Absa Tanzania Yashinda Tuzo Ya Benki Bora Ya Kimataifa nchini Tanzania

Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe Exaud Silaoneka Kigahe (wa pili kulia) akikabidhi cheti cha shukrani kwa kutambua mchango wa Benki ya Absa Tanzania kama mdhamini mkuu wa tuzo za kila mwaka za walaji (Tanzania Consumer Choice Awards), kwa Ofisa Fedha Mkuu wa benki hiyo, Obedi Laiser katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Lavine International Agency, Albert Makoye na Mwanzilishi wa tuzo hizo, Diana Laiser.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga (katikati ) akikabidhi tuzo ya kampuni bora ya vinywaji laini nchini kwa Meneja Mkuu wa Kundi la Mampuni ya Vinywaji ya Sayona, Nitin Menon na Meneja Mkuu wa Uzalishaji, Shahid Choudhary wakati wa hafla ya Tuzo bora za mwaka za Walaji (Tanzania Consumer Choice Awards), iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Absa ilikuwa mdhamini mkuu wa tuzo hizo ikitoa jumla ya shs milioni 20 kuzidhamini.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi (katikati) akikabidhi tuzo ya kampuni bora ya bima nchini kwa Meneja Mkuu Msaidizi wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance, Abdul Rauf Suleiman wakati wa hafla ya Tuzo bora za mwaka za Walaji (Tanzania Consumer Choice Awards), iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Marco Yambi. Absa ilikuwa mdhamini mkuu wa tuzo hizo ikitoa jumla ya shs milioni 20 kuzidhamini.
Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser (wa pili kulia) akikabidhi tuzo ya kampuni bora ya mafuta na gesi nchini kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya Lake Oil, Frank Nyabundege wakati wa hafla ya utoaji tuzo bora za walaji za kila mwaka (Tanzania Consumer Choice Awards), iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Maofisa wa kampuni hiyo. Benki ya Absa ni mdhamini mkuu wa tuzo hizo. Absa ilikuwa mdhamini mkuu wa tuzo hizo ikitoa jumla ya shs milioni 20 kuzidhamini.
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Exaud Silaoneka Kigahe (wa tatu kulia) akikabidhi tuzo ya Benki Bora ya Kimataifa ya Mwaka nchini kwa Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo bora za walaji za kila mwaka (Tanzania Consumer Choice Awards) iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo. Absa ilikuwa mdhamini mkuu wa tuzo hizo ikitoa jumla ya shs milioni 20 kuzidhamini.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages