ACEX CEO URGES LOCAL INVESTORS TO USE DIGITAL PLATFORM IN TRADING EFFECTIVELY

     
African Consolidated Exchange (ACEX) Chief Executive Officer, Peter Mucheru (right), toasts with some of Acex's co-workers, during the official launching of unified exchange platform, ACEX that will allow people to buy and sell assets such as stocks, bonds, forex, cryptocurrencies and other traditional commodities. A brief occasion was held in Nairobi recently.

Tanzanians have been called upon taking advantage offered by the newly launched unified exchange platform, the African Consolidated Exchange (ACEX) that will allow people to buy and sell assets such as stocks, bonds, forex, cryptocurrencies and other traditional commodities.

The trailblazing digital infrastructure would also allow investors to stake in real estate, Venture Capital, Micro-funding, mining and exploration among other projects while earning dividends on trading.

According to ACEX's chief executive officer, Mr Peter Mucheru, the platform intends to rewrite African history by revolutionizing the finance ecosystem through digital means.

Speaking during an exclusive interview with this paper, during the launching event that was conducted in Kenyan capital Nairobi, the chief executive told the paper that ACEX will be the first exchange where native producers from Africa can list their produce, fix their competitive price and earn direct rewards from their efforts.

African products such as cobalt, cocoa, and timber will be synthetically indexed and offered as quotes for traders to take advantage of, he says.

"We also have a microfinancing model, which allows us to partner with local microfinance institutions and facilitate them with funds to provide as credits to micro, small and medium enterprises," he said.

Mr Mucheru said for Tanzania, ACEX are currently reviewing some few microfinance institutions - that when approved will start empowering MSMEs with capital access.

"We understand there is still faint knowledge when it comes to digital economy, with many people in the region fearing scams and online fraudsters. The platform offers education materials and through our local franchises, we ensure that one is well informed before they start trading, " he said.

To start tapping on the company potentials one will need to purchase an initial investment of 100 of Temcoin ($XTEM) which is the native cryptocurrency of ACEX.

Tanzanian Digital trader Mr Elibariki Shilla, who has had near three years experience with the ACEX's potential company TE Markets said that stakeholders and investors can take advantage of the centralized platform because it offers multiple assets trading options unlike any other consolidated market in the world.

"For those who fear the digital trading initiatives, there are experts who offer knowledge and understanding on how to properly exploit the opportunity, as one can also trade by following what the verified traders do, step by step," he said.

Another digital entrepreneur Mr Joshua Fanuel also insisted on the youth using this platform to fully exploit the digital opportunities and overcome the unemployment challenges.

He however said in doing so, one need to make sure they gain enough information so that they can make informed and profitable trading decisions.

"Like in any business, before you put your money one needs to know everything there is about that business. Same for this, you need to be well informed and understand how it goes then start trading, " said Fanuel.

In the ACEX platform there will be a handful of verified people who will be known as merchants who will be allowed to engage in the business of converting $XTEM to fiat (nationally issued currencies) and vice versa.

According to ACEX these merchants will be cast across all regions of Africa to facilitate smooth financial transactions because their fee will be minimal. These merchants will additionally be solving the issue associated with foreign remittances on the African continent.
Share:

KP MOTORZ YANG’ARISHA FAMILIA MARATHON 2021 YAKABIDHI GARI KWA MSINDI WA KM 21 WANAWAKE

    
Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Kuagiza na Kuuza Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe (kulia), akikabidhi funguo ya gari jipya aina ya Toyota Passo lenye thamani ya shs milioni 9.5 kwa mshindi wa kwanza wa KM 21 Wanawake wa mbio za Familia Marathon 2021, Aisha Ibrahim, jijini Dar es Salaam leo. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Meneja Mauzo kwa Makampuni wa KP Motorz, Protas Mbeya na Mwenyekiti wa Familia Marathon, Francisca Alphonce
Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Kuagiza na Kuuza Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe (kushoto), akikabidhi cheti kwa mshindi wa kwanza wa KM 21 Wanawake wa mashindano ya mbio za Familia Marathon 2021, Aisha Ibrahim, wakati wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Familia Marathon, Francisca Alphonce.
Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Kuagiza na Kuuza Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe (kushoto), akikabidhi cheti kwa mshindi wa pili wa KM 21 Wanawake wa mashindano ya mbio za Familia Marathon 2021, Jamila Abdallah, wakati wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Familia Marathon, Francisca Alphonce.
Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Kuagiza na Kuuza Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe (kushoto), akikabidhi cheti kwa mshindi wa tatu wa KM 21 Wanawake wa mashindano ya mbio za Familia Marathon 2021, Verah Mrema, wakati wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Familia Marathon, Francisca Alphonce.
Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Kuagiza na Kuuza Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe (kushoto), akikabidhi cheti kwa mshindi wa nne wa KM 21 Wanawake wa mashindano ya mbio za Familia Marathon 2021, Shameeza Mukhi, wakati wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Familia Marathon, Francisca Alphonce.
Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Kuagiza na Kuuza Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe (kushoto), akikabidhi cheti kwa mshindi wa tano wa KM 21 Wanawake wa mashindano ya mbio za Familia Marathon 2021, Nimishal Ladha, wakati wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Familia Marathon, Francisca Alphonce.
Mshindi wa Mbio za KM 21 Wanawake za Familia Marathon 2021, Aisha Ibrahim akijaribu kuwasha gari lake mara baada ya kukabidhiwa na wadhamini, Kampuni ya Magari ya KP Motorz mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijini Dar es Salaam leo. Aisha atakuwa pia balozi wa KP Motorz kwa muda wa mwaka mmoja.
Mwenyekiti wa Familia Marathon 2021, Francisca Alphonce (wa nne kushoto), akikabidhi tuzo kwa Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe ya kutambua mchango wa udhamini wa kampuni hiyo katika mbio za mwaka huu za Familia Marathon zilizotimua vumbi jijini Dar es Salaam leo zikifanyika eneo la Msasani Beach Club. KP Motorz ilitoa gari jipya aina ya Toyota Passo kwa mshindi wa pili wa KM 21 Wanawake.
Mshindi wa Mbio za KM 21 za Familia Marathon 2021, Aisha Ibrahim akipozi kwa picha mbele ya gari lake, Toyota Passo lililotplewa zawadi na Kampuni ya kuagiza na kuuza magari ya KP Motorsz mara baada ya kuibuka kidedea katika mbio hizo jijini Dar es Salaam leo.
Share:

FAMILIA MARATHON 2021 KUTIMUA VUMBI JUMAMOSI DISEMBA 11

Mwenyekiti wa mbio za Familia Marathon 2021, Bi. Francisca Alphonce (wa tatu Kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Disemba 11, jumamosi. Wengine ni wawakilishi wa Kampuni zinazodhamini mbio hizo.
Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya KCB, Christina Manyenye (wa nne kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu udhamini wao katika mbio za Familia Marathon 2021 zinazotarajiwa kutimua vumbi lake jijini Dar es Salaam jumamosi wiki hii. Usajili unaendelea kufanyika katika Tawi la KCB Mlimani City.
Ofisa Habari Familia Marathon (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Disemba 11, jumamosi. Mbio zitaanzia Msasani Beach Club kuanzia saa 12 asubuhi zikijumuisha mbio za 21km -half marathon, 10km- Corporate Run na 5km -Social Run.
Mkurugenzi Mtendaji was Kampuni ya magari ya KP Motors, Anita Kisima (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu udhamini wao katika mbio za Familia Marathon 2021 zinazotarajiwa kutimua vumbi lake jijini Dar es Salaam jumamosi wiki hii. KP Motors itatoa zawadi ya gari aina ya Passo mpya kwa mshindi mwanamke kati ya washindi kumi atakayeshinda mbio za KM 21. Kushoto kwake ni Mkuu wa Masoko Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya KCB, Christina Manyenye na Ofisa Masoko wa UTT Amis, Rahim Mwanga.
Mkurugenzi Uendeshaji wa Planet Fitness, Ramadhani Mdula (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu udhamini wao katika mbio za Familia Marathon 2021 zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam jumamosi wiki hii.
Meneja wa Kampuni ya Rani Sanitary Pads, Mawi Zahor (kulia ), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu udhamini wao katika mbio za Familia Marathon 2021 zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam jumamosi wiki hii.
Waandaaji na wadhamini wa Familia Marathon 2021 wakionyesha kwa waandishi habari, Dar es Salaam leo, medani na baadhi ya zawadi watakazopewa washiriki wa mbio hizo zitakazofanyika kwa mtindo wa kutembea na kukimbia jijini humo jumamosi wiki hii. Mbio za mwaka huu zimedhaminiwa na KCB Bank, KP Motors, UTT Amis, Premier Security, Optical Centre, Rani Sanitary Pads, Planet Fitness, Knight Support na Xpress Rent.
Share:

WADAU WAKOSHWA NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA BENKI YA TCB

01

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangassa (kulia), akizungumza na wafanyakazi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), alipotembelea kwenye banda la lao, wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika viwanjani hapo leo. ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali,

02
Mkurugenzi Mtendaji wa banki ya biashara Tanzania (TCB)   Sabasaba   Mushingi akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika viwanjani hapo leo. ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali,
03
Meneja Masoko wa Benki ya Biahara ya Tanzania TCB Gloria Mutta (kushoto), akitoa maelezo kwa mteja alietembelea banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika viwanjani hapo leo. ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, katikati ni Meneja Mahusiano wa Benki ya TCB Geace Majige 04Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangassa (kulia), akipokea zawadi kutoka kwa Meneja uwendeshaji Matawi wa Benki ya Biashara ya Tanzania (TCB), alipotembelea kwenye banda  lao, wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika viwanjani hapo leo. ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, wengine ni Maofisa wa Benki hiyo.

05Mkurugenzi wa Masoko na ukuzaji biashara wa Benki ya Biashara ya Tanzania TCB Deo Kwiyukwa (kulia), akizungumza na Meneja Masoko wa kampuni ya simu ya Vodacom kitengo cha Mpesa Noel Mazoya  wakati alipotembelea banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika viwanjani hapo leo. ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, kushoto ni Meneja Mahusiano wa Benki ya TCB Geace Majige

06
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangassa (kulia), akisaini kwenye kitabu cha wageni  alipotembelea banda la Benki ya Biashara Tanzania (TCB), wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika viwanjani hapo leo. ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali,

 

Wadau  pamoja na  wataalam wa huduma za fedha nchini  wamesema Tanzania ipo miongoni mwa nchi zilizopo kwenye  jangwa la sahara  ambazo zina  idadi  ndogo sana ya wananchni wanao tumia huduma za  kifedha   licha ya ujio wa huduma  za simu banki na wakala wa banki  kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma hizo  asilimia 42 kutoka asilimia 23 katika kipindi cha miaka  miwili iliyopita lakini baado kunakazi kubwa ya kutoa elimu ili kukuza ulewa kwa watanzania   kuhakikisha wanafaidika na utumiaji wa huduma  za kifedha.

 

Ambapo Benki ya Biashara ya Tanzania TCB imejipanga kimkakati kwaajili yakutoa elimu ya kifedha nchi nzima ili kuleta tija na hamasa kila mtanzania aweze kutumia huduma hizo kwa urahisi ili kukuza uchumi wa nchi kupitia huduma za fedha.


 Akitoa taarifa hiyo  wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mkurugenzi Mtendaji wa banki ya biashara Tanzania (TCB)   Sabasaba   Mushingi amesema tanzania ni miongoni mwanchi ambazo zipo kusini mwa jangwa la sahara ambazo utafiti uanonyesha  inakazi kubwa ya kutoa elimi kwa   wananchi wake kuelewa umuhimu wa  kutumia huduma za fedha  licha ya ujio Taasisi nyingi za kifedha pamoja na mawakala wa Benki mbalimbali kuongeza idadi ya watumiaji wa uhuduma za kifedha

 

 ameongeza kwakusema kwa asimilimia 42 kutoka asilimia 23 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita bado idadi hiyo  ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine ambazo  hazipo kwenye ukanda huo  kwa hiyo ni muhimu kwa wadau wa fedha kuendelea kutoa elimu hiyo kwakuzingatia mahitaji ya watumiaji. 

 

 Aidha  mushingi ameongezea kuwa utafiti uanonyesha  suala la uelewa  mdogo wa masuala ya uhuduma za kifedha  ndio sababu inayopelekea wananchini wengi  wanaoishi kusini mwajangwa la sahara ikiwemo Tanzania  kuogopa kutumia huduma za kifedha   kwa kuamini sio huduma zinazoweza kumkomboa mtu wa kipato cha chini  lakini kupitia juhudi zilizoanza kuchukuliwa na serikali anaamini wananchi wengi watapata muamko wa kutuia huduma hizo ikiwemo huduma za bima.

 

Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango yameanza toka Novemba 08 hadi Novemba 14 mwaka huu yanalenga wadau mbalimbali wakiwemo; watumishi wa umma, wanafunzi, wakufunzi, wanawake, vijana, watu wenye mahitaji maalumu; wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs); asasi za kiraia; Wahariri na waandishi wa vyombo vya habari; watoa huduma za fedha; na umma kwa ujumla.

 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Zanzibar, Jamal Kassim Ali amesema Serikali imepanga kutumia Fedha kwenye mitaji ya wajasiriamali wadogowadogo ambao wanatoa huduma za kifedha kwenye Mpango wa Maendeleo ya sekta ya Fedha hapa nchini.

 

Amesema Elimu ijikite kwenye huduma za Fedha ili waweze kukuza kipato cha mtu mmojamoja na kuongeza mapato kwa taifa hivyo ni vyema kujipima ipasavyo ili kuongeza ufanisi kwenye huduma za kifedha hapa nchini.

 

kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko na ukuzaji biashara wa Benki ya Biashara ya Tanzania TCB Deo Kwiyukwa amesema Benki hiyo imeshiriki katika maonesho hayo ili kuweza kitangaza huduma wanazozitoa ili kuweza kupanua wigo kwa wananchi hasa wajasiriamali wadogowadogo.

 

Pia amesema TCB wanatoa huduma za kifedha kama vile kufungua akaunti, huduma ya benki kwa njia ya wakala, bima pamoja mikopo pamoja kuinua Biashara zinazowahusu wanawake hii yote ikiwa ni kuwafikia wananchi wote na kutoa huduma iliyobora

Share:

BENKI YA TCB YATINGA MWANZA YAWAFUNDA WANAWAKE WAJASIRIAMALI.

.com/img/a/Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa wa Benki ya Biashara ya Tanzania TCB Bw Moses Manyatta, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa kongamano lenye lengo la kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake wafanya biashara lililoandaliwa na Benki ya TCB kwaajili ya kuwainua na kuwawezesha wanawake wajasiriamali Mkoa wa Mwanza.

01


Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Angelina Mabula (wapili kulia), pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa wa Benki ya Biashara ya Tanzania TCB Bw Moses Manyatta, wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kongamano lenye lengo la kutoa elimu ya ujasiriamali lililoandaliwa na Benki ya TCB kwaajilio yakuwainua na kuwawezesha wanawake wafanya biashara Mkoa wa Mwanza, wengine pichani kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Benki hiyo Grace Majige na Meneja wa Bima wa TCB Emanuel Kaganda na kulia ni Mkurugenzi wa Sheria wa Benki ya Biashara ya Tanzania TCB Bi Mystica Mapunda Ngongi, hafla hiyo imefanyika leo jijini Mwanza.


.com/img/a/Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Angelina Mabula, akikagua bidhaa alipotembelea moja ya banda la mfanya biashara na mjasiriamali na mteja wa Benki ya TCB wakati wa uzinduzi rasmi wa kongamano lenye lengo la kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake wafanya biashara lililoandaliwa na Benki ya TCB kwaajili ya kuwainua na kuwawezesha wanawake wajasiriamali Mkoa wa Mwanza, wengine ni maofisa wa Benki hiyo.
.com/img/a/ 

Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Angelina Mabula akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa kongamano lenye lengo la kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake wafanya biashara lililoandaliwa na Benki ya TCB kwaajili ya kuwainua na kuwawezesha wanawake wajasiriamali Mkoa wa Mwanza


Benki ya Biashara ya Tanzania (TCB) imedhamiria kuinua hadhi ya wanawake nchini kifedha kwa kuwawezesha kiuchumi na kuwasaidia kuwa wajasiriamali shupavu kupitia mikakati mbalimbali endelevu.



Taasisi hiyo kongwe ya fedha nchini imeweka bayana dhamira hiyo wakati wa Kongamano la Wanawake na Biashara la tatu ililoliandaa hapa jana kuwasaidia akinamama kuzing’amua na kuzitumia fursa za kibenki kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla.



TCB imesema itatekeleza jukumu hilo adhimu kwa kuwa kinara wa huduma jumuishi za kifedha za akinamama na kiongozi mbunifu wa huduma hizo sokoni.



Wakiongea kwenye kongamano hilo, maofisa wake waandamizi walisema mafanikio ya jitihada hizo yatatokana na mpango mkakati wa TCB wa kufanya mapinduzi makubwa ya kuwahudumia akinamama.



Aidha, benki hiyo itawaonyesha fursa zinazopatikana TCB na kuwaelimisha jinsi ya kufanya biashara zenye tija. Pia suluhishi za kibenki zilizopo na mpya za kisasa zaidi zitatumika kumkomboa mwanamke kifedha na kumshirikisha kikamilifu katika ujenzi wa taifa.



Wataalamu hao walisema benki hiyo imejiandaa vizuri kwa hilo. Iko imara kifedha, ni uhodari kidijitali na bingwa wa ubunifu ikiwa na wigo mpana wa huduma na mtandao mkubwa wa kuzifikisha popote kwa wakati.



“Tuna mtandao wa matawi makubwa 46, matawi madogo 36, ofisi za wakala za Shirika la Posta Tanzania 120, ATM 84 ambazo zimeunganishwa na ATM 350 za mtandao wa Umoja Switch,” Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Moses Manyatta alibainisha.



Alisema itakuwa rahisi kuwafikia wanawake wengi na kusaidia kuwawezesha kupitia matawi na vituo vyake vya huduma vilivyosambaa kote Tanzania Bara na Visiwani.



"Pamoja na vikwazo vingi vya kiuchumi wanavyokumbana navyo wanawake na changamoto za kifedha walizonazo, tutahakikisha ajenda ya kuwezesha kiuchumi inafikia malengo yaliyokusudiwa," Bw Manyatta alitabainisha.



"Kupitia makongamano haya, tunataka kubainisha mahitaji maalumu ya kifedha ya akinamama na kuihudumia sehemu hii kubwa ya soko kwa namna ya kipekee,” aliongeza.



Mikutano kama hiyo pia itaandaliwa Zanzibar, Tanga, Arusha na Dar es Salaam kama jukwaa la kuwakutanisha akinamama kujifunza mambo mbalimbali na kuijua zaidi Benki ya TCB na huduma zake.



Kongamano la Wanawake na Biashara la TCB la ufunguzi lilifanyika mwanzoni mwa mwezi huu jijini Dodoma. La jana lililofunguliwa rasmi na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angeline Mabula (MB), na liliwajumuisha washiriki wapatao 400 waliotumia mijadala ya pamoja kubadilishana uzoefu, kujuana na kujifunza kutoka kwa wajasiriamali waliofanikiwa.



“Lengo kuu la kuwa na utaratibu huu wa makongamano ya akinamama ni kusaidia kuongeza mchango wao katika uchumi wa taifa kupitia fursa mbalimbali hasa zile zinazopatikana TCB,” Bw Manyatta alifafanua katika wasilisho lake.

Kiongozi huyo alitumia takwimu za mafanikio ya TCB kwa kipindi cha mwaka 2007 hadi 2020 kuonyesha uwezo wa kifedha wa benki hiyo kutimiza jukumu hilo.

Mizania ya TCB ilikua kwa zaidi ya asilimia 1,000 hadi takribani TZS trilioni 1.04 huku mikopo ikiongezeka kwa zaidi ya TZS bilioni 580. Hadi sasa akinamama ambao ni nusu ya wateja milioni moja wa TCB wamekopeshwa zaidi ya TZS bilioni 120.



Kuhusu makongamano hayo ambayo mada yake kuu ni “Nafasi ya Mwanamke katika Kukuza Uchumi wa Taifa”, Mhe. Mabula alisema yamekuja wakati muafaka na yataisadia serikali kuhakikisha hakuna mwanamke anayeachwa nyuma kiuchumi na kimaendeleo.



"Kupitia mpango huu, TCB itatoa mchango mkubwa katika kubadilisha hadhi ya wanawake nchini kifedha na kiuchumi. Nawapongeza kwa kuja na wazo hili na kuwekeza muda na rasilimali kuhakikisha linafanikiwa," alisema Mhe. Mabula.



Aidha, aliitaka benki hiyo isitoe mikopo yake kiholela bila kuhakiki miradi tarajiwa na kutoa miongozo ya kuitumia mikopo hiyo vizuri.



Wachokoza mada ambao wote walikuwa wafanyakazi wanawake wa TCB walisema mikutano hiyo inalenga kuonyesha utayari na uwezo wa benki hiyo kuwasaidia wanawake wajasiriamali.



Walisema TCB inazo fursa lukuki za kibiashara na uwezeshaji kwa ajili yao kupitia huduma maalumu kama akaunti ya Tabasamu na suluhishi mbalimbali kama zile za bima za Nishike Mkono Bima na Kinamama Policy (sera).



Share:

BENKI YA TCB YAAZIMISHA WIKI YA MTEJA KWA KUTOA VYETI KWA WATEJA WAKE

1E1A3180
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Bw Sabasaba Moshingi, (wa pili kulia) akiongoza zoezi la kugongesha glasi kuashiria upendo na furaha kwa wateja wa benki hiyo wakati hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika leo Jumatano Oktoba 6, 2021 katika makao makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Rasilimali watu na Utawala Diana Myonga.
1E1A3188
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Bw Sabasaba akimkabidhi cheti Mteja wa Benki hiyo Goodluck Luhanjo, wakati hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika leo Jumatano Oktoba 6, 2021 katika makao makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.


BENKI ya Biashara Tanzania TCB imesema hatua ya serikali kuweka mifumo imara ya kifedha imezidi kuziboresha huduma za kifedha nchini ikiwemo kuongeza namba ya watu wanaotumia mifumo rasmi ya kifedha.

Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha wiki ya huduma Kwa wateja Mkurugenzi mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi amesema Nia Yao ni kutoa huduma hasa kuwapa fursa wateja wadogo wadogo ambao ndiyo azma ya Serikali na Benki hiyo ya Biashara ya Tanzania.

Moshingi amesema kuwa nia yao nikusogeza huduma rafiki kwa wateja wake ili kuhakikisha kuwa kila mtanzania wa hali ya chini anatumia benki hiyo kwaajili ya uendeshaji wa biashara zao katika Nyanja tofauti.

Kwa upande wao baadhi ya wateja na watumiaji wa mifumo ya kibenki wamesema kitendo Cha baadhi ya taasisi kuanzisha huduma za kuwajali wastaafu imezidi kuongeza weledi hivyo wameishukuru Benki ya TCB kwakuendelea kuwaamini nakuwawezesha kupata mikopo kwa wakati na kwamashart rafiki
Share:

ATE INA MATUMAINI THABITI YA KUTEKELEZA MALENGO NA DIRA YAKE KATIKA USAWA WA KIJINSIA

 WhatsApp%2BImage%2B2021-09-27%2Bat%2B4.16.13%2BPMWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB), akihutubia wageni waalikwa wakati wa kumpongeza na kumuaga Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka, ambaye amemaliza muda wake wa utumishi katika chama hicho. Hafla hiyo iliandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.WhatsApp%2BImage%2B2021-09-27%2Bat%2B4.16.13%2BPM%2B%25281%2529Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka, akizungumza wakati alipokuwa akiwaaga wafanyakazi wa chama hicho pamoja na wadau mbalimbali baada ya kumaliza muda wake wa utumishi katika chama hicho, katika hafla hiyo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama Hafla hiyo iliandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.WhatsApp%2BImage%2B2021-09-27%2Bat%2B4.16.14%2BPM%2B%25281%2529

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)  Wakili Suzanne Ndomba, akihutubia wageni waalikwa wakati wa hafla ya kumpongeza na kumuaga mtanguliziwake, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Chama hicho Dkt. Aggrey Mlimuka, ambae amemaliza muda wake wa utumishi wake, kwenye hafla iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
WhatsApp%2BImage%2B2021-09-27%2Bat%2B4.16.14%2BPM%2B%25282%2529

WhatsApp%2BImage%2B2021-09-27%2Bat%2B4.16.15%2BPM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB) (wapilikushoto), akikabidhi zawadi kwa Mkurungezi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka, iliyotolewa na Chama hicho wakati wa hafla ya kumpongeza na kumuaga mara baada yakumaliza muda wake wa utumishi katika chama hicho kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Chama hicho Bi jayne Nyimbo pamoja na Mke wa Dkt. Aggrey Mlimuka.
 


CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) wamefanikisha tukio kubwa na la kihistoria katika utaratibu wake wa kupokezana uongozi wa ngazi za juu, ambapo Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu Mtendaji Dk. Aggrey Mlimuka anastaafu na kutoa  fursa kwa awamu mpya ya uongozi chini ya mrithi wake, Suzanne Ndomba.



Pamoja na mabadiliko hayo ni jambo la  kujivunia kwamba katika uwepo wake, ATE imefanikiwa katika kupevuka kishughuli kiasi cha malengo yake kupanuka zaidi ya lile la kudumisha uhusiano kazini, na sasa ni mdau thabiti katika kuhakikisha mazingira ya kufanya biashara Tanzania yanaboreshwa.



Pamoja na hayo, ATE kama taasisi mama inayounganisha waajiri imefanikiwa kuongeza idadi ya wanachama, na vilevile imekuwa ikiibua miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikitekelezwa kwa kushirikian na wadau nawashirika mbalimbali.



Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake Dk. Aggrey Mlimuka alisema : “ Mafanikio yaliyofikiwa katika awamu yangu ya uongozi yamewezekana kutokana na ushirkiano wa uongozi    wa sasa na uliopita, pamoja na bodi, na nina wiwa kuona nao pia wanapokea shukurani zao zinazostahili”



Dk.Mlimuka alibainisha kuwa ATE inazo changamoto zake zandani ya taasisi, mojawapo na kubwa zaidi ni ulipaji mdogo wa ada za wanachama. “ Tunatakiwa kufanya mabadiliko makubwa kwenye vyanzo vyetu vya fedha na kuondoa hali ya sasa ambapo pamoja na kwamba ATE ni chama chenye wanachama matajir ilakini  chenyewe kinabakia kuw nimasikini” alisema Dk Mlimuka.



Kama taasisi inayojihusisha na ajira, ATE inaona haya ya sheria za nchi kuhusiana na maswala ya ajira kufanyiwa mabadiliko ili kuendana na hali halisi ilivyo duniani, hasa kutokana na mabadiliko yaliyoletwa na utandawazi. “ Sheria zetu zimepitwa na wakati na hazishabihiani na haliiliyopo. Baadhi ya sheria zilitungwazaidi ya miaka 17 iliyopita na zina mapungufu. Sheria za ajira  hazina budi kuendana na hali halisi ya kisiasa na kiuchumi”, alisema Dk. Mlimika.



“ Nina matumaini kuwa Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini itafanyiwa marekebisho yapasayo ili kuboresha na kuleta ulinganifu katika wajibu na haki za waajiri na wafanyakazi. Natumaini vilevile kuwa ATE  itashiriki ipasavyo na kutoa mchango ili kurekebisha hali hiyo na hivyo kusaidia kupanua ajira. Waajiri hawana budi sasa kuitambua ATE.”



Taasisi ya ATE  bado itaendelea kuimarisha uhusiano kati yake na serikali na wafanyakazi. Maboresho hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukuza ufanisi kazini, kuongeza kipato cha wafanyakazi na kwa upande wao wafanyakazi watazalisha zaidi, kodi itaongezeka  na kufanya hali ya kifedha ya serikali iimarike. Kuboresha uhusiano kutasaidia kuwepo kwa ajira endelevu na ya uhakika. Wafanyakazi wote katika sekta zote bila kubagua watafaidika na mahusiano mazuri maeneo ya uzalishaji.



Alisema Dk Mlimuka : “ Hadi sasa uhusiano na serikali umekuwa ni mzurisana, kwa kuwa ATE imekuwa ikifanya kazi kwa karibu zaidi na wizara mama, viongozi wa ngazi za juu wa serikali  na muungano wa wafanyakati yaani TUCTA.  Kwa mfano, ATE ni mjumbe wa bodi mbalimbal I za taasisi za umma.”



Kwa upande wa miradi, ATE imekuwa ikiendesha program za  kuzuia ajira za watoto kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya watoto, yaani UNICEF. Vilevile ATE imekuwa ikishiriana na vyama visivyokuwa  vya kiserikali ili kuongeza tija kwa walemavu na kuwaandaa wawe na sifa za kuajirika. Eneo lingiine limekuwa ni katika kuwawezesha wanawake kushika nyadhifa za uongozi,  ambapo mafunzo mbalimbali yamekuwa yakiendeshwa kwa lengo la kuwapa wanawake sifa  zitakazowawezesha kukwea hadi ngazi za juu kabisa za uongozi.



Alisema Mlimuka, “ Kwa siku za usoni, tunategemea kupanua wigo wa mradi huu wa wanawake kujumuisha wanasiasa, ambapo tumepanga kuendesha mafunzo kwa Wabunge wanawake kwa upande wa Tanzania Bara na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa upande wa Visiwani.”



Hivyo basi, ikiwa imejipanga vyema kutekeleza malengo yake, ATE leo inastahili kuwa na fahari wakati inamkaribisha Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu Mtendaji mpya, Suzanne Ndomba, ambaye ni matokeo ya program hiyo ya ATE ya kuwawezesha  wanawake na kuwaweka tayari kushika nyadhifa za juu za uongozi.



“ ATE imefanya kwa vitendo falsafa yake kwa kutumia mafunzo hayo vyema. Nikiwa moja wa waliofaidika na program hiyo, itoshe kusema tuna uwezo, weledi, uzoefu na sifa ambavyo vinatuwezesha kushika nyadhifa za juu za unongozi vyema,” alisema Suzanne Ndomba. “ Nina msimamo wangu na nina uwezo wa kufanya maamuzi, hata hivyo ninakaribisha maoni na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali. Uongozi unahitaji ushirikiano, na kiongozi si lazima  awe anafahamu kila kitu.”



Akigusia kuhusu dira ya ATE, Suzanne alisema dira hiyo imebeba azma ya ATE ya kuhakikisha inatoa mchango kwenye kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania. “ Tutahakikisha tunatekelzea dira hiyo, na nichukue fursa hii kuwahakikishia wadau ya kuwa ATE itaendelea kuwa sauti ya waajiri Tanzania,” alisema.



“Tutaendeela kufanya kazi kwa karibu zaidi na serikali katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini. Kwa Upande wetu, ATE tunaridhishwa na hatua ambazo zimekwisha chukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania.”

Kuhusiana na kupanua wigo wa wanachama, Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu Mtendaji mpya Suzanne Ndomba amesisitiza haja ya waajiri kujiunga na ATE.  Alisema kama taasisi mama inayounganisha waajiri wote, shughuli za ATE  zinazaa manufaa yasiyobabu ambayo mwisho  siku yananufaisha waajiri wote katika sekta zote.



“ Hivyo basi, natoa wito kwa waajiri wasio wanachama kujiunga na ATE na kuongeza nguvu kwenye utakelezaji wa malengo yake. Ili ATE ifanikiwe, inatakiwa waajiri wote wawe wanachama wa taasisi hii,” alisema Suzanne. “ Mimi kama Mkurugenzi  Mtendaji na Ofisa Mkuu Mtendaji  mpya  nitahakikisha kuwa  naongeza idadi ya wanachama kwa kuhakikisha kila mwajiri anakuwa mwanachama wa ATE.”

Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages