Benki ya DCB kupitia mfuko wake wa kuisaidia jamii wa DCB FOUNDATION wasaidia kampeni ya usafi wa mazingira Temeke.

      
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo (wa tatu kushoto) akifanya usafi pamoja na wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya DCB katika siku ya usafi ya mwisho wa mwezi iliyofanyika kiwilaya katika kata ya Keko jijini Dar es Salaam jana. DCB imeshiriki kampeni hiyo kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa DCB Foundation kwa kufanya usafi na kukabidhi msaada wa vifaa vya kufanyia usafi.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo (katikati), Meneja Mahusiano wa Benki ya Biashara ya DCB, Brino Londo (kulia) na Ofisa Masoko wa benki hiyo, Agness Ntabaye wakifanya usafi katika siku ya usafi ya mwisho wa mwezi iliyofanyika kiwilaya katika kata ya Keko jijini Dar es Salaam jana. DCB imeshiriki kampeni hiyo kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa DCB Foundation kwa kufanya usafi na kukabidhi msaada wa vifaa vya kufanyia usafi.
Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Mtinika (kulia) akipokea sehemu ya vifaa vya kufanyia usafi kutoka kwa Meneja Mahusiano wa Benki ya Biashara ya DCB, Brino Londo katika siku ya usafi ya mwisho wa mwezi iliyofanyika kiwilaya katika kata ya Keko jijini Dar es Salaam jana. DCB imeshiriki kampeni hiyo kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa DCB Foundation kwa kufanya usafi na kukabidhi msaada wa vifaa vya kufanyia usafi.
Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Mtinika (kulia) akipokea sehemu ya vifaa vya kufanyia usafi kutoka kwa Meneja wa Benki ya Biashara ya DCB Tawi la Temeke, Loyce Lwiza katika tukio la siku ya usafi ya mwisho wa mwezi lililofanyika kiwilaya katika kata ya Keko jijini Dar es Salaam jana. Benki ya DCB chini ya mfuko wake wa kusaidia jamii wa DCB Foundation wasaidia usafi wa mazingira ya Wilaya ya Temeke.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo (katikati) akishikana mikono na Meneja Mahusiano wa Benki ya Biashara ya DCB, Brino Londo baada ya kukabidhiwa vifaa vya kufanyia usafi katika siku ya usafi ya mwisho wa mwezi iliyofanyika kiwilaya katika kata ya Keko jijini Dar es Salaam jana. DCB imeshiriki kampeni hiyo kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa DCB Foundation kwa kufanya usafi na kukabidhi msaada wa vifaa vya kufanyia usafi.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo (wa tatu kushoto), Ofisa Masoko wa benki hiyo, Agness Ntabaye (wa pili kushoto) na Meneja Mahusiano wa Benki ya Biashara ya DCB, Brino Londo wakiwa pamoja wakati wa zoezi la siku ya usafi ya mwisho wa mwezi ambapo kiwilaya ilifanyika katika Kata ya Keko jijini Dar es Salaam. DCB imeshiriki kampeni hiyo kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa DCB Foundation kwa kufanya usafi na kukabidhi msaada wa vifaa vya kufanyia usafi.
Share:

DCB KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI

  
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Pamela Nchimbi (kushoto) akizungumza katika kongamano la wanawake lililoandaliwa na Kampuni ya ushauri wa masuala ya fedha ya Bridge Consult kwa udhamini mkuu wa Benki ya DCB jijini Dar es Salaam jana. Lengo la jukwaa hilo ni kubadilishana mawazo na kupeana ujuzi wa masuala ya kifedha, uwekezaji pamoja na maendeleo endelevu.
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Biashara ya DCB, Fortunata Benedict akitoa elimu ya maswala ya fedha katika kongamano la wanawake lililoandaliwa na Kampuni ya ushauri wa masuala ya Kifedha ya Bridge Consult kwa udhamini mkuu wa Benki ya DCB jijini Dar es Salaam jana. Lengo la jukwaa hilo ni kubadilishana mawazo na kupeana ujuzi wa masuala ya kifedha, uwekezaji pamoja na maendeleo endelevu.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Dk. Anna Abdul akizungumza katika kongamano la wanawake lililoandaliwa na Kampuni ya ushauri wa masuala ya kifedha ya Bridge Consult kwa udhamini mkuu wa Benki ya DCB jijini Dar es Salaam jana. Lengo la jukwaa hilo ni kubadilishana mawazo na kupeana ujuzi wa masuala ya kifedha, uwekezaji pamoja na maendeleo endelevu.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Pamela Nchimbi (wa pili kulia) akitoa elimu ya masuala ya maendeleo endelevu katika kongamano la wanawake lililoandaliwa na Kampuni ya ushauri wa masuala ya kifedha ya Bridge Consult kwa udhamini mkuu wa Benki ya DCB jijini Dar es Salaam jana. Lengo la jukwaa hilo ni kubadilishana mawazo na kupeana ujuzi wa masuala ya kifedha, uwekezaji pamoja na maendeleo endelevu. Kutoka kulia ni Mtaalamu wa masuala ya Kimaisha, Mihaela Marcu, Mshauri wa masuala ya afya kwa jamii, Naomi Serbantez na Mkurugenzi wa Mgahawa wa Terrace, Sarah Raqey.
Baadhi ya washiriki wakichangia mada katika kongamano la wanawake lililoandaliwa na Kampuni ya ushauri wa masuala ya kifedha ya Bridge Consult kwa udhamini mkuu wa Benki ya DCB jijini Dar es Salaam jana. Lengo la jukwaa hilo ni kubadilishana mawazo na kupeana ujuzi wa masuala ya kifedha, uwekezaji pamoja na maendeleo endelevu.
Share:

TANZANIA COMMERCIAL BANK YATINGA KIBABE KATAVI YAFUNGUA TAWI JIPYA

 .com/img/a/

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mh. Mwamvua Mrindoko (kushoto),  akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Tanzania Commercial Bank (TCB) katika Manispaa ya Mpanda  mjini mkoani Katavi,  kulia ni  Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Onesmo Buswelu  Meneja wa Tawi la Mpanda Julius Mlang'a  pamoja na maofisa wa kamati ya ulinzi ya mkoa..com/img/a/Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mh. Mwamvua Mrindoko wa  (kushoto),  akipokea kadi ya ATM kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB,  Sabasaba Moshingi, alipofungua akaunti alipoalikwa kuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tawi jipya la Tanzania Commercial Bank  lililofunguliwa katika Manispaa ya Mpanda  mjini mkoani Katavi jana  wengine pichani ni Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Onesmo Buswelu  Meneja wa Tawi la Mpanda Julius Mlang'a  pamoja na maofisa wa wengite kutoka TCB

.com/img/a/

Tanzania Commercial Bank (TCB)  imezindua tawi jipya Mkoa wa Katavi Wilaya ya Mpanda ikiwa ni jitihada za kusogeza huduma za kibenki kwa wateja na Wananchi kwa ujumla.

Tawi hilo la kwanza kwa taasisi za fedha kuzinduliwa Mkoa Katavi Wilaya ya Mpanda, limezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko .

 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Sabasaba Moshingi alisema huo ni mwendelezo wa Tanzania Commercial Bank katika kusogeza huduma kwa wateja wake.

 

Alisema tawi hilo jipya la Mpanda litarahisisha utoaji huduma za kibenki kwa wateja wake hali ambayo itapunguza mzunguko wa wananchi kuzifuata huduma za kibenki maeneo mengine ya mbali

Aliongeza kuwa Tanzania Commercial Bank (TCB) imezingatia shughuli za kiuchumi zinazoendeshwa Wilayani humo kwa  wafanyabiashar  wafugaji na wakulima wa na kufungua tawi hilo hivyo wateja hawatalazimika kwenda mjini kupata huduma za kibenki kama hapo awali

 

AlisemaTanzania Commercial Bank sio kwamba tu ni benki kubwa nchini, bali inatoa mchango mkubwa katika shughuli za kijamii  hasa kuinua elimu pamoja na Afya.

Kwa kuona umuhimu wa kusongeza huduma kwa wateja hasa maeneo ya vijijini Tanzania Commercial Bank (TCB) inaendelea kuwawezesha mawakala watakaosaidia kutoa huduma hizo jambo ambalo litasaidia kusogeza huduma kwa wateja wetu nchi mzima.

 

Aliongeza, kwa sasa Benki hiyo ina matawi  82 Mawakala tunao zaidi 3,800  mashine zakutolea pesa ATM zetu tunazojitegemea Kama TanzaniaCommercial Bank ni 84 lakini zile ATM ambazo tupo chini ya Umoja Switch ni zaidi ya 250.

 

Akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Tawi jipya la Tanzania Commercial Bank  Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko  ameupongeza uongozi wa Tanzania CVommercial Banki  kwa kuja kuwekeza katika  Mkoa huu na anaamini kwa wingi wa watu waliojitikeza katika tukio hili watakwenda kufungua akaunti.

 

Mrindoko pia ameipongeza  Tanzania Commercial  Banki (TCB)  kwa kufika Mkoani Katavi na kuwakaribisha kwani fursa zipo nyingi katika mkoa huo zikiwemo za uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara pamoja na mazao mengine  ya kimkakati.

 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliuhakikishia uongozi wa Tanzania Commercial  Banki (TCB)  kwamba Katavi ni mkoa unaokua kwa kasi sana kutokana na shughuli za uzalishaji na za kimaendeleo hivyo huduma ya  Tanzania Commercial Bank kwakfungua tawi hilo limekuja wakati muafaka

 

“Kuzinduliwa kwa Tawi la Tanzania Commercial Bank (TCB)  hapa Katavi maana yake ni kwamba huduma za kibenki zitapatikana kwa urahisi zaidi hivyo wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara wa Katavi jitokezeni kwa wingi wenu kuchangamkieni  fursa hii na kuja kufungua akaunti na kufanya miamala mengine kama kulipa kodi alisisitiza Mrindoko

Share:

KWAHILI WALILOFANYA TANZANIA COMMERCIAL BANK MUNGU ANAWAONA

 

.com/img/a/Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Prof: Faustin Kamuzora (wa pili kulia), akikata utepe wakati akikabidhiwa msaada wa jengo la madarasa, Vyoo, pamoja na Madawati mapya 50 lililokarabatiwa na Tanzania Commercial Bank (TCB) Hafla ya makabidhiano hayo yalifanyika katika Shule ya Msingi Kitunga iliyopo wilaya ya Muleba mkoani Kagera kushoto ni Mkurugenzi wa BiasharaWateja Wakubwa wa Tanzania Commercial Bank Adolfina William, Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki hiyo Muondakweli Kaniki pamoja na Mkuu wa Shule hiyo Hashim Kibaiza, Tanzania Commercial Bank kupitia mpango wake wa kusaidia jamii (CSR) imetumia zaidi kiasi cha shs milioni 36 kukamilisha ujenzi wa Madawati pamoja na choo   Madawati pamoja na choo cha walimu chenye matundu mawili 

.com/img/a/


Mkurugenzi wa Biashara Wateja Wakubwa wa Tanzania Commercial Bank Adolfina William,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa jengo la madarasa, Vyoo, pamoja na Madawati mapya 50 lililokarabatiwa na Tanzania Commercial Bank (TCB) Hafla ya makabidhiano hayo yalifanyika katika Shule ya Msingi Kitunga iliyopo wilaya ya Muleba mkoani Kagera kupitia mpango wake wa kusaidia jamii (CSR) imetumia zaidi kiasi cha shs milioni 36 kukamilisha ujenzi wa madarasa Madawati pamoja na choo.

.com/img/a/

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Prof Faustin Kamuzora amewataka wazazi na wakazi wa Mkoa wa Kagera kusaidiana na serikali katika kutatua changamoto za walimu.

Hayo ameyasema wakati wa kukabidhiwa ukarabati wa madarasa, madawati na Choo cha matundu mawili kilichojengwa na Tanzania Commercial Bank (TCB) kitakachosaidia kuboresha mazingira rafiki ya walimu kufundisha.

Prof Kamuzora amesema, wazazi na walezi wengi wa watoto wamesoma katika shule hiyo ila walimu wamekuwa na changamoto ya mazingira ambayo si rafiki na inaweza kupelekea walimu hao kuondoka na kwenda sehemu zingine.

“Walimu hawa wakiondoka tutakosa wa kuwafundisha watoto wetu, nyie wazazi wengi mmesoma hapa na mtu aliyesoma miaka ya nyuma akija hapa atapashangaa ila tusiwaachie serikali peke yake ila tushirikiane pamoja na wadau wa elimu pia,” amesema Prof Kamuzora.

Amesema, Benki ya TCB wamekuja na kujenga choo ila hii isiwe mwisho katika kutoa msaada bali walimu pia wanahitaji elimu ya fedha sababu wengi wamekuwa wanaingia katika mikopo inayowadidimiza kimaslahi.

Aidha, Prof Kamuzora ameitaka elimu ya fedha kuanza kutolewa mashuleni ili wanafunzi waanze kuwa na uelewa mkubwa na itawasaidia baadae.

“Na kwa upande wa walimu, haimaanishi ndio unajua kila kitu nao ni muhimu kuwa uelewa juu ya elimu ya fedha,”Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Tanzania Commercial Bank Adolphina William amesema wananchi wa Kijiji cha Msole wameweza kufurahia mradi wa kukarabati madarasa, kukabidhi madawati na walimu kupata choo cha kisasa.



Amesema, mradi huo uliofanyika katika Shule ya Kituga umeweza kugharimu kiasi cha Milioni 36.3 hadi kukamilika kwake.



“Tanzania Commercial Bank imekuwa inatenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kusaidia jamii na mwaka huu tumetenga takribani Milioni 500 na kujikita zaidi katika sekta ya elimu na afya,” amesema Adolphina.


Kwa upande wa Mkuu wa shule Hashim kibaiza ameishukuru Tanzania Commercial Bank kwa kufanikisha mradi huo ambao utaenda kuboresha mazingira bora ya walimu katika kuinua taaluma.

Ameomba wadau mbalimbali kuiga mfano kwa Tanzania Commercial Banki ili kuendelea kujikita katika kusaidia jamii ikiwemo shule yao ya Kitunga.



Tanzania Commercial Bank imekabidhi ukarabati wa madarasa mawili, ujenzi wa choo cha walimu pamoja na kuchangia madawati 50 katika shule ya Msingi Kitunga iliyopo Muleba, mkoani Kagera mradi umegharimu Milioni 36,274,500 pesa za kitanzania.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages