ABSA yasherehekea kuhitimisha kujitenga na BARCLAYS

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni mama ya Benki ya ABSA Tanzania, Absa Group ya Afrika Kusini, imetangaza kukamilika kwa safari yake muhimu ya kujitenga na Barclays.

Safari hiyo ilianza baada ya uamuzi wa Barclays PLC wa mwaka 2016 wa kuiuzia Absa hisa zake za Afrika, huku ikiruhusu benki hiyo kuendelea kutumia chapa ya Barclays katika kipindi cha mpito kati ya Juni 2017 na Juni 2020.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema wiki hii, safari hiyo imekamilika kwa mafanikio Juni 5 mwaka huu.

“Tukiwa kama na chapa ya umoja wa Kiafrika, hatujawahi kuwa tayari kuwa benki iliyojitosheleza zaidi kama tulivyo sasa,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed na kuongeza:

“Sasa tunao uwezo wa kuhodhi na kumiliki michakato yetu mbalimbali pamoja na miundombinu, kuboresha mifumo na maoni kwa ajili ya kuwapa wateja wetu wa Tanzania huduma bora zaidi.

“Kingine cha ziada ni kwamba juhudi hizo zilizoanzishwa zimeboresha uwezo na uimara wa Absa, zikiwanufaisha wafanyakazi sawasawa na wateja wetu.”

Naye Mtendaji Mkuu wa Operesheni wa benki hiyo, Peter Matlare, alisema hatua hiyo iliyofanyika kwa wakati na kwa bajeti iliyopangwa ilikuwa muhimu zaidi ya kubadili jina.

“Sasa tuna fursa ya kubuni na kufanyia uendelevu ushirikiano muhimu unaotuwezesha sisi na wadau wetu kustawi.

“Hata hivyo, kutokana na matukio ya sasa na hali ya uchumi, tumeirekebisha mikakati yetu kuhakikisha tunaweka kipaumbele katika kulinda mtaji. Kubadilisha chapa na kuwa Absa katika mataifa 12 ya Afrika kumetuunganisha chini ya chapa mpja, utambulisho. Malengo na mikakati,” alisema Matlare.

Alisema benki hiyo itaendelea kutekeleza mikakati yake ya kukua; kukuza ufanisi katika huduma na kusonga mbele katika masuala ya kidijitali.

“Tuna historia ndefu na tumekuwa sehemu muhimu katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania. Tutaendelea kuwa washirika katika ukuzaji wa sekta muhimu.

“Kwa mikakati tuliojiwekea, sasa tuna uwezo wa kuongoza sekta hii. Tunaamini kuwa haya yanawezekana kwa kutoa bidhaa zenye ushindani, huduma bora na uzoefu halisi wa Kiafrika,” alisema Abdi.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages