikali ya Biashara Tanzania Commercial Bank (TIB) ambayo ni muunganiko wa  Benki mbili TIB pamoja na  Benki ya Posta TPB zenye lengo la kuleta ushindani wa kibiashara.

31

 Afisa Mtendaji Mkuu wa  Benki ya TCB  Sabasaba Moshingi, akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Muonekano  mpya wa jina na Nembo mpya ya Benki mpya ya  Serikali ya Biashara Tanzania Commercial Bank (TIB) ambayo ni muunganiko wa  Benki mbili TIB pamoja na  Benki ya Posta TPB zenye lengo la kuleta ushindani wa kibiashara.

 

19

Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt.  Mwigulu Lameck Nchemba (watatu kushoto), akikabidhiwa mfano wa kadi zitakazotumika katika Benki hiyo na Afisa Mtendaji Mkuu wa  Benki ya TCB  Sabasaba Moshingi, wapili kulia20

Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt.  Mwigulu Lameck Nchwmba akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo  Edmund Mndolwa.23

Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amezindua rasmi benki ya Serikali ya Biashara 'Tanzania Commercial Bank' (TCB,) ambayo ni muunganiko wa benki ya Maendeleo (TIB)na benki ya Posta (TPB) huku lengo kuu likielezwa ni kuundwa kwa benki kuu ya Serikali na ushindani ambayo itatoa huduma zote za kibenki na biashara kama benki nyingine za kibiashara duniani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri Nchemba amesema benki hizo zimeunganishwa kwa kuzingatia ushauri na matakwa ya kisheria hivyo wafanyakazi wa benki hiyo mpya hawana budi kulitendea haki kwa jina hilo kwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii, ushindani na ubunifu wa hali ya juu na kuleta mageuzi makubwa ya kiutendaji, kimfumo na taswira ya kuhimili ushindani wa kibiashara katika sekta ya fedha.

Amesema, benki hiyo itahudumia wateja wote na wafanyabashara waliokuwa TPB na TIB na itatoa huduma kwa viwango vya kuhakikisha mageuzi zaidi yanaendelea katika sekta ya fedha nchini ili kujenga uchumi imara na shindani katika viwango vya kimataifa.

"Hizi ni jitihada za Serikali katika kujenga uchumi wa taifa kwa kuzingatia uadlifu na ubunifu na sisi Wizara ya fedha na benki kuu tutatoa ushirikiano katika kuijenga benki ya biashara ya Serikali nchini TCB.'' Amesema Mwigulu.

Aidha Waziri Nchemba amezishauri benki zote nchini kushusha riba katika hatua zilizopo mikononi mwao na hiyo ni pamoja na kuangalia namna wanavyofilisi mali za wateja pindi wanaposhindwa kurejesha mikopo yao.

"Baadhi ya madalali wamekuwa wakiendesha minada ya dhamana za wateja kitapeli, mteja anaweza kuwa amelipa asilimia 95 ya mkopo na kubaki asilimia 5 pekee....hapa baadhi ya madalali wasio waaminifu wanauza dhamana kwa mnada ambao unazidi fedha iliyobaki, huu ni utapeli." Amesema.

Pia Mwigulu amewashauri wananchi kutumia fursa za uwepo wa mabenki na kuacha tabia ya kukwepa mifumo rasmi ya fedha na kutumia mifumo isiyo rasmi ikiwemo kukopa sehemu za riba ya juu pamoja na masharti magumu yasiyoweza kuhimili kupitia biashara.

Awali Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa benki TPB na sasa TCB Sabasaba Moshingi amesema kuanzishwa kwa benki hiyo ya biashara ya Serikali ni muhimu sana katika kujenga uchumi imara na shindani pamoja na kuimarisha sekta ya fedha.

Moshingi amesema, Benki kuu ya Tanzania (BOT,) pamoja na Wizara ya Fedha imesimamia mageuzi hayo na kuahidi kufanya kazi kwa uadilifu katika kujenga uchumi imara wa taifa.

Vilevile amesema, benki hiyo ikiwa taasisi ya umma itatoa huduma kwa wateja wote kuanzia ngazi ya chini kulingana na mahitaji yao.

Serikali imeendelea kuunganisha taasisi zake zinazofanya kazi zinazofanana ili kuimarisha ufanisi na ushindani zaidi, Benki ya Biashara ya Serikali (TCB,) ni zao la benki ya Posta (TPB) na benki ya Maendeleo (TIB.)
Share:

Yaraconnect Ya Kampuni Ya Mbolea Ya Yara Kuleta Suluhisho La Kidigitali Katika Sekta Ya Kilimo Nchini

 
Katibu Tawala Msaidizi, Uchumi na Uzalishaji wa Mbeya, Said Maditto ( kushoto), akizungumza na wauza pembejeo za kilimo wa Mkoa wa Mbeya na Songwe na wadau wengine wa mbolea ya Yara wakati wa uzinduzi wa programu ya yaraConnect mjini Mbeya leo. Alimwakilisha mkuu wa mkoa huo katika uzinduzi huo. Kushoto kwake ni Bwanashamba Mwandamizi wa Yara, Maulidi Mkima, Meneja Biashara Kanda ya Kusini, Andrew Ndundulu na Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Yara, Deodath Mtei.
Katibu Tawala Msaidizi, Uchumi na Uzalishaji wa Mbeya, Said Maditto (katikati) waliokaa, Bwanashamba Mwandamizi wa kampuni ya mbolea ya Yara Tanzania, Maulidi Mkima (kushoto), na Meneja Biashara wa Yara Kanda ya Kusini , Andrew Ndundulu, wakipiga picha ya pamoja wauza pembejeo za kilimo wa Mkoa wa Mbeya na Songwe na wadau wengine wa mbolea ya Yara baada ya uzinduzi wa programu ya yaraConnect mjini Mbeya.
Meneja Huduma kwa Wateja Kidigitali wa Kampuni ya Mbolea ya Yara, Eva Sauwa (kulia), akitoa maelekezo kwa mmoja wa wauza pembejea za kampuni hiyo katika hafla ya uzinduzi wa programu ya yaraConect kwa Mkoa wa Njombe ambapo pamoja na mambo mengine wauzaji hao wa pembejeo za yara walipewa mafunzo mbalimbali ya matumizi ya programu hiyo na masuala mengine ya kitaalamu kuhusu kilimo na jinsi watakavyoweza kuwasaidia wakulima ambao ndio wateja wao kitaalamu. Hafla hiyo ilifanyika mjini Njombe jana.
Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Kampuni ya Mbolea ya Yara, Deodath Mtei (wa pili kushoto), akitoa maelekezo kwa mmoja wa wauza pembejea za kamupuni hiyo katika hafla ya uzinduzi wa programu ya yaraConect kwa Mkoa wa Njombe ambapo pamoja na mambo mengine wauzaji hao wa pembejeo za yara walipewa mafunzo mbalimbali ya matumizi ya programu hiyo na masuala mengine ya kitaalamu kuhusu kilimo na jinsi watakavyoweza kuwasaidia wakulima ambao ndio wateja wao kitaalamu. Hafla hiyo ilifanyika mjini Njombe jana.
Katibu Tawala Msaidizi, Uchumi na Uzalishaji wa Mbeya, Said Maditto, akizungumza na wauza pembejeo za kilimo wa Mkoa wa Mbeya na Songwe na wadau wengine wa mbolea ya Yara wakati wa uzinduzi wa programu ya yaraConnect mjini Mbeya leo.
Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Kampuni ya Mbolea ya Yara, Deodath Mtei akizungumza na wauza pembejeo za kilimo wa Mkoa wa Mbeya na Songwe na wadau wengine wa mbolea ya Yara wakati wa uzinduzi wa programu ya yaraConnect mjini Mbeya leo. 
Share:

Dk Batilda Aipongeza Yara Kuwezesha Kilimo Kidigitali

      
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dk. Batilda Burian akitoa hotuba kuzindua program ya yaraConnect ya Kampuni ya mbolea ya Yara, inayolenga katika kutoa elimu ya utaalamu wa kilimo katika hafla iliyofanyika mkoani humo jana. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilata ya Tabora, Dk. Yahya Nawanda na Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Kampuni ya Yara, Deodath Mtei. Progamu hiyo inapatikana katika simu janja kupitia programu za play store na app store.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Dk. Yahya Nawanda, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya yaraConnect kwa Mkoa wa Dodoma jana. Programu hiyo inayopatikana kwenye simu janja kupitia ‘play store na app store’ inalenga katika kutoa elimu ya utaalamu wa masuala ya kilimo ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa huo, Balozi Dk. Batilda Burian (kushoto kwake
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dk. Batilda Burian (kulia), akitambulishwa kwa baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mbolea ya Yara na Bwanashamba Mauzo Kanda ya Ziwa na Magharibi wa kampuni hiyo, Khaji Halidi (kulia kwake), alipokwenda kuzindua program ya yaraConnect kwa Mkoa wa Dodoma jana. Programu hiyo inayopatikana katika simu janja kupitia ‘play store na app store’ inalenga katika kutoa elimu ya utaalamu wa masuala ya kilimo.
 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dk. Batilda Burian (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Dk. Yahya Nawanda (kushoto), akiwa na baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Mbolea ya Yara wakati wakiwasili kwa ajili ya uzinduzi wa program ya yaraConnect kwa mkoa wa Tabora jana. Programu hiyo inayopatikana katika simu janja kupitia ‘play store na app store’ inalenga katika kutoa elimu ya utaalamu wa masuala ya kilimo. Wa pili kushoto ni Meneja Masoko wa Yara, Sheila Chatto na Meneja Huduma kwa Wateja Kidigitali, Eva Sauwa.
Baadhi ya mawakala na wauzaji wa mbolea ya Yara mkoani Tabora wakihudhuria uzinduzi wa programu ya yaraConnect kwa mkoa huo mjini humo jana. Programu hiyo inayolenga katika kutoa elimu ya kitaalamu katika masuala ya kilimo inapatikana katika simu janja kupitia programu za play store na app store.
 
Meneja Masuluhisho wa Huduma za Kidigitali wa Kampuni ya Mbolea ya Yara, Deodath Mtei (katikati), akielekeza jinsi ya kujiunga na programu ya yaraConnect kwa baadhi ya mawakala wa mbolea ya yara wa Mkoani Tabora, wakati wa uzinduzi wa programu hiyo mkoani humu jana. Programu ya yaraConnect inapatikana kwenye simu janja kupitia ‘play store na app store’
Share:

WAZIRI GWAJIMA AZINDUA BARAZA JIPYA LA NACONGO ATOA MAAGIZO

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Doroth Gwajima, akizungumza wakati akipokea taarifa na kuzindua Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO) iliyofanyika leo Julai 10, 2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kutoka Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt.John Jingu, akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Afya Dkt. Doroth Gwajima kuzungumza na kupokea taarifa na kuzindua Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO) iliyofanyika leo Julai 10, 2021 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi Wakili Flaviana Charles, akisoma taarifa kuhusu mchakato wa uchaguzi wa baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Doroth Gwajima, wakati akipokea taarifa na kuzindua Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO) iliyofanyika leo Julai 10, 2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Doroth Gwajima, akipokea taarifa na kuzindua Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO) kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi Wakili Flaviana Charles, iliyofanyika leo Julai 10, 2021 jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Doroth Gwajima, (hayupo pichani) akizungumza na kupokea taarifa na kuzindua Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO) iliyofanyika leo Julai 10, 2021 jijini Dodoma.

Mwenyekiti Mpya wa NaCoNGO, Bi.Lilian Badi, akizungumza wakati wa kupokea taarifa pamoja na uzinduzi wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) hafla iliyofanyika leo Julai 10, 2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa NGOs Dkt.Richard Sambaiga, akizungumza wakati wa kupokea taarifa pamoja na uzinduzi wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) hafla iliyofanyika leo Julai 10, 2021 jijini Dodoma.


WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Doroth Gwajima, akiwa katika picha za pamoja mara baada ya kupokea na kuzindua Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO) iliyofanyika leo Julai 10, 2021 jijini Dodoma.

Na: Mwandishi wetu, DODOMA | WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Doroth Gwajima amelitaka Baraza la la Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali (NaCONGO) kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uzalendo pamoja na kuzingatia Sheria, kanuni, na miongozo iliyopo ili kukidhi matarajio ya waliowachagua.

Hayo ameyasema leo, Julai 10, 2021 jijini Dodoma wakati akipokea taarifa na kuzindua Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyokuwa yakiserikali (NaCONGO), Waziri Gwajima amelitaka Baraza hilo kufanya kazi weledi, uadilifu na uzalendo.

Nitoe wito kwa viongozi na Wajumbe kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uzalendo pamoja na kuzingatia Sheria, kanuni, na miongozo iliyopo ili kukidhi matarajio ya waliowachagua na Jamii ya watanzania kwa ujumla,” amesema.

Waziri Gwajima amesema hana shaka na uongozi mpya kwani wataweza kutoa ratiba mapema baada ya miaka mitatu uchaguzi ufanyike lini.

Mmesema tangu mwaka 2019 lilikuwa mfu sasa sijui tulikuwa tunafanyaje kazi,Baraza hili nimeliamini sina Shaka na weledi,haiba yenu na mtasema haraka lini uchaguzi ufanyike baada ya miaka mitatu,” amesema

Amesema Baraza hilo lilifanya uchaguzi mwaka 2016 ambapo mara baada ya hapo waliokuwa viongozi waligoma kufanya uchaguzi.

Mimi nasema baraza hili liligoma sasa tuwaache ninyi tizameni mbele hao waliogoma mungu anawaona.Kutokufanyika kwa uchaguzi kunasababisha baadhi ya Vyombo vishindwe kufanya kazi,” amesema.

Amesema viongozi wa Kamati ya mpito wamefanya kazi nzuri kwani lilikuwa mambo yalikuwa ni mazito.

Nitoe shukrani zangu za dhati kwa kusimamia zoezi hili,Tunautambua umuhimu wenu hivyo tunawapongeza sana,” amesema.

Waziri Gwajima amemtaka Mwenyekiti wa Baraza hilo, Lilian Badi kusimamia mambo yaende vizuri huku akidai kwenye mambo ya fedha Mayuda huwa hawakosekani.

Baraza hili ni zito simama kwenye nafasi yako kwenye pesa mayuda hawakosekani,” amesema

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kutoka Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt.John Jingu ameipongeza Kamati ya mpito kwa kusimamia vizuri uchaguzi.

Nilikuwa na wasiwasi mwezi mmoja utatosha Leo tunathibitisha kweli umetosha ila watanzania wana matumaini makubwa nendeni mkasimamie Sheria na muwe waadilifu,” amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti mpya wa NaCONGO, Lilian Badi amesema wanaahidi kufanya kazi kisayansi na kwa uadilifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kuwajibika ambapo amedai wamedhamiria kuona NaCONGO inarudi katika ubora wake.

Amesema watakuwa mabalozi wa msajili katika Wilaya kwa kuhakikisha NGO’s zinafuata taratibu na sheria katika kujiendesha.

Pia, amesema wataendelea kushirikiana na Serikali ambapo wameomba kuonana na Rais ili waseme kile ambacho wanacho.

Muda wa kuleta sintofahamu hatuna sisi tunataka kutoa Mchango kwa Taifa letu ila tunaomba (mgeni rasmi) Mwambie Rais mama yetu Samia Suluhu Hassan tunampenda na mama yetu sio mgeni kwenye hii tasnia ya NGO’s,” amesema.

Awali, Mwenyekiti wa Kamati teule ambayo ilisimamia uchaguzi, Flaviana Charles amesema mara baada ya kuchaguliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Doroth Gwajima June 7 mwaka huu walihakikisha uchaguzi unafanyika katika Mikoa 26 na Wilaya 139 kwa kushirikiana na Ofisi za Msajili.

Amesema katika chaguzi hizo walisimamia kanuni na vigezo ikiwemo mgombea kuwa mfanyakazi wa Shirika ambalo limekidhi vigezo vya NGO’s, kuwa raia wa Tanzania, kutokuwa na rekodi ya makosa ya jinai pamoja.

Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa baraza jipya kutengeneza ratiba mapema ya uchaguzi ujao kwani Tanzania ni kubwa, kutengeza kanuni mpya kwani za mwaka 2016 zimepitwa na wakati, kuwe na mfuko wa fedha, kutafuta wafadhili ili waweze kujiendesha, baadhi ya Mikoa iwe na wawakilishi wengi kwani ni mikubwa akitolea mfano Mkoa wa Dar es salaam. 
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages