NBC yatoa elimu ya kifedha kwa mama na baba lishe soko la feri

Mkurugenzi wa wateja wadogo wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko, Sarah Laiser (kushoto), na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Alina Maria Kimaryo wakikabidhi msaada wa vifaa vya kufanyia usafi kwa Mtendaji wa Soko la Samaki la Kivukoni, Mkuu Chanje (kulia), ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. Katika hafla hiyo iliyofanyika sokoni hapo juzi, NBC ilikabidhi pia tanki la maji vizibao kwa ajili ya baba na mama lishe na watoza ushuru pamoja pamoja na kutoa elimu ya masuala ya kifedha kwa wafanyabiashara sokoni hapo.

Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Alina Maria Kimaryo (kushoto), akikabidhi vizibao kwa baadhi ya baba na mama lishe pamoja na watoza ushuru wa Soko la Samaki la Kivukoni katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pia msaada wa vifaa vya kufanyia usafi na tanki la maji sokoni hapo, Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. NBC pia ilitoa elimu ya  masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao.

Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko wa Benki ya NBC ambaye pia alimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wake, Sarah Laiser (kushoto), akikabidhi vizibao kwa baadhi ya baba na mama lishe pamoja na watoza ushuru wa Soko la Samaki la Kivukoni katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pia msaada wa vifaa vya kufanyia usafi na tanki la maji sokoni hapo, Dar es Salaam juzi  ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. NBC pia ilitoa elimu ya masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao.

Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko wa Benki ya NBC ambaye pia alimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wake, Sarah Laiser (kushoto), akikabidhi vizibao kwa baadhi ya baba na mama lishe pamoja na watoza ushuru wa Soko la Samaki la Kivukoni katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pia msaada wa vifaa vya kufanyia usafi na tanki la maji sokoni hapo, Dar es Salaam juzi ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. NBC pia ilitoa elimu ya  masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao. 

Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko wa Benki ya NBC ambaye pia alimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wake, Sarah Laiser (wa tatu kushoto), akikabidhi msaada wa tanki la maji kwa Mtendaji wa Soko la Samaki la Kivukoni, Mkuu Chanje katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pia vizibao kwa baba na mama lishe pamoja na watoza ushuru sokoni hapo, Dar es Salaam juzi pamoja na vifaa vya kufanyia usafi, ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. NBC pia ilitoa elimu ya  masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao.

Nguli Wa masuala ya elimu za biashara na ujasiariamali, James Mwang’amba (kushoto), akizungumza na baadhi ya baba na mama lishe na wafanyabiashara wa Soko la Samaki la Kivukoni katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa wafanyabiashara hao sokoni hapo. 

Baadhi ya baba na mama lishe na wachuuzi wengine katika Soko la Samaki la Kivukoni, wakifungua akaunti  kujiunga na Benki ya NBC kupitia huduma yao ya kufunguliwa akaunti mahali alipo mteja. NBC pia sokoni hao, Dar es Salaam, ilitoa elimu ya  masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao pamoja na kuwapa msaada wa vitendea kazi ikiwa ni pamoja na tanki la maji, vizibao na vifaa vya kufanyia usafi.

Mama lishe wa Soko la Kivukoni wakibeba pia la kuwekea takataka muda mfupi baada ya kukabidhiwa na benki ya NBC sokoni hapo juzi.
Share:

Benki ya Biashara ya DCB Yang’ara Tuzo za NBAA

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (wa tatu kushoto) akikabidhi tuzo ya ushindi wa pili katika kitengo cha benki ndogo na za kati katika tuzo za Mwasilishi Bora wa Hesabu za Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi  wa Mahesabu (NBAA) kwa mwaka 2017 kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Biashara ya DCB, Zacharia Kapama, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, Prof. Isaya Jairo.
Mkurugebzi wa Fedha wa DCB, Zacharia Kapamba (katikati) akionyesha tuzo ambayo benki hiyo imeshinda, muda mfupi baada ya kukabidhiwa na naibu waziri wa fedha. Pamoja naye ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo. 
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Biashara ya DCB, Zacharia Kapama (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Utendaji cha DCB, Siriaki Kiriki, wakionyesha tuzo ambayo benki hiyo imeshinda katika kitengo cha benki ndogo ngodo na za kati katika tuzo za  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)
Share:

Barclays hosts an iftar to its staff in Dar

Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (centre), talking to some banks workers to an iftar meal hosted by the bank for its staff  in Dar es Salaam recently.
Barclays Bank Marketing Manager, Joe Bendera (left), talks to some bank’s workers in an iftar dinner hosted by the bank to its members of staff  in Dar es Salaam recently.
Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (second left), is serving a meal during an iftar hosted by the bank for its staff in Dar es Salaam recently.
Some Barclays Bank staff having and iftar meal hosted by the bank in Dar es Salaam recently. 
Share:

WAITARA AFANYA UKAGUZI WA UJENZI WA MIUNDO MBINU UKONGA

Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kulia) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakazi wa Beach Pemba kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam jana katika ziara yake ya ukaguzi wa miundo mbinu inayotengenezwa  pamoja na kusiliza kero za wakazi wa kata hiyo.Moja ya Miundo mbinu inayotengenezwa Beach Pemba ni ujenzi wa mifereji ya chini kwa chini ambayo inatoa maji ya mvua yanayotuama katika eneo hilo na kumwaga moja kwa moja katika bonde la mto Mzinga.Wanne kulia ni Diwani wa kata hiyo Job Isaack.
Diwani Viti maalumu Manispaa ya Ilala, Sara Katanga akizungumza jambo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya kero ya kutuama kwa maji ya mvua katika eneo la Beach Pemba kata ya Mzinga ambayo imefanyiwa utatuzi kwa kutengenezwa mifereji ya chini kwa chini  itakayo yaongoza maji hayo moja kwa moja katika Bonge la Mto Mzinga.
Mkazi wa Beach Pemba, Alhaji Hassani Magogwa akitoa shukrani za dhati kwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (hayupo pichani) baada ya kutatua kero ya maji ya mvua yanayotuama katika eneo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (ailyevaa shati la kaki) akiongozana na wakazi wa kata ya mzingo baada ya kumaliza kukagua mradi wa Beach Pemba.
Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa kituo Kikubwa cha Polisi kata ya Mzinga, Godfrey Mujungu (kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (watatu kushoto) baada ya kuwasili katika kata hiyo kwa aijli ya ukaguzi wa ujenzi wa Kituo hicho kinachotengezwa kwa nguvu ya wananchi kutoka katika mitaa mitatu ambayo ni Mwanagati, Mzinga na Magole. Wapili kulia ni Diwani wa kata hiyo, Job Isaack na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mzinga, Mussa Mtani.

Msimamizi wa ujenzi wa kituo Kikubwa cha Polisi upande wa wakazi wa kata ya Mzinga, Nasir Suleiman (kushoto) akimuonesha Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kipo katika msingi.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Kituo cha Kikubwa cha Polisi cha kata ya Mzinga.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akifanya ukaguzi wa ujenzi wa Barabara inayounganisha Kitunda, Kivule na Msongola.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akizungumza na msimamizi wa ujenzi wa Barabara inayounganisha Kitunda,Kivule na Msongola baada ya kuwasili maeneo ya Matembele kata ya Kivule katika ziara yake ya ukaguzi wa miundo mbinu inayotengenezwa jimboni jijini Dar es Salaam jana.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (wapili kulia) akiongozana na Diwani wa kata ya Kivule, Wilson Molel (watatu kulia) pamoja na viongozi wengine wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuelekea katika ujenzi wa Daraja la Mto Mzinga katika hafla yake ya ukaguzi wa miundo mbinu inayotengenezwa jimboni.

 Daraja la Mto Mzinga likimaliziwa kuwekwa kifusi.

 Mkazi wa Kata ya Kivule akitoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kulia) kwa kutatua kero ya Daraja la Mto Mzinga ambalo lilikuwa ni kikwazo kikubwa cha shughuli za kiuchumi na kijamii kuwa ngumu kwa sababu gari zilikuwa hazivuki kutokana na kuvunjika kwa daraja hilo.Huu ni mwendelezo wa Mbunge kutimiza ahadi ambazo aliziahidi kwa wakazi wa jimbo la Ukonga.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kulia) akiongozana na Diwani wa kata ya Kivule, Wilson Molel katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Daraja la Mto Mzinga.
Diwani wa kata ya Kivule, Wilson Molel (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika ziara ya Mbunge wa Jimbo la Ukonga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi wa Barabara Mabibo Construction Company Limited, Charles Werongo akizungumza katika ziara ya Mbunge wa Jimbo la Ukonga.Mkurugenzi alisema baada ya wiki tatu Daraja litakuwa tayari kwa aijli ya matumizi ya wananchi.
Mkazi wa kata ya Kivule pia Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa kata hiyo, Bihimba Mpaya akitoa neno la Shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara pamoja na Diwani wa kata hiyo, Wilson Molel kutoka na juhudi walizozifanya juu ya kupambana na kero ya  Daraja la Mto Mzinga ambayo ilikuwa ni kikwazo kikubwa kwa wakazi wa kata hiyo pamoja na wafanyakazi wa Taasisi za Kijamii kama Walimu,Madaktari ilikuwa ni ngumu sana kufika maeneo ya kazi mapema kutokana gari kuishia kati kutokana na kukatika kwa Daraja hIvyo kwa Juhudi za Mbunge na Diwani wake kero imetatulika kwa muda mfupi.
Share:

Tanga Cement yajenga wodi ya wazazi Hospitali ya Wilaya ya Handeni

Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Mhandisi Ben Lema (wa pili kulia), akishikana mikono na Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni,Upendo Magashi, katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi jengo la wodi ya
daraja la kwanza
la hospitali ya wilaya hiyo pamoja na samani zake lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87. Wengine ni baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo. Hafla ya makabdhiano ilifanyika Handeni, Tanga hivi karibuni.
Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Mhandisi Ben Lema na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Mgaya Twaha (kulia), wakikata utepe kuashiria makabidhiano rasmi ya  jengo la wodi ya
daraja la kwanza​
la hospitali ya Wilaya ya Handeni lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87 na Tanga Cement. Anayeshuhudia ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Upendo Magashi. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Mgaya Twaha, akizungumza katika hafla ambayo Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC) ilikabidhi jengo la wodi ya
daraja la kwanza
pamoja samani zake la hospitali ya wilaya hiyo lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87. Hafla ya makabidhiano ilifanyika, Handeni mkoani Tanga. Kushoto ni Meneja Kiwanda wa Tanga Cement, Mhandisi Ben Leman na kulia ni Katibu Tawala wa Handeni, Upendo Magashi.
Ofisa Mawasiliano wa  Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Helen Maleko (kulia), akizungumza katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi jengo la wodi ya
daraja la kwanza
pamoja samani zake la hospitali ya wilaya hiyo lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87. Hafla ya makabidhiano ilifanyika, Handeni, Tanga mwishoni mwa wiki. Wengine ni viongozi wa wilaya na kutoka TCPLC. 
Baadhi ya wananchi  na wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya ya Handeni waliohudhuria hafla hiyo.
Viongozi wa kiserikali na kisiasa pamoja na maofisa wa Tanga Cement wakipiga picha ya kumbukumbu mbele ya jengo la wodi ya daraja la kwanza la Hospitali ya Wilaya ya Handeni lililojengwa na kampuni hiyolitatumika kwa wagonjwa maalumu na hata kwa viongozi wakipata dharura wilayani humo.
Share:

Tanzia : MSANII SAM WA UKWELI AFARIKI DUNIA


Usiku wa June 6, 2018 Muimbaji Sam wa Ukweli aliyevuma kwa wimbo wa 'Hata kwetu wapo' amefariki dunia baada ya kuzidiwa ghafla akiwa studio, na kupelekwa katika hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam huku Producer wake Steve aliyekuwa akifanya kazi na Msanii huyo na amesema Sam alikuwa akiumwa na walipomuuliza alisema ni UKIMWI wa kulogwa.

Walichoandika Wolper, Snura na Prof.Jay kuhusu kifo caha Sam wa Ukweli 

..>>> “Sam alianza kuzidiwa toka J’mosi, tulipomuuliza anaumwa nini alisema UKIMWI lakini sio UKIMWI wa kawaida bali wa kulogwa” – Steve

Sasa baadhi ya mastaa mbalimbali wameguswa na tukio hilo na kupost kwenye ukura zao za Instagram…>>>“Dah!!!😢😢😢😢nitasema nini sasa mimi 😢😢tangulia tu mdogo wangu harakati ndio zimeishia hapa kweli????😢😢😢😢😢” – SNURA


.…>>>”Poleni Ndugu wafiwa wote na Mashabiki kwa ujumla jamani🙌 R.i.p Sam Tangulia mwaya 🙏” – WOLPER


……>>>Whaaaat? R.I.P SAM WA UKWELI🙏” Prof. Jay

Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages