DCB YATENGENEZA FAIDA YA SHILINGI BILIONI 2.3 MWAKA 2019

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Biashara ya DCB, Zacharia Kapama (wa pili kushoto), akisoma hotuba yake katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza  taarifa za fedha ambapo alisema DCB imepata faida ya shs bilioni 2.3 kwa mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 43 kutoka faida ya mwaka 2018 ambayo ilikuwa shs bilioni 1.6. Wengine kutoka kushoto ni; Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano, Rahma Ngassa, Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Fortunata Benedict, wote kutoka DCB.  

Benki ya biashara ya DCB (DCB Commercial Bank Plc) imetangaza kupata faida ya shilingi bilioni 2.3 katika mwaka 2019, ikiwakilisha ongezeko la asilimia 43 kutoka faida ya mwaka 2018 ambayo ilikuwa shilingi bilioni 1.6

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo mbalimbali vya habari leo tarehe 31 Januari 2020 na iliyochapishwa katika magazeti kwa mujibu wa sharia za benki kuu, utendaji wa benki umeendelea kuimarika ikilinganishwa na mwaka uliotangulia huku ufanisi katika nyanja zote muhimu ukiongezeka kwa kiwango cha kuridhisha.

Akiwakilisha taarifa za fedha za robo ya nne ya mwaka 2019, mkurugenzi wa Fedha wa benki ya DCB Ndugu Zacharia Kapama, ameeleza kuwa mafanikio haya yametokana na ukuaji wa mizania ya benki, ambao umechagizwa na ukuaji wa amana za wateja kwa asilimia 14 (Shilingi bilioni 10.1), ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.

Ukuaji wa amana umeisaidia benki pia kuongeza ukuaji wa mikopo ambapo benki imefanikiwa kuongeza kiwango ghafi cha mikopo kwa asilimia 11 (shilingi bilioni 8.0), ambacho ni kiasi kikubwa ukilinganisha na ongezeko la mikopo katika miaka miwili iliyotangulia. Mikopo ghafi ya benki imekua kutoka shilingi bilioni 90.5 mwaka 2018 kufikia shilingi bilioni 93.3 mwaka 2019.

Ili kufikia kiwango hiki, benki imefanikiwa kutoa mikopo mipya kwa wateja wake kinachofikia shilingi bilioni 60, huku shilingi bilioni 18 zikiwakilisha mikopo kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs), na Shilingi Billioni 10 ikiwakilisha mikopo ya wanawake na vijana. Benki pia imeendelea kutoa mikopo kwa sekta mbalimbali zikiwemo sekta binafsi za biashara, elimu afya na ujenzi.

Akielezea upatikanaji wa faida, Ndugu Kapama ameainisha kuwa ukuaji wa faida, ukiachilia mbali kuchangiwa na ukuaji wa mizania, pia umechagizwa na ongezeko la mapato yasiyotokana na riba baada ya benki kufanikiwa kukuza idadi ya wateja wake kutoka 175,000 mwaka 2018 kufikia wateja 194,000 mwaka 2020. Ongezeko hili limeongeza idadi ya akaunti za amana na miamala ya kibenki, huku wateja wakifurahia huduma za kidijitali bila kwenda matawini.

Kwa kuongezea, ufanisi wa benki umeongezeka hasa katika usimamizi wa matumizi ya riba na yasiyo ya riba. Benki imefanikiwa kudhibiti ukuaji wa matumizi yasiyo ya riba, huku ikihakikisha huduma kwa wateja zinaboreshwa. Benki pia imefanikiwa kudhibiti ongezeko la riba kwa wateja na kuhakikisha wateja wanapata thamani bora ya huduma zake bila kuathiri ukuaji wake.

Katika taarifa hiyo, Ndugu Kapama pia ameainisha upunguaji wa mikopo chechefu ya wateja kutoka asilimia 19 mwaka 2018 kufikia asilimia 13 mwaka 2019. Hii imetokana na juhudi za benki kuhakikisha kuna ufanisi na usimamizi madhubuti katika utoaji mikopo na ukusanyaji madeni. Benki itaendelea na juhudi za kuhakikisha mikopo chechefu inafikia kiwango kinachokubalika na wadau wa sekta ya fedha mnamo mwaka huu wa 2020.

Katika miaka yake takriban 17 ya uendeshaji, benki ya DCB imeweza kukuza idadi ya matawi kutoka tawi moja na kufikia manane (8) hadi mwaka huu wa 2019. Pia imekuza idadi ya wateja kufikia 194,000. Ukuaji huu umechangia benki kupata faida mfululizo tangu mwaka 2004 hadi mwaka 2015, na imekuwa ikitoa gawio kwa wanahisa wake katika kipindi chote cha miaka 12.

Hapo mbeleni, benki ya DCB, inatazamia kukuza mizania yake kwa kutumia fursa za ukuzaji biashara na ina azimia kutumia ipasavyo fursa na njia mbadala za utoaji huduma kwa wateja kupitia mitandao, wakala wa kibenki, na upanuzi wa mitandao ya matawi na vituo vidogo vya huduma ambapo itasaidia kwa kiasi kikubwa utengenezaji wa mapato kupitia njia ya mapato yasiyo ya riba.

Benki ya DCB ndio benki ya kwanza kuorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam huku ikiwa ndio benki pekee iliyokua kutoka benki ya wananchi/jamii (community bank) na kufanikiwa kuwa benki ya biashara (commercial bank).

Benki ya DCB imefanikiwa kukuza mtandao wa matawi yake kufikia manane huku ikifungua tawi Dodoma na inaendelea na mchakato wa kufungua matawi na vituo vya huduma (service centers) katika mikoa mingine na imefungua mtandao wa mawakala na huduma za kijiditali hadi kufikia mawakala zaidi ya 700 nchini nzima.

Benki imefanikiwa kuongeza mtaji wake kupitia soko la hisa kwa miaka yote 18 huku ikipata faida mfululizo na kujiimarisha kibiashara. Hivi sasa benki inao uwezo wa kutoa mikopo mikubwa zaidi na ya muda mrefu kwa wateja.

Benki imefanikiwa kuzindua mfumo wa akaunti za kidijitali ambapo umeiwezesha kuhudumia wateja wengi zaidi na kuwafikia hadi wale wa vijijini. Hii imeongeza ukuaji wa mapato na ongezeko la idadi ya wateja na ufanisi katika utoaji huduma.

Akielezea maboresho zaidi ya huduma za kibenki yaliyofanyika, Mkurugenzi wa biashara Mr James Ngaluko  alieleza:

Benki imefanikiwa kuzindua huduma na bidhaa mpya kwa wateja wake ambazo ni Lamba kwanza (Fixed deposit), Akaunti ya Skonga, DCB sokoni, pamoja na garantii za wakandarasi zisizo na dhamana wakati wa kuomba tenda.

Tumeboresha huduma ya mikopo ya nyumba ujenzi wa nyumba kwa kuongeza ushirikiano na Tanzania Mortgage Refinancing Company.

Tumeongeza ufanisi wa huduma ya mikopo kwa ushirikiano na  taasisi ya ushauri FSDT, hivyo kufanya huduma ya utoaji mikopo kwa wateja kuwa ya haraka Zaidi.

Benki imeboresha gharama zake kwa kuondoa gharama katika akaunti za community kama vikoba, akaunti za miradi ya serikali, na akaunti za wastaafu. Hii imepelekea kuongeza idadi kubwa ya wateja ambao wengi ni wa kipato cha cha chini na cha kati.

Benki ya Biashara ya DCB ilianzishwa mwaka 2002 (Ikijulikana kama Dar es Salaam Community Bank)  kutokana na kilio cha wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam kutokuwa na namna ya kupata mitaji midogo ya biashara jambo ambalo lilikuwa changamoto kubwa kwa wajasiriamali wadogo wadogo katika jitihada za kuboresha biashara zao sambamba na masharti magumu kutoka kwa benki nyingi za kibiashara. Kwa kipindi chote cha miaka 17 ya uendeshaji, jukumu mama la benki hii limeendelea kuwa ni kutoa huduma bora za kifedha huku ikijikita zaidi katika kutengeneza miradi endelevu ya kupunguza umaskini na kuendeleza jamii.
Share:

KAMPENI YA USAFI YA OMO NG’ARISHA YAZINDULIWA

Umati wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofurika katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Dar es Salaam jana, kushuhudia uzinduzi rasmi wa Kampeni usafi ya OMO Ng'arisha Festival wakifuatilia matukio ya uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Unilever Tanzania, David Minja (wa nne kushoto), akikata utepe kuzindua kampeni ya kitaifa ya usafi wa iliyopewa jina la Omo Ng'arisha Festival katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam jana.
Wasichana wa promosheni wa Kampeni ya OMO Ng'arisha festival, wakishika mifuko yenye sabuni za Omo kunogesha uzinduzI rasmi wa kampeni ya miezi sita ya usafi iliyopewa jina la OMO Ng'arisha Festival katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Unilever Tanzania, David Minja, akizungumza na umati wa watu uliojitokesa katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Dar es Salaam jana kushuhudia uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya usafi iliyopewa jina la OMO Ng'arisha familia katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam.
Wakazi wa Jiji la Dar e Salaam wakichangamkia kununua sabuni za OMO wakati wa uzinduzi wa kampeni ya OMO Ng'arisha Festival jijini humo jana.
Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam akisikiliza maelezo kuhusu ubora wa sabuni ya OMO kutoka kwa wasichana wa mauzo wa bidhaa hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya OMO Ng'arisha Festival jijini Dar es Salaam jana.
Hapa wakionyesha jinsi ya ufuaji bora wa nguo kwa kutuma sabuni ya OMO ili kupata matokeo bora. Hapo ni katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Dar es Salaam kwenye wa Kampeni ya OMO Ng'arisha Festival.
Balozi wa Kampeni ya OMO Ng'arisha Festival, msanii nguli wa muziki wa taarabu nchini Tanzania, Bi. Isha Mashauzi akifanya vitu vyake wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Msani mahiri wa muziki wa singeli, Seif Mwinjuma 'Sholo Mwamba' akikonga nyoyo za maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofurika katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Dar es Salaam jana kushuhudia uzinduzi rasmi wa Kampeni ya OMO Ng'arisha Festival.


UNILEVER TANZANIA Kampuni inayotengeneza bidhaa mbalimbali leo inazindua kampeni maalumu ya usafi kwa kipindi cha miezi sita iitwayo ‘OmoNg’arisha Festival’ itakayofanyika Tanzania nzima ikiwa na lengo la kuhamasisha faida, ubora na matumizi sahihi ya sabuni bora ya Omo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Jijini Dar es Salaam leo, Meneja Masoko wa bidhaa ya Omo, Bi. Upendo Mkusa alisema ni matumaini yao kwa kupitia kampeni hiyo jamii itatambua matumizi sahihi ili kupata matokeo yanayotarajiwa.

“Ni matumaini yetu watanzania watatumia sabuni ya Omo kwa usahihi kutokana na ukweli kuwa Omo Fast Action na Omo Extra Fresh ni bora katika kupambana na uchafu kwani ina nguvu zaidi ya mara 10 kuliko sabuni za kawaida na ni ukweli kuwa ukitumia Omo kufulia nguo za familia yako wewe na nguo za familia yako mtang’aa, nguo zako ziking’aa wewe na familia yako mtang’aa, pia tunataka kuona watanzania waking’aa,” alitanabaisha Bi. Upendo.

Akizungumza zaidi kuhusu kampeni hiyo, Bi.Upendo meneja masoko wa Omo alisema mara baada ya uzinduzi huo, kampeni hiyo itaendelea katika mikoa ya Dodoma, Dar, Mwanza, Arusha, Moshi na Mbeya. Kuifanya kampeni hii kuwa yenye bashasha na mvuto, Unilever Tanzania inamtangaza Msanii maarufu nchini Tanzania, Bi. Isha Mashauzi kuwa  Balozi wa Kampeni hii ya Omo Ng’arisha, ambaye atakayeshiriki katika matukio mbalimbali katika kampeni hii ikiwemo michezo ya kufurahisha na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali.

Kampeni itashirikisha timu ya promosheni ya Omo kwa kupita mlango kwa mlango majumbani, kwenye maeneo ya wazi na katika sehemu za biashara kuijulisha jamii juu ya ubora, faida na matumizi sahihi ya OMO, ambayo ni moja ya bidhaa kubwa zaidi ya Unilever.

Bi. Upendo meneja huyo alisema pia, wameandaa zoezi maalumu la kuwatambua Wanawake Wajasiriamali 10 katika kila mkoa watakapofanya kampeni hiyo na kuwapa zawadi itakayowasaidia kuboresha biashara zao hivyo kuwafanya kung’aa.“Ni imani yetu wanawake hawa miongoni mwao kuna wenye biashara ndogondogo, tutawatambua na kuwapa zawadi. Ni matarajio yetu utambuzi huu utaleta tija na kuwa kichocheo katika utendaji wao na kukuza biashara zao’’, alimalizia Bi Upendo Mkusa. 

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Unilever Tanzania, Bw. David Minja, alisema “Unilever inatambua na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuendeleza uchumi wa viwanda na katika kuwaletea watu wake maendeleo na kwa kuonyesha uungaji wetu mkono, timu yetu ya kampeni katika mikoa hiyo tuliyoitaja itatembelea katika mahospitali ambako tutaonyesha moyo wa kujali kwa kutoa msaada wa sabuni za Omo kwenye hospitali ya mikoa hiyo tukiongozwa na balozi wetu wa Omo Bi. IshaMashauzi.

“Katika kuendelea kuunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali ya awamu ya tano, tutakuwa mstari wa mbele kuhimiza jamii na wananchi kufanya usafi wa mazingira yao, na nina furaha kwamba kupitia kampeni ya Omo Ng’arisha katika kila mkoa tutakaopitia, timu yetu ya Omo Ng’arisha itashiriki katika shughuli za usafi kwa kushirikiana na viongozi wa mkoa huo,” aliongeza Bw.Minja.

Aidha Mkurugenzi Mkuu huyo alisema Unilever inatoa shukrani kubwa kwa ushirikiano inaoupata kutoka mamlaka mbalimbali za kibiashara na kiserikali hapa nchini. “Tunaipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuweka mazingira wezeshi na juhudi yake katika kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazoikabili jumuiya ya wafanyabiashara. Kwa upande wetu tunaahidi kuongeza ubora wa bidhaa zetu kuhakikisha zinakidhi mahitaji ya wateja wetu, tukifanya biashara kwa kuzingatia kanuni na taratibu zote zilizopo huku tukiangalia namna bora zaidi ya kuinufaisha jamii ya watanzania,” alisema.    

Licha ya bidhaa ya Omo ikiwa na aina mbili za Omo Fast Action na Omo Extra Fresh yenye nguvu mara kumi zaidi, Unilever inazo bidhaa nyingine kama; Sunlight-sabuni ya unga, inayotakatisha vizuri, yenye manukato na kulainisha ngozi, mafuta ya mgando na losheni ya Vaseline yenye uwezo wa kutunza ngozi,Vim-sabuni ya kusafishia ambayo ni kiboko ya uchafu wa nyumbani,  AXE-sprei ya mwili kwa wanaume inayokuacha na harufu nzuri kwa zaidi ya masaa 48 na Royco mchuzi mix, kiungo cha chakula chenye viungo asilia 16 kwa kuongeza ladha murua ya chakula.
Share:

NBC yawataka wanawake wajasiriamali kujiunga na klabu ya biashara ya benki hiyo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia  Uwekezaji, Angela Kairuki, (wa pili kushoto) akishikana mikono na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Rejareja Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri wakati wa semina ya kwanza ya wanawake wa Kiislam kuhusu Ujasiliamali na  Tanzania ya Viwanda iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na waalikwa wengine.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angela Kairuki (wa pili kushoto), akishikana mikono na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Rejareja Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri wakati wa semina ya kwanza ya wanawake wa Kiislam kuhusu Ujasiliamali na  Tanzania ya Viwanda iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Weningine kutoka kushoto ni Meneja wa Tawi la NBC Corporate, Mariam Kombo, Meneja wa Tawi la NBC samora Zubeider Haroun, pamoja na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya semina  hiyo, Mariamu Dedes.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Rejareja Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri, akizungumza na Wanawake wajasiliamali wakati Warsha ya kwanza ya wanawake wa Kiislam kuhusu  Ujasiliamali na  Tanzania ya Viwanda iliyodhaminiwa na Benki ya NBC na kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Mgeni rasmi katika semina hiyo alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angela Kairuki akimwakilisha Makamu wa Raisi, Mama Samia suluhu Hassan.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angela Kairuki (katikati), akipunga mkono wakati akiondoka katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es salaam juzi, baada ya kufungua semina ya kwanza ya wanawake wa Kiislam kuhusu Ujasiliamali na Tanzania ya Viwanda iliyodhaminiwa na Benki ya NBC. Kushoto ni Naibu waziri wa zamani na mmoja wa viongozi wa wanawake wa kiislamu katika Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mama Shamin Khan pamoja na wahudhuriaji wengine.
Baadhi ya Washiriki wakiwa katika semina hiyo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es salaam juzi. Semina hiyo ilidhaminiwa na Benki ya NBC. (Picha zote na Brian Peter)
Share:

Liquid Telecom to launch first 5G wholesale roaming network service in South Africa




Liquid Telecom to launch first 5G wholesale roaming network service in South Africa Access to ultra-fast roaming network will enable network operators to create innovative, reliable and scalable digital services for their customers.

Johannesburg, January 20, 2020 – Leading pan-African telecoms group Liquid Telecom is to launch the first 5G wholesale roaming service in South Africa. Available from early 2020 in all major South African cities, this latest fifth generation of mobile internet connectivity will enable wholesale operators to create innovative, ultra-fast and scalable digital services for their customers.

The 5G wholesale network will also help accelerate the evolution of the Fourth Industrial Revolution (4IR) in South Africa. Reliable connectivity up to 10 times faster than 4G will allow businesses to harness trends such as the Internet of Things (IoT), robotics and artificial intelligence (AI) to innovate transformative new services, increase productivity and deliver more connected customer experiences.

 “This breakthrough 5G wholesale service will create innovation in every aspect of South African society and industry,” says Strive Masiyiwa, Chairman, Liquid Telecom. “For the first time, mobile network operators and ISPs will have open access to Liquid Telecom’s new 5G mobile network. The launch of the service also underscores Liquid Telecom’s vision to bring high-speed connectivity to everyone.”

Liquid Telecom will use its 3.5GHz spectrum asset to build the 5G network and provide nationwide 5G wholesale services to the market early in 2020.

One of the most profound implications of the new service will be its impact on South Africa’s 4IR ambitions, where connected devices communicate with each other, automating the factory floor without the need for human intervention. The fusion of 5G, IoT and other technologies like AI and robotics will touch and transform every facet of business, creating entirely new ways of serving existing needs.

“This is a milestone moment for Liquid Telecom South Africa,” said Nic Rudnick, Group CEO. “Our wholesale operating partners can exploit our new ultra-fast 5G roaming network to build the next generation of communications and make innovation possible, anytime, anywhere. 5G will facilitate real-time remote collaboration, improved business efficiency and lower costs – ultimately driving growth in the South African economy.”

The launch of the 5G wholesale roaming service is another step towards Liquid Telecom ‘Building Africa’s digital future’. The organisation has been investing heavily across the continent where it operates Africa’s largest independent fibre network, spanning almost 70,000km length.

About Liquid Telecom

Liquid Telecom is a leading communications solutions provider across 13 countries primarily in Eastern, Southern and South Africa that serves mobile operators, carriers, enterprise, media and content companies and retail customers with high-speed, reliable connectivity, hosting and co-location and digital services.

 It has built Africa’s largest independent fibre network, approaching 70,000km, and operates state-of-the-art data centres in Johannesburg, Cape Town and Nairobi, with a combined potential 19,000 square metres of rack space and 78 MW of power.

This is in addition to offering leading cloud-based services, such as Microsoft Office365 and Microsoft Azure across our fibre footprint. Through this combined offering Liquid Telecom is enhancing customers’ experience on their digital journey. In October 2019, Liquid Telecom was recognised as ‘The Best African Wholesale Carrier’ for the 8th consecutive year at the Global Carrier Awards. www.liquidtelecom.com
Share:

SAYONA DRINKS LIMITED YAINGIZA KINYWAJI CHA ‘ TWIST’ SOKONI


15 Januari 2020, Dar es Salaam. Wateja wa vinywaji vya Sayona, sasa watakuwa na fahari ya kuchagua zaidi baada ya kampuni inayotengeneza vinywaji baridi ambayo inakuwa kwa kasi jijini Dar es salaam, Sayona Drinks Limited kuboresha na kuzindua upya kinywaji kinachofahamika kwa jina la TWIST.

Kampuni ya Sayona imedhamiria kuwapa machaguo mengi zaidi wateja wake ili kukidhi hitaji za ladha mbalimbali zinazopendwa na wateja.

Akizungumza wakati wa hafla ya utambulisho wa bidhaa hiyo, Pawan Patel, Mkurugenzi Mtendaji wa Sayona Drinks Limited alisema, “Twist ni kiburudisho chenye ladha nzuri, kinachokupa thamani ya pesa yako. Twist inakuja na ladha saba za kipekee ikiwemo ya pasheni, chungwa, limao, embe, nanasi, tangawizi na ladha ya Cola,”

Pia amebainisha kuwa Kampuni itatangaza ujio wa ladha nyingine za kipekee katika siku za usoni. Aliongeza kuwa, Sayona, imedhamiria kukidhi hitaji la wateja wake ndiyo maana wameendelea kuwa wabunifu na kila mwaka wamekuwa wakitambulisha bidhaa mpya sokoni.

“Tunaamini kupitia Twist, tunayo bidhaa bora ambayo ina utofauti na bidhaa nyingine zilizopo sokoni, kuwapa wateja wetu kiburudisho chenye ladha nzuri na ya kipekee,"alisema.

Kwa upande wake, Nitin Menon, Mkurugenzi Mkuu wa Sayona Drinks Ltd Group yeye alizungumzia juu ya utoaji wao huduma kwa wateja na gharama za bidhaa hii mpya.

Menon alisema, hatua ya kuizindua Twist ni matokeo ya kazi kubwa inayofanyika ya kuimarisha ukuaji wa kampuni kupitia mkakati kabambe ambao unaenda sambamba na badiliko la ladha kwa watumiaji na tabia katika ununuzi.

“Bidhaa yetu mpya ya Twist inakuja kwa ujazo wa milimita 300 na 400 katika chupa ya plastiki. Bidhaa itauzwa kwa bei ya rejareja ya shilingi 500 na itapatikana nchi nzima,” aliongeza.

Aidha, alitumia fursa hiyo kuutangazia umma kuwa, wameingia makubaliano na staa wa bongo fleva, Rajabu Abdul Kahali (Harmonize) kuwa balozi wa heshima wa bidhaa za Sayona, ambaye pia alishiriki katika uzinduzi huo.

“Tunajisika fahari kuwa na Harmonize kama balozi wa heshima wa bidhaa yetu. Ni miongoni mwa vijana wapambanaji, mwenye msaada kwa watanzania wengi, anayefanya kazi kwa bidii, lakini pia amekuwa na chachu ya kuupeleka muziki wa Tanzania mbali zaidi. Hili ni Jambo ambalo linaunga mkono malengo na maono yetu ya kuwa kinara katika biashara ya vinywaji baridi barani Afrika,” alisema Menon.

“Tuna imani kwamba ushirikiano huu utawezesha vinywaji vya Sayona kuwa miongoni mwa bidhaa zenye nguvu zaidi Tanzania. Harmonize atatusaidia kuwafikia walengwa wetu nchini Tanzania na sisi kufanya naye kazi kama balozi, ni miongoni mwa hatua muhimu ya yeye kushiriki katika miradi yetu mingi inayokuja.”

Kwa upande wa Harmonize, alisema ni jambo la faraja kufanya kazi na Sayona Drinks Limited na huu ni mwanzo wa ushirikiano mzuri zaidi baina yake na kampuni.

Akizungumzia juu ya uzinduzi wa bidhaa hiyo, Harmonize amesema, “Twist ni kinywaji kizuri chenye ladha za kipekee. Nimekuwa nikikitumia mara kwa mara na nimekuwa sehemu ya ubunifu huu mpya wa bidhaa hii, nina hakika kuwa Watanzania watafurahia bidhaa hii na matumizi yake yatafika nje ya Tanzania. Pia ninajisikia fahari sana kujumuishwa ndani ya Sayona Group ambao wamekuwa na sifa kubwa ya ubora wa bidhaa zao,” alimalizia.
Share:

Wateja watano wa NBC washinda Yamaha, Ibuka Kidedea na NBC Malengo

Meneja wa Kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Mtenya Cheya (kushoto), akizungumza na mmoja washindi aliyeshinda zawadi ya bodaboda katika droo ya tatu ya kampeni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza wa NBC, Dorothea Mabonye, Meneja Chapa na Mawasiliano wa benki hiyo, David Raymond na Wakaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga na Abdallah Hemedi.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa Benki ya NBC, David Raymond (wa tatu kushoto), akizungumza waandishi wa habari katika droo ya tatu ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni; Meneja wa kampeni hiyo, Mtenya Cheya, Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza wa NBC, Dorothea Mabonye, na mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga.
Maofisa wa NBC na kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, wakichezesha droo ya tatu ya kqampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo ambapo wateja watano walijishindia pikipiki mpya aina ya Yamaha.
Meneja wa Kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Mtenya Cheya  (kushoto), akizungumza na mmoja washindi aliyeshinda zawadi ya bodaboda, huku Meneja Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye (kushoto kwake) akishangilia katika droo ya tatu ya kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto kwa Dorothea ni; Meneja Chapa na Mawasiliano wa benki hiyo, David Raymond, Wakaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga na Abdallah Hemedi pamoja na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imewahamasisha watanzania kutumia akaunti ya malengo ya benki hiyo kama suluhisho ya changamoto mbalimbali za kifedha hivyo kuwawezesha kutimiza malengo ya ndoto zao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo kwenye droo ya tatu ya kampeni ya Ibuka kidedea na NBC Malengo, Meneja Chapa na Mawasiliano wa benki hiyo, David Raymond alisema kwamba wateja wa benki hiyo waendelee kutumia benki hiyo ili kutatua changamoto zao za kila siku.

“Huu ni mwanzo wa mwaka na watanzania wengi wanakabiliwa na majukumu kadhaa kama vile ada za shule, kodi za nyumba na bima za gari na nyumba, ni muhimu kwao kuendelea kuwa karibu na benki hii na kwa wale ambao bado hawajafungua akaunti ya malengo ni vyema wakufungua ili waweze kunufaika na zawadi,” alisema Raymond.

Meneja huyo wa Chapa na Mawasiliano alisema kwamba droo hiyo ni ya tatu ambayo ilianza mwezi wa Oktoba mwaka jana na washindi kadhaa wa bodaboda na safari za kutalii mbuga za wanyama Serengeti na Visiwani shelisheli walikwenda na kurudi salama kwa usimamizi na ufadhili wa benki hiyo kupitia kampeni ya malengo akaunti.

Kwenye droo hiyo ya jana washindi watano waliibuka kidedea kwa kujishindia pikipiki aina ya Yamaha, washindi hao ni; Luka Haule Baraka wa Dodoma, Juma Halfani kutoka Songea, Rebeka Ndosh anayeishi Mwanza, Rosemary Kibodya wa Dar es Salaam na Restituta Mbuya wa Morogoro.



Kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo itashuhudia washindi watatu wakiibuka kidedea na kujishindia zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu aina ya Toyo katika droo kubwa inayotarajiwa kufanyika Mwezi Machi mwaka huu.
Share:

DCB ya wahamasisha watanzania kuifanya DCB Skonga suluhisho la elimu ya watoto wao

Balozi wa akaunti maalumu ya DCB Skonga ya Benki ya Biashara ya DCB, Angel Joachim (wa tatu kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja waliofika maeneo ya Mlimani City Dar es Salaam hivi karibuni kuhusu faida za akaunti hiyo inayompa mteja uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi chuo kikuu hata itakapotokea majanga yatakayosababisha ulemavu wa kudumu ama kifo.
Balozi wa akaunti maalumu ya DCB Skonga ya Benki ya Biashara ya DCB, Irene William (kulia), akizungumza na wateja waliofika katika banda la benki hiyo katika maeneo ya Mlimani City Dar es Salaam hivi karibuni kuhusu faida za akaunti hiyo inayompa mteja uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi chuo kikuu hata atakapopata ulemavu wa kudumu au kifo. 
Balozi wa akaunti maalumu ya DCB Skonga ya Benki ya Biashara ya DCB, Hadija Kimaro (kushoto), akizungumza na wanafunzi waliofika katika banda la benki hiyo katika maeneo ya Mlimani City Dar es Salaam hivi karibuni uhusu faida ya akaunti hiyo inayompa mteja uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi chuo kikuu hata atakapopata majanga yatakayosababisha ulemavu wa kudumu ama kifo.  
Balozi wa akaunti maalumu ya DCB Skonga ya Benki ya Biashara ya DCB, Neema Mziray (kulia), akizungumza na baadhi ya watu waliofika katika banda la benki hiyo katika maeneo ya Mlimani City Dar es Salaam hivi karibuni kuhusu faida na jinsi ya kujiunga na akaunti hiyo inayomhakikishia mteja uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi kufika chuo kikuu hata yanapotokea majanga yatakayosabisha ulemavu wa kudumu ama kifo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa wateja wa kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance, Dk. Maria Janja na Mfanyabiashara wa Vyakula, Happy Lyimo.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages