TANZANIA COMMERCIA BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI UKUTA WA CHUO CHA TIBA MTWARA

 


Meneja wa Tanzania Commerical Bank Plc, Tawi la Newala Mkoa wa Mtwara Bw.Alex Minai (wapili Kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 100 ya Saruji kwa Mbunge wa jimbo la Newala Mhe. George Huruma Mkuchika iliyotolewa na Benki hiyo kwaajili ya kusaidia ujenzi wa ukuta wa chuo cha Uuguzi na Ukunga hii ni kampeni ya Benki ya TCB kuunga mkono juhudi za Serikali hususani Sekta ya Afya ili kuondoa changamoto zilizopo. Wengine pichani ni maofisa kutoka Chuoni hapo.
Share:

MAENDELEO BANK PLC YAJIVUNIA KUWEKA REKODI MPYA YA MAFANIKIO

 


2Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Biashara wa Maendeleo Bank, Emmanuel Mwaya akizungumza wanahabari pamoja na maofisa wa benki hiyo wakati akitangaza rekodi mpya ya mafanikio kuwa ni benki yenye faida kwa miaka nane mfululizo.hafla yakutangaza faida hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyi jijini Dar es Salaam.

1Baadhi ya maofisa wakiwa Maendeleo Bank wakifuatilia kwa umakini rekodi mpya ya mafanikio kuwa ni benki yenye faida kwa miaka nane mfululizo.hafla yakutangaza faida hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyi jijini Dar es Salaam.

Maendeleo Bank yaweka rekodi mpya ya mafanikio faida ya mwaka 2022 ni shilingi Bilioni 1.984 ambalo ni ongezeko la mara mbili Zaidi.

Akiungumza wakati akitangaza rekodi hiyo mpya Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Biashara wa Maendeleo Bank, Emmanuel Mwaya alieleza kuwa Maendeleo Bank Plc imeendelea kuwa benki yenye faida kwa miaka 8 mfululizo, kwa mujibu wa taarifa za fedha zilizokaguliwa za mwaka 2022, ikiwa na mambo yafuatayo;


Ameeleza kuwa “Faida kabla ya kodi: TZS 1.984 bilioni, ukuaji wa mwaka 181%

Faida baada ya kodi: TZS 1.415 bilioni, ukuaji wa mwaka wa 141%

Jumla ya amapato: TZS 12. bilioni, ukuaji wa mwaka wa 5%

Amana: TZS 72.0 bilioni ukuaji wa 11%

Mikopo: TZS 61.0 bilioni ukuaji wa 5%


 Ukuaji mzuri wa faida hizi umechangiwa Zaidi na timu iliyojitolea na ikiwa na lengo la kuifanya benki kuwa moja wapo ya wadau muhimu wa sekta ya kifedha katika uchumi. Ningependa kuangazia baadhi ya vichochezi vya faida ambavyo ni pamoja na; ukuaji wa jumla ya mapato kwa asilimia 26 mwaka hadi mwaka kutoka TZS 14.23 bilioni hadi TZS 17.97 bilioni mwaka 2022.

Benki pia imeendelea kuonyesha ufanisi mkubwa wa utendaji kazi, huku uwiano wa gharama kwa mapato ikiongezeka hadi 58% kutoka 74% katika kipindi kama hicho mwaka jana,ukiwa na nia ya kufikia kiwango elekezi kutoka benki kuu cha 55% ifikapo juni 2023.

Amana za wateja ziliongezeka kwa 11% kutoka TZS 70 bilioni mwaka 2021 hadi TZS 77.8 bilioni mwaka 2022 wakati mikopo ilongezeka kwa asilimia 5 kutoka TZS 57.7 bilioni hadi hadi TZS 60.6 bilioni mwaka 2022.


Mbinu iliyotumika katika uhamasishaji na ukuaji wa amana kwa wateja ulichangiwa kwa kiasi kikubwa uboreshaji wahuduma na bidhaa bunifu ambazo benki imekuwa ikitoa. Kuongezeka kwa bidhaa za kidijitali kama vile huduma za kibenki kwa simu, huduma za uwakala ambapo Zaidi ya benki mawakala 1300 (maendeleo Bank Wakala) Zimechangia ukuaji huu unaoshuhudiwa leo hii.


Akihitimisha wakati akitoa matokeo ya mwaka mzima ya benki hiyo mkuu wakitengo cha biashara Emmanuel Mwaya alisema”ninajivunia sana na ninashukuru kwa mafanikio yetu kama timu, nab ado nina Imani kubwa kwa ya  utekelezaji wa mkakati wetu, kuongezeka kwa mahusiano ya wateja wetu, ari ya utendaji wa wafanyakazi, na uongozi thabiti tutadumisha kasi hii ya ukuaji wa biashara yetu kuu.

Share:

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAFUTURISHA WATEJA WAKE JIJINI DAR ES SALAAM

    

Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi (watatu kushoto), wakiwaongoza wateja wa  pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo kupata mlo wa futari uliyoandaliwa na Tanzania Commercia Bank kwa ajili ya wateja wake  jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium towerMkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi (kushoto), akiongozana pamoja na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,  Sheikh Walid Alhad Omar na viongozi mbalimbali wa kidiniwa mkoa wa Dar es Salaam wakati wa hafla yakushiriki mlo wa futari uliyoandaliwa na Tanzania Commercia Bank kwa ajili ya wateja wake  jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium towerMkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa hafla yakushiriki mlo wa futari uliyoandaliwa na TCB kwa ajili ya wateja wake  jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium tower

Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,  Sheikh Walid Alhad Omar akitoa neno la shukrani kwa Mkurungenzi Mtendaji waTanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, kwakujali na kuona umuhimu wa mfungo wa Ramadani na kuandaa mlo wa futari kwaajili ya wateja wake wa Dar es Salaam.hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la milenium tower.Maofisa wa Tanzania Commercial Bank (TCB) pamoja na wateja wa benki hiyo wakishiriki mlo huo.

wafanya kazi wa TCB pamoja na wageni waalikwa wakiendelea kupata mlo 

Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank TCB,  Bi Chichi Banda (kushoto), akiwa kwenye picha ya pozi na Meneja Mawasiliano na Uhusiano  wa Benki hiyo Bi Gloria Mutta wakati wa hafla yakupata mlo wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo ambapo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally
Share:

TCB YATOA MSAADA WA MADAWATI MKOANI TABORA


IMG-20230402-WA0001
Mkuu wa wilaya ya Nzega Mh Naitapwaki Tukai akizungumza wakati wa hafla yakupokea msaada wa madawati 70 kwa shule ya msingi Nyasa iliyopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora yaliyotolewa na Tanzania Commercial Bank ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Benki hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Raia Dk Samia Suluhu Hassani katika sekta ya elimu. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika shuleni hapo
IMG-20230402-WA0000
Meneja wa Tanzania Commercia Bank Tawi la Nzega Shomari Shabani, (kushoto mwenyekoti jeusi), Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bi Veronica Ng'waru kushoto kwake na Maofisa kutoka TCB pamoja na wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Benki ya TCB kukabidhi msaada wa madawati 70 kwa shule ya msingi Nyasa iliyopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya kampeni Benki hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Raia Dk Samia Suluhu Hassani katika sekta ya elimu. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika shuleni hapo.

Tanzania Commercia Bank imetoa msaada wa madawati 70 kwa shule ya msingi Nyasa iliyopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, ikiwa ni muendelezo wa mpango wa benki hiyo katika kusaidia Serikali kuboresha ubora wa elimu hapa nchini.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi madawati hayo iliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja wa benki ya TCB tawi la Nzega Bw. Shomari Shabani alisema msaada huo ni sehemu ya jitihada ambazo benki hiyo imekuwa ikifanya kusaidia jamii inayoizunguka.

Alisema kuwa benki hiyo imekuwa ikijiweka mstari wa mbele kushirikiana na serikali kufanikisha mipango mbalimbali katika kuboresha sekta ya elimu, afya hapa nchini hatua inayopelekea kuwa ndio chachu ya maendeleo kwa sekta zote ikiwemo ya benki pia.

Mchango uliotolewa na Tanzania Commercia Bank wa kuchangia katika elimu unatokana na matumaini yetu kuwa bila kuwa na jamii iliyoelimika hata huduma za kibenki tunazozitoa zitadhoofika kutokana na ukweli kwamba biashara yetu hii inategemea sana mafanikio ya jamii inayotuzunguuka mafanikio ambayo tunaamini yataletwa na elimu,’’ alisema.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, mkuu wa Wilaya ya Nzega Mh. Naitapwaki Tukai pamoja na kuishukuru Tanzania Commercia Bank kwa msaada huo alisema msaada huo umepatikana kwa wakati muafaka kwa kuwa shule hiyo ipo kwenye mkakati wa kutafuta madawati zaidi kutokana na uhaba wa madawati unaoikabili shule hiyo.

Alisema shule hiyo sasa bado inakabiliwa na uhaba wa madawati zaidi na hivyo kutoa wito kwa taasisi na mashirika mengine kuiga mfano kwa Tanzania.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages