LG Electronics yafungua duka jipya la kisasa jijini Dar es Salaam

Kutoka Kushoto ni Meneja Mkaazi wa kampuni ya LG Tanzania, Aashim Wadhw, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania (MeTL) Indrabhuwan Singh, na Mkurugenzi wa F&S, Frank Rwamlima, pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya (MeTL) Fatma Dewji, wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi Duka jipya la LG Electronics Mlimani City, Dar es Salaam.”

Dar es Salaam, Septemba 24, 2025 – Kampuni ya LG Electronics Kanda ya Afrika Mashariki imezindua duka jipya la bidhaa zake (brandshop) katika Kituo cha Ununuzi cha Mlimani City jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha uwepo wake kwenye soko la Afrika Mashariki.

Duka hilo jipya limefunguliwa kwa ushirikiano na kampuni ya F&S pamoja na msambazaji rasmi wa bidhaa za LG nchini, METL. Hatua hiyo inalenga kuongeza urahisi wa upatikanaji wa bidhaa za LG huku wateja wakipewa huduma za kisasa zenye viwango vya kimataifa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Meneja wa LG Electronics Tanzania, Aashim Wadhwa alisema“Duka hili jipya ni uthibitisho wa dhamira ya LG kuendelea kuwapatia wateja wa Tanzania teknolojia za kisasa na huduma bora zaidi. Dar es Salaam ni jiji lenye kasi kubwa ya ukuaji, na tunaona fursa kubwa ya kushirikiana na ukuaji huo kwa kuwakaribia zaidi wateja wetu na kuhakikisha wanapata msaada wa baada ya mauzo kwa kiwango cha juu.”

Katika duka hili, wateja wataweza kushuhudia na kutumia moja kwa moja ubunifu wa hivi karibuni wa LG, ikiwemo vifaa vya nyumbani (home appliances), vifaa vya burudani majumbani (home entertainment systems) na suluhisho za hali ya hewa (HVAC). Pia kutakuwa na huduma ya haraka, usaidizi wa baada ya mauzo na uhakika wa kupata bidhaa halisi.

Mwakilishi wa F&S alisema Frank Mwamlima-F&S Tunafurahia kushirikiana na LG na METL kuwaletea Watanzania uzoefu wa ununuzi wa kisasa.

 Duka hili litawawezesha wateja kuona na kutumia bidhaa za LG moja kwa moja, na hivyo kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi ya ununuzi katika mazingira ya kiwango cha kimataifa.

”kwa upande wake, mwakilishi wa METL aliongeza kuwa“Uzinduzi huu ni ishara ya uhusiano unaozidi kukua kati ya METL na LG East Africa. LG ni chapa inayotambulika duniani kwa ubora na uimara wake, na duka hili linaonesha dhamira yetu ya pamoja ya kuwaletea Watanzania bidhaa zenye viwango vya juu, imara na za kuaminika.”

Kwa mujibu wa tafiti, soko la vifaa vya nyumbani Afrika Mashariki linatarajiwa kukua kwa wastani wa asilimia 6.55 kila mwaka, huku familia nyingi zikielekeza kipaumbele katika teknolojia endelevu na zenye kuokoa gharama.


Duka jipya la LG jijini Dar es Salaam ni sehemu ya mkakati mpana wa upanuzi wa kampuni hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki, ambapo tayari imejitanua katika nchi mbalimbali zikiwemo Kenya, Sudan, Ethiopia, Tanzania, Somalia, Uganda, Zambia, Sudan Kusini na Rwanda. Kupitia uwekezaji huu, LG inalenga kuongeza upatikanaji wa bidhaa zake, kuboresha huduma kwa wateja na kuimarisha uzoefu wa matumizi ya teknolojia za kisasa.

Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (277) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (119) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages