WANAHISA wa DCB wapata GAWIO

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka (wa pili kulia), akizungumza na wanahisa wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanahisa wa benki hiyo ulifanyika kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni; Mwanasheria wa Makampuni, Alex Mgongolwa, Mkurugenzi wa Sheria na Katibu wa Kampuni, Regina Mduma, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa na Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Zawadia Nanyaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa akizungumza na wanahisa wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanahisa wa benki hiyo ulifanyika kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam jana. Kushoto kwake ni Mwanasheria wa Makampuni, Alex Mgongolwa, Mkurugenzi wa Sheria wa DCB na Katibu wa Kampuni, Regina Mduma, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka na Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Zawadia Nanyaro.
Kaimu Mkurugenzi wa fedha wa Benki ya Biashara ya DCB, Ester Bgoya akitoa taarifa za kiutendaji wa kifedha kwa wanahisa wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanahisa wa benki hiyo ulifanyika kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam jana. Kushoto kwake ni Mwanasheria wa Makampuni, Alex Mgongolwa, Mkurugenzi wa Sheria wa DCB na Katibu wa Kampuni, Regina Mduma, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa, Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Lucian Msambichaka na Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Zawadia Nanyaro.
Mkurugenzi wa Sheria wa DCB na Katibu wa Kampuni, Regina Mduma akizungumza na wanahisa wa benki hiyo kwa njia ya mtandao katika Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanahisa wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Makampuni, Alex Mgongolwa, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka  na Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Zawadia Nanyaro.
Mjumbe wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro akichangia hoja katika mkutano mkuu wa 18 wa wanahisa wa benki hiyo ulifanyika kwa njia ya mtandao ofisini mwa benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto kwake ni Mwanasheria wa Makampuni, Alex Mgongolwa, Mkurugenzi wa Sheria na Katibu wa DCB, Regina Mduma, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa na Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Lucian Msambichaka.

WANAHISA wa BENKI ya Biashara ya DCB wana kila sababu ya kuwa na matumaini na benki yao baada ya Bodi ya benki hiyo kutangaza gawio la shs 5.40 kwa kila hisa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanahisa wa DCB  uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Akitangaza gawio hilo lililopitishwa na wanahisa wote kwa njia ya mtandao, Mwenyekiti wa Bodi anayemaliza muda wake wa DCB. Prof. Lucian Msambichaka alisema gawio hilo limetokana na faida waliyopata ya shs bilioni 2.038 baada ya kodi  kufikia Disemba 31, 2019 huku  kiasi cha shs milioni 500 kikitumika kulipia gawio hilo.

Akizungumza zaidi mwenyekiti huyo alisema bodi ilifikia azma ya kulipa gawio la kiasi hicho licha ya faida waliyopata kwa kuzingatia sababu mbalimbali ikiwemo hali ya kibiashara iliyopo nchini iliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na athari za ugonjwa wa homa kali ya mapafu  wa Covid-19.

“Sababu nyingine muhimu iliyochangia azma ya kutoa gawio hili  ni kutumia faida hiyo kuiwezesha benki kuendelea kuimarisha mtaji hivyo kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kupata faida.

“Mafanikio ya DCB yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mchango mkubwa unaotoka kwa wanahisa wa benki yetu kwani hata mwaka 2018 pale benki yetu ilipopata faida ya shs milioni 995, bado wanahisa wetu waliazimia kutumia faida hiyo kuimarisha mtaji badala ya kugawana faida,” aliongeza Prof.  Msambichaka.

Akizungumza na wanahisa hao Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa alisema benki imeendelea kuimarika kimtaji huku wakitimiza kwa uhakika maazimio yote yaliyofikiwa katika mkutano mkuu wa wanahisa wa mwaka uliopita.

Alisema moja ya maazimio ya mkutano huo ilikuwa ni benki kutanua wigo wake na kuwa na mawakala Dar es Salaam na mikoani huku azimio lingine likiwa ni  kupunguza kiwango cha mikopo chechefu. 

“Hayo tuliyachukua na sasa tuna mawakala nchi nzima na vituo vidogo vya kutolea huduma vitano na matawi manane huku tukifanya vizuri katika kupunguza mikopo chechefu kwa kuchukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kuimarisha kitengo cha ukusanyanyi madeni na kudhibiti mawakala wanaokusanya madeni na kuweka utaratibu mzuri ili mikopo inayotolewa ikidhi taratibu zilipo.

“Matokeo ya hatua hizi ni kuwa tumepunguza mikopo chechefu kwa asilimia 19 mwaka 2018 hadi asilimia 14 mwaka 2019 na pia tumepunguza uhamaji wa mikopo kutoka mikopo safi kwenda chechefu kutoka asilimia 2.6 hadi 0.3 mwaka 2019 na tunaendelea kuhakikisha kwamba mikopo inayotolewa inakuwa na uhakika wa kurejeshwa”, aliongeza mkurugenzi huyo.

Akizungumza utendaji wa kifedha, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha ya DCB, Ester Bgoya alisema moja ya sababu inayochangia benki kufanya vizuri ni kupungua kwa gharama za uendeshaji kwa mwaka jana kutoka shs bilioni 17 hadi bilioni 15.8 kunakotokana na udhibiti wa matumizi yasiyo ya lazima pamoja na kuboresha shughuli zao za uendeshaji wa biashara kwa kutumia teknolojia.
Share:

WANAHISA 7,000 DCB KUWEKA HISTORIA JUMAMOSI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati). akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mkutano mkuu wa 18 wa mwaka wa wanahisa wa benki hiyo unaotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam Juni 27 mwaka huu. Kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Deogratius Thadei na Mkurugenzi wa Sheria na Katibu wa Kampuni, Regina Mduma. 

Na mwandishi wetu, Dar

Takriban wanahisa 7,000 wa Benki ya DCB wanatarajiwa kufanya Mkutano Mkuu wa Mwaka Jumamosi ya Juni 27 mwaka huu kwa njia ya mtandao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa, amesema hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kufanyika kidijitali.

“Ninawakaribisha wanahisa wote katika mkutano huo utakaoanza saa nne asubuhi, utakaotoa fursa kwa Benki na wanahisa kutathimini mkakati wa miaka mitano tuliojiwekea,” anasema Ndalahwa.

Hatua ya mkutano mkuu kufanyika kidijitali, mbali na kusababishwa na uwepo wa ugonjwa wa corona, imewezeshwa kutokana na uimara wa kitengo cha teknolojia ndani ya DCB.

Ndalahwa anasema mkakati huo uliopitishwa na kuanza kutekelezwa mwaka 2018, unatarajiwa kukamilika mwaka 2022.

“Mkakati huu una hatua tatu; kwanza kuiondoa benki katika kutengeneza hasara na kuanza kupata faida, pili benki kujiimarisha na tatu na kukukua na kutanuka kwa Benki ya DCB,” anasema.

Tayari mafanikio ya mkakati huo yameshaoneka kwani katika mwaka wa kwanza wa utekelezaji wake, mwaka 2018 benki ilipata faida ya Sh bilioni 1.6 kutoka katika hasara ya Sh bilioni -6.5 mwaka 2017.

Mwaka 2019 DCB imepata faida ya Sh bilioni 2.1 kutoka Sh bilioni 1.6 ya mwaka 2018 huku thamani ya uwekezaji ikiongezeka:

“Hivyo kutoa nafasi kwa wanahisa kupata gawio kutokana na uamuzi watakaoufikia Jumamosi, Pia kutokana na mkakati huu, ukwasi umeongezeka huku mikopo chechefu ikipungua ikiwa ni katika hatua ya pili ya mkakati, yaani kujiimarisha.” Ndalahwa amesema.

Katika hatua ya tatu ya kujipanua, Benki ya DCB imefungua vituo 28 mikoa mbalimbali nchini na inatarajia kufungua matawi matano kwenye mikoa ya kimkakati kiuchumi nchini.

“Ninaamini wanahisa, pamoja na kujiadili gawio linalotokana na faida iliyopatikana; bado wanatamani kuiona benki yao ikiimarika na kuwafikia Watanzania wengi zaidi hivyo kusaidia juhudi za serikali za kuifikisha nchi yetu katika uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025,” anasema Mkurugenzi Mtendaji huyo.
Share:

ABSA yasherehekea kuhitimisha kujitenga na BARCLAYS

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni mama ya Benki ya ABSA Tanzania, Absa Group ya Afrika Kusini, imetangaza kukamilika kwa safari yake muhimu ya kujitenga na Barclays.

Safari hiyo ilianza baada ya uamuzi wa Barclays PLC wa mwaka 2016 wa kuiuzia Absa hisa zake za Afrika, huku ikiruhusu benki hiyo kuendelea kutumia chapa ya Barclays katika kipindi cha mpito kati ya Juni 2017 na Juni 2020.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema wiki hii, safari hiyo imekamilika kwa mafanikio Juni 5 mwaka huu.

“Tukiwa kama na chapa ya umoja wa Kiafrika, hatujawahi kuwa tayari kuwa benki iliyojitosheleza zaidi kama tulivyo sasa,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed na kuongeza:

“Sasa tunao uwezo wa kuhodhi na kumiliki michakato yetu mbalimbali pamoja na miundombinu, kuboresha mifumo na maoni kwa ajili ya kuwapa wateja wetu wa Tanzania huduma bora zaidi.

“Kingine cha ziada ni kwamba juhudi hizo zilizoanzishwa zimeboresha uwezo na uimara wa Absa, zikiwanufaisha wafanyakazi sawasawa na wateja wetu.”

Naye Mtendaji Mkuu wa Operesheni wa benki hiyo, Peter Matlare, alisema hatua hiyo iliyofanyika kwa wakati na kwa bajeti iliyopangwa ilikuwa muhimu zaidi ya kubadili jina.

“Sasa tuna fursa ya kubuni na kufanyia uendelevu ushirikiano muhimu unaotuwezesha sisi na wadau wetu kustawi.

“Hata hivyo, kutokana na matukio ya sasa na hali ya uchumi, tumeirekebisha mikakati yetu kuhakikisha tunaweka kipaumbele katika kulinda mtaji. Kubadilisha chapa na kuwa Absa katika mataifa 12 ya Afrika kumetuunganisha chini ya chapa mpja, utambulisho. Malengo na mikakati,” alisema Matlare.

Alisema benki hiyo itaendelea kutekeleza mikakati yake ya kukua; kukuza ufanisi katika huduma na kusonga mbele katika masuala ya kidijitali.

“Tuna historia ndefu na tumekuwa sehemu muhimu katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania. Tutaendelea kuwa washirika katika ukuzaji wa sekta muhimu.

“Kwa mikakati tuliojiwekea, sasa tuna uwezo wa kuongoza sekta hii. Tunaamini kuwa haya yanawezekana kwa kutoa bidhaa zenye ushindani, huduma bora na uzoefu halisi wa Kiafrika,” alisema Abdi.
Share:

Absa bank Tanzania provides payment holiday to its customers

  • A three months’ loan repayment holiday,
  • For Retail Banking, Business Banking, and Corporate and Investment Banking segments,
  • Will not attract additional administration fees for customers.

As Tanzania and the world confront the financial and economic implications of the Covid-19 pandemic, Absa Bank Tanzania has implemented a payment holiday programme to its customers spanning across Retail, Business Banking, and Corporate and Investment Banking segments. 

The comprehensive debt relief programme is a three months’ loan repayment holiday, which comes alongside other efforts initiated by the bank to support its customers amidst covid19 pandemic. The programme, which started in April, is being conducted in full compliance with the Bank of Tanzania regulatory requirements. 

Speaking about the relief programme, the bank’s Managing Director, Mr. Abdi Mohamed, said “We realize that this is a difficult time for many of our customers and businesses whose financial means are being negatively affected. As such, being responsible financial partners we are happy to support our customers and businesses in order to continue to build thriving businesses and a vibrant economy despite the present challenges.

We urge those customers who have not been impacted to continue making their payments as usual. This will enable us to extend this relief programme to many more customers who may have pressing needs. Customers are encouraged to reach out to their Relationship Managers” 

On his part, the Head of Client Experience, Mr. Samuel Mkuyu, said “Our passion for our customers is as strong as ever and our commitment to serve and protect them is unwavering. This is why our services continue to run smoothly even as we adhere with the guidelines and protocols set out by the Ministry of Health. We continue to encourage our customers to use our digital channels which are more efficient and safer given the present time circumstances.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages