Airtel Afrika yaitaja Tanzania Miongoni mwa nchi Tatu kuwashwa Masafa ya Teknolojia ya Mawasiliano ya kasi ya 5G

     
  • Airtel Tanzania miongoni mwa himaya tatu za Airtel zitakazohamia teknolojia ya 5G hivi karibuni
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Airtel Africa, kampuni inayoongoza katika kutoa huduma za mawasiliano na za kuhamisha pesa kwa kutumia simu za mkononi, ikiwa imejikita katika nchi 14 barani Afrika, leo hii nchini Nigeria imezindua mchakato wa kuhamia masafa ya mtandao wa 5G ili kutoa huduma za kisasa na kasi Zaidi kwa wateja wake wote huku ikibainisha Tanzania itafuta kuwashwa kwa teknolojia hiyo ya mawasiliano ya kisasa ya 5G.

Uzinduzi wa masafa hayo ya mtandao wa 5G utafanyika awali katika nchi tatu ikianza Nigeria, ikifuatiwa na Tanzania na Zambia, huku mipango ikiwa inaandaliwa ya kusambaza maeneo yaliyobaki kwenye soko zima.

Kwa kutumia 5G, wateja sasa wanaweza kufurahia kuangalia video zikiwa ngáavu zaidi ya ilivyo sasa, kufurafia kutazama michezo mtandaoni, kurusha matukio mubashara Pamoja na kufurahia kasi zaidi wakiwa popote. Kutokana na kwamba wigo wa mawasiliano utapanuka zaidi kutokana na teknolojia ya kisasa ya 5G pia shughuli za biashara zitaimarika hasa zile zinazotumia mtandao kutoa huduma zake, pamoja na kufanikisha mikutano ya mbali mubashara kupitia mtandao.

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Airtel Afrika Group, Segun Ogunsanya alisema: “Kupitia mtandao wa 5G, tunawapa wateja wetu fursa ya kuishi kidijitali kwa kufurahia maajabu yanayoweza kufanywa na mtandao huu wa teknolojia ya mawasiliano ya kisasa ya 5G. Kwa kukamilisha hili kwa nchi zetu hizi tatu Ikiwemo Tanzania tunadhihirisha tunadhihirisha dhamira yetu tuliyojiwekea ya kuwekeza katika teknolojia ya mtandaoni ya kisasa zaidi ili kufungua wigo mpana na kutoa fursa kwa watumiaji kufanya makubwa, tunawezesha kuiunganisha dunia kidijitali pamoja na wateja wetu kukamilisha maono waliyonayo.

Mtandao wa 5G utajikita zaidi katika maeneo maalum, mfano maeneo ya makazi yenye msongamano mkubwa wa watu na yale yenye huduma kama maduka, hospitali, maeneo ya kati ya mji na maeneo makuu ya kibiashara na mjini. Wakiwa katika maeneo haya mahsusi ya 5G ambayo yatatambulika rasmi na kuwekewa alama, wateja wanaweza kufurahia mtandao kwa kasi ya mara kumi zaidi ya kawaida, na kurusha picha za video za ubora wa hali juu mubashara bila ya kukatika katika. Mtandao wa 5G unaweza kuunganishwa tu kupitia vifaa vinavyoendana nao.
Share:

Mheshimiwa Spika akutana na Uongozi wa juu wa Benki ya Absa Tanzania na kufanya mazungumzo

  
Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser, wakati yeye na ujumbe wake ukimtembelea ofisini kwake, bungeni, Dodoma Jana.
Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson (kushoto) kuzungumza na na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser, wakati yeye na ujumbe wake ukimtembelea ofisini kwake, bungeni, Dodoma Jana.
Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson (wa tatu kushoto) akipiga picha ya kumbukumbu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser (kulia kwake), wakati yeye na ujumbe wake ukimtembelea ofisini kwake, bungeni, Dodoma Jana.
Share:

Benki ya Absa yajitosa kuokoa maisha ya Watoto Njiti

Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser katika hafla ya makabidhiano wa msaada wa vifaa vitakavyosaidia huduma za watoto wanaozaliwa kabla ya muda (Njiti) wakiwa hospitalini. Benki ya Absa imetoa ufadhili wa kiasi cha shs milioni 30 kwa taasisi ya Doris Mollel Kwa ajili hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Doris Mollel.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akizunguza katika hafla ya makabidhiano wa msaada wa vifaa vitakavyosaidia huduma za watoto wanaozaliwa kabla ya muda (Njiti) wakiwa hospitalini. Benki ya Absa imetoa ufadhili wa kiasi cha shs milioni 30 kwa taasisi ya Doris Mollel kwa ajili hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser(katikati), akizungumza katika hafla ya makabidhiano wa msaada wa vifaa vitakavyosaidia huduma za watoto wanaozaliwa kabla ya muda (Njiti) wakiwa hospitalini. Benki ya Absa imetoa ufadhili wa kiasi cha shs milioni 30 kwa taasisi ya Doris Mollel Kwa ajili hiyo. Kushoto kwake ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati), akikata utepe kuzindua hafla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vitakavyosaidia huduma za watoto wanaozaliwa kabla ya muda (Njiti) wakiwa hospitalini. Benki ya Absa imetoa ufadhili wa kiasi cha shs milioni 30 kwa taasisi ya Doris Mollel kwa ajili hiyo.
Mkurugenzi wa taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel akitoa shukurani Kwa mgeni rasmi, benki ya Absa na wote wakiofanikisha upatikanaji wa vifaa hivyo vitakavyosaidia kuokoa maisha ya watoto nyiti wakiwa hospitalini.
Share:

Benki ya DCB yazidi kujiimarisha kimtaji na kuendelea kupata faida

  
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Alexander Sanga (wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe wa bodi ya benki hiyo wakati wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Mwaka wa Wanahisa wa benki hiyo 2023 jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mwanasheria wa benki hiyo, Alex Mgongolwa, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Isidori Msaki na wajumbe wengine; Dk. Amina Baamary, Cliff Maregeli na David Shambwe.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Alexander Sanga akifungua Mkutano Mkuu wa 21 wa Mwaka wa Wanahisa wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Mwaka wa Wanahisa wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Dk. Amina Baamary (kulia) akizungumza na baadhi ya wanahisa na wajumbe wengine wa bodi hiyo, baada ya kumaliza Mkutano Mkuu wa 21 wa Mwaka wa Wanahisa wa benki hiyo jijini Dar es Salaam Jana.
Sehemu ya wanahisa wa Benki ya DCB wakihudhuria Mkutano Mkuu wa 21 wa Mwaka wa Wanahisa wa benki hiyo, jijini Dar es Salaam jana.

Na Mwandishi Wetu,

BENKI ya Biashara ya DCB imeendelea kujivunia kuongezeka kwa mtaji wake huku ikijiendesha kwa faida inayoongezeka kila mwaka licha ya changamoto kadhaa za kiuchumi, wanahisa wa benki hiyo wameelezwa jijini Dar es Salaam jana

Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 21 wa Mwaka wa Wanahisa wa DCB, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Bi. Zawadia Nanyaro alisema benki yao ipo imara kimtaji unaofikia kiasi cha shs 28.5 bilioni unaovuka vigezo vya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) vya shs 15 bilioni vilivyowekwa kwa benki za biashara.

Benki yetu ilipata faida baada ya kodi ya shs 747 milioni kwa mwaka 2022, faida iliyochangiwa na mapato yasiyotokana riba ya shs 10.3 bilioni ambayo ni mafanikio ya asilimia 111 ya malengo tuliyojiwekea kwa mwaka 2022, huku mapato yatokanayo na riba yakifika shs 28.6 bilioni ikiwa ni asilimia 86 ya malengo tuliyojiwekea".

Mazingira ya uendeshaji wa taasisi za fedha kwa mwaka 2022 yaliendelea kuwa tulivu huku thamani ya shilingi ya kitanzania ikiendelea kuimarika dhidi ya mataifa mengine, uchumi ukikua tena baada ya janga la Uviko-19, mfumuko wa bei ukiendelea kuwa chini kwa mwaka mzima, mafanikio katika sekta ya utalii na kufunguliwa kwa milango ya biashara kumechagiza kwa DCB kuendelea kufanya vizuri sokoni”,

Akizungumzia utendaji wa benki, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wa benki hiyo Bw. Isidori Msaki alisema DCB imekuwa makini katika kusimamia mikakati yake ya muda mrefu jambo linaloleta matokeo chanya ikiwemo kukua kwa mali za benki.

Mwaka 2022 mali za benki zimekuwa hadi kufikia shs 211 bilioni kutoka shs 192 bilioni kwa mkwa 2021, ukuaji ulioitoa benki yetu kutoka kwenye kundi la benki ndogo za biashara hadi kufikia benki za kati nchini."

DCB imeendelea kulinda thamani ya wanahisa wake kwa kukuza mapato yasiyotokana na riba kutoka asilimia 30 ya mapato yote mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 49 kwa mwaka 2022 ongezeko lililotokana na kuimarika kwa mifumo ya kidigitali inayochangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la miamala kwa zaidi ya asilimia 135”, alisema Bwana Msaki.

Akizungumzia baadhi ya vipaumbele vya benki hadi ifikapo mwaka 2025 kwa wanahisa waliofurika katika ukumbi wa JK Nyerere International Conference Centre jijini humo mkurugenzi huyo alisema ni kuhakikisha huduma za benki hiyo zinapatikana nchi nzima na hiyo inawezekana kwa kupitia hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha huduma zake kwa njia za kidigitali.

Tumeanzisha vituo vidogo vya huduma katika maeneo ya kimkakati, huduma za mawakala zaidi ya 700 nchini kote pamoja na mtandao wa matawi saba ndani na nje ya mkoa wa Dar es Salaam".

Benki yetu inalenga kuongeza wigo wa kutoa mikopo kwa njia za kidigitali kwa kiwango kikubwa ifikapo mwaka 2025, mwaka 2022 tulitoa mikopo isiyopungua shs 1.2 bilioni, mikopo hii ni salama zaidi kwa sababu inalipwa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja” , aliongeza mkurugenzi huyo.

Aidha mkurugenzi huyo alisema DCB inaendelea na mkakati wake wa kuhakikisha inapata faida mwaka hadi mwaka ili kufikia thamani ya hisa ya asilimia 18.9 na kuendelea kupunguza uwiano wa mikopo chechefu hadi kufikia chini ya asilimia 5 na pia kuongeza idadi ya wateja.

Aliwaomba wanahisa hao kuzidi kuwekeza ndani ya benki yao na kuzidi kuiamini menejimenti na bodi kwani uwekezaji wao umeleta faida kubwa kwa maisha ya watoto wa watanzania kwani umewawezesha kutoa msaada wa madawati kwa shule zenye uhitaji mkubwa jambo linalowapa amani watoto hao kusoma katika mazingira bora.

Ni kwa uwekezaji wenu wanahisa wetu uliotuwezesha pia kutoa elimu ya ujasiriamali kwa watanzania, elimu hii ni muhimu katika maendeleo ya biashara na maisha yao, tutaendelea kuimarisha ufanisi wa utendaji kazi wetu ili kuendelea kuleta matokeo chanya”, alisema.

Pamoja na kupata faida ya baada ya kodi ya sh 747 milioni 2022, na kwa kuzingatia sheria ya Benki Kuu, Bodi ya Wakurugenzi ya DCB imependekeza faida iliyopatikana ikaongeze fedha za wanahisa badala ya kutoa gawio.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages