Pages

Thursday, April 30, 2026

RC SINGIDA APONGEZA JITIHADA ZA NBC KUCHOCHEA MAPINDUZI YA KILIMO

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi. Halima Dendego (wa tatu kulia), akionesha baadhi ya zawadi zinazotolewa kwa washindi kampeni ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde” inayoratibiwa na Benki ya NBC. Wengine pichani ni Mkuu wa Kanda ya Kati wa NBC, Bw. Miraji Msuya (wa tatu kushoto), Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Bw. Benjamini Nkaka (wa pili kushoto) Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Wakulima wa NBC, Bw. Raymond Urassa (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Mkoa wa Singida (SIFACU) Bw. Julius Kitundu (kulia) na Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Singida Bi. Nuria Gulamali (wa pili kulia).
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi. Halima Dendego (katikati), akipokea zawadi maalum ya picha yake kutoka kwa wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Kanda ya Kati wa NBC, Bw. Miraji Msuya (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde” inayoratibiwa na Benki ya NBC.

Singida, Aprili 30, 2026 — Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi. Halima Dendego, amepongeza mchango wa wadau mbalimbali, hususan Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuharakisha maendeleo ya sekta ya kilimo. Ameitaja kampeni ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde” kuwa kichocheo muhimu cha ustawi wa wakulima na ukuaji wa uchumi wa mkoa huo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo uliofanyika jana mkoani Singida, Bi. Dendego alisema kuanzishwa kwa mpango huo kwa mara ya kwanza katika mkoa huo ni hatua muhimu inayosaidia kufanikisha malengo ya Serikali ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kimkakati pamoja na kuinua kipato cha wakulima.
Hafla hiyo iliwaleta pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika, wakulima, pamoja na wadau wengine katika mnyororo wa thamani wa kilimo. Uongozi wa NBC uliwakilishwa na Mkuu wa Idara ya Bima, Bw. Benjamini Nkaka, na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Wakulima, Bw. Raymond Urassa, wakishirikiana na timu ya maofisa wa benki hiyo akiwemo Mkuu wa Kanda ya Kati, Bw. Miraji Msuya.

Kwa mujibu wa Bi. Dendego, kampeni hiyo inaendana na mafanikio ya jitihada za Serikali ambazo tayari zimeanza kuzaa matunda. Alitaja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na usajili wa zaidi ya asilimia 92 ya wakulima mkoani Singida, utoaji wa ruzuku za pembejeo kama mbegu na mbolea, pamoja na uwekezaji katika huduma za ugani na kilimo cha umwagiliaji.

Kampeni ya NBC Shambani inakuja kuimarisha juhudi hizi kwa kuchochea ujumuishaji wa kifedha kwa wakulima. Hii ni hatua muhimu kuelekea kilimo chenye tija na chenye manufaa kwa wananchi mmoja mmoja, kaya na mkoa kwa ujumla,” alisisitiza Bi. Dendego.

Aidha, aliwahimiza wakulima kuchangamkia fursa zinazotolewa na kampeni hiyo, ikiwemo akaunti zisizo na makato ya kila mwezi, upatikanaji wa mikopo ya pembejeo na zana za kilimo, elimu ya fedha, pamoja na huduma za bima ya afya na mazao.

Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo, Bw. Nkaka alisema NBC inaendelea kubuni suluhisho za kifedha bunifu ili kuunga mkono azma ya Serikali ya kuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo kutoka asilimia 5 hadi 10 ifikapo mwaka 2030. Aliongeza kuwa benki hiyo pia inawekeza katika utoaji wa elimu ya fedha, huduma za kidijitali, pamoja na bima zinazolenga kupunguza hatari kwa wakulima.

Kwa upande wake, Bw. Urassa alisema kampeni hiyo ya miezi minne inalenga wakulima wa mazao ya dengu, choroko, mbaazi, soya na ufuta. Alieleza kuwa wakulima wana nafasi ya kushiriki binafsi au kupitia vyama vya ushirika na kushinda zawadi mbalimbali, zikiwemo pikipiki na kompyuta mpakato (laptops).

Lengo kuu ni kuwahamasisha wakulima kutumia mifumo rasmi ya kifedha kwa kutunza fedha zao benki. Tunawakaribisha kufungua akaunti za NBC Shambani ili waweze kunufaika na huduma na fursa hizi,” alibainisha.

Baadhi ya wakulima walioshiriki katika hafla hiyo walieleza matumaini yao juu ya kampeni hiyo, wakiwahimiza wenzao kuitumia kikamilifu ili kunufaika na huduma za kifedha, elimu, bima pamoja na zawadi zinazotolewa.

Uzinduzi wa kampeni ya Wekeza NBC Shambani Ushinde unaashiria hatua mpya katika juhudi za kukuza sekta ya kilimo mkoani Singida. Kupitia ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi, wakulima wanapata fursa ya kuimarisha uzalishaji wao, kuongeza kipato na kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa taifa.

Tuesday, April 28, 2026

YAS UNVEILS ‘ZINGATIA MTANDAO WA VIWANGO’ CAMPAIGN FOLLOWING MAJOR INFRASTRUCTURE INVESTMENT

 

Chief Technology and Information Officer at Yas Tanzania, Emmanuel Mallya (right), with the Head of Brand and Communications at Yas, Anna Loya (left), pose for a photo during the official launch of its new identity dubbed ‘Zingatia Mtandao wa Viwango’, unveiled on April 28, 2026, in Dar es Salaam. The campaign encourages Tanzanians to use high-quality, fast, and reliable network services, following Yas’s significant investment in digital infrastructure across the country.

Dar es Salaam, April 28, 2026 — Telecommunications company Yas Tanzania has officially launched its new brand campaign, “Zingatia Mtandao wa Viwango” (Experience a quality network), signaling a strategic shift toward enhancing customer experience as demand for reliable digital connectivity continues to rise across the country.

The campaign reflects the company’s broader ambition to position itself strongly within Tanzania’s increasingly competitive telecom sector—where network quality, speed, and coverage are now critical differentiators.

From Infrastructure to Experience

According to Yas, the campaign follows a cumulative investment of over TZS 1 trillion in network expansion and modernization. This significant capital outlay has enabled the company to expand its coverage footprint while improving service reliability nationwide.

Speaking during the launch in Dar es Salaam, the company’s Chief Technology and Information Officer, Emmanuel Mallya, emphasized that the initiative marks a transition from infrastructure development to delivering tangible value to customers.

He noted that after years of building and upgrading network capacity, the company is now focused on ensuring users fully benefit from improved connectivity in their everyday activities.
Supporting Tanzania’s Digital Economy

Yas says its network is designed to support a wide range of use cases—from online business and digital finance to education, entertainment streaming, and agriculture—underscoring the growing importance of connectivity in Tanzania’s socio-economic development.

The company currently operates over 4,800 network sites nationwide, approximately 1,000 more than its nearest competitor. This infrastructure allows Yas to reach more than 95% of the population, including rural and previously underserved areas.

In parallel, the company has invested heavily in fiber optic infrastructure to strengthen backbone capacity and enhance data transmission speeds. Yas has also standardized 4G connectivity across all its sites, while rolling out 5G services in select strategic towns to meet rising data demand and support emerging digital applications.

Industry Recognition and Competitive Edge

Yas’ network performance has gained international recognition from Ookla, a global authority in internet performance analysis. Based on data from its Speedtest platform, Yas has been ranked as the fastest network in Tanzania for three consecutive years.

However, Mallya stressed that the new campaign goes beyond speed, focusing on broader elements of network quality, including consistency, accessibility, and reliability.

Improved network performance, he noted, enables users to:
  • Conduct online business transactions more efficiently
  • Access digital learning platforms without disruption
  • Enjoy seamless entertainment streaming with minimal buffering
Shifting Market Dynamics

The launch comes at a time when Tanzania’s telecommunications sector is undergoing a notable shift. Operators are increasingly competing on service experience rather than pricing, as consumers become more discerning about network quality.

With the “Zingatia Mtandao wa Viwango” campaign, Yas aims to influence consumer behavior by encouraging users to prioritize quality connectivity when choosing service providers—particularly as digital services become central to both economic participation and daily life.

Multi-Platform Rollout

The campaign will be executed across multiple channels, including mass media, digital platforms, and on-ground activations, with messaging designed to highlight the real-life benefits of a high-quality network.
A Broader Industry Shift

Ultimately, the launch underscores a wider transformation within the telecommunications industry: connectivity is no longer just a basic utility—it is now a critical enabler of productivity, innovation, and inclusive growth.

As Tanzania continues to embrace digital transformation, investments in high-quality network infrastructure are expected to play a pivotal role in shaping the country’s economic future.

Monday, April 27, 2026

ABSA YATAJWA MIONGONI MWA CHAPA 3 BORA ZA BENKI BARANI AFRIKA, THAMANI YA CHAPA YAVUKA R30 BILIONI (TZS TRILIONI 4.74), YASHIKA NAFASI 5 ZA JUU KATIKA SEKTA ZOTE AFRIKA KUSINI

Johannesburg: Absa Group imetajwa miongoni mwa chapa tatu za benki zenye thamani kubwa zaidi barani Afrika, huku pia ikishika nafasi ndani ya tano bora za chapa zenye thamani kubwa zaidi nchini Afrika Kusini katika sekta zote na makundi yote.

Hii ni baada ya thamani ya chapa yake kuvuka R30 bilioni (TZS trilioni 4.74) kwa mara ya kwanza. Kwa mujibu wa ripoti inayotolewa na kampuni ya kimataifa ya ushauri wa thamani ya chapa ‘Brand Finance South Africa 2026’, thamani ya chapa ya Absa imeongezeka hadi kufikia R30.6 bilioni (TZS trilioni 4.83), ikiwa ni ongezeko la asilimia 12 mwaka hadi mwaka, na kuimarisha nafasi ya Kundi hilo kama mtoa huduma za kifedha anayeongoza barani Afrika.

Hatua hii muhimu inaakisi mafanikio ya mkakati wa Absa wa “Stori yako ina Thamani”, uliozinduliwa miaka miwili iliyopita ukiwa na lengo la kumweka mteja katikati ya shughuli za biashara. Mkakati huu, unaozingatia uelewa wa kibinadamu na utoaji wa huduma zilizounganishwa kwa urahisi, umepata mwitikio mkubwa barani Afrika, ukiongeza umuhimu wa chapa, kuimarisha uhusiano na wateja, na kujenga imani imara zaidi.

Katika kipindi cha mwaka uliopita, Absa imeongeza kasi ya ukuaji unaoongozwa na mahitaji ya wateja, kuimarisha uwepo wake barani, na kuharakisha uwezo wake katika masuala ya kidijitali na ubunifu. Uwekezaji unaoendelea katika kuboresha mifumo na kupanua huduma zinazotanguliza matumizi ya kidijitali umeimarisha uwezo wa Kundi kutoa huduma za benki zilizounganishwa na zenye urahisi. Wakati huo huo, Absa imeendelea kuimarisha nafasi yake kama mshirika wa taasisi anayeaminika katika masoko muhimu.

Sydney Mbhele, Afisa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano ya Kundi la Absa, alisema; “Kutambuliwa miongoni mwa chapa bora za benki barani Afrika na kushika nafasi ya tano ya juu nchini Afrika Kusini ni uthibitisho mkubwa wa imani ambayo wateja wetu wanaweka kwetu, pamoja na nguvu ya chapa yetu katika soko lenye ushindani mkubwa. Kielezo chetu cha nguvu ya chapa kinaendelea kuonesha uimara na kuboreka, huku viashiria muhimu kama ‘Brand Love’ vikikua kwa kasi. Hii inaonesha uhusiano wa maana tunaoujenga na wateja wetu pamoja na matokeo chanya ya mkakati wetu unaoweka mteja mbele na unaoendeshwa na teknolojia ya kidijitali.

Miaka miwili iliyopita tulianzisha ‘Stori yako ina Thamani’ kama kauli thabiti ya kumweka mteja katikati ya kila tunachofanya, leo, tunaona ahadi hiyo ikitimia kupitia ushiriki mkubwa zaidi, mahusiano imara, na uzoefu wa chapa ulio karibu zaidi na maisha ya watu katika masoko yetu,” aliongeza.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, chapa imara za benki zina jukumu muhimu katika kujenga imani na uimara wa uchumi wa Afrika Kusini. Absa inaendelea kujitolea kutekeleza jukumu hili kwa kuzingatia utoaji wa suluhisho zilizounganishwa na zinazotanguliza huduma za kidijitali ili kusaidia wateja, taasisi na jamii kukabiliana na mazingira yanayobadilika kwa kasi.

Utendaji huu mzuri wa chapa unaungwa mkono na matokeo imara ya kifedha. Absa Group iliripoti ongezeko la asilimia 12 la faida kuu hadi kufikia R24.8 bilioni, likichangiwa na faida kubwa kabla ya makadirio ya hasara na kupungua kwa mikopo chechefu, hali inayoonesha utekelezaji makini na mfumo thabiti wa uendeshaji.

Kundi pia lilirekodi ongezeko kubwa la matumizi ya huduma za kidijitali, ambapo idadi ya wateja wanaotumia huduma hizo iliongezeka kwa asilimia 11 na kufikia milioni 3.6 katika mwaka wa fedha 2025. Hii inaashiria mwelekeo unaoendelea wa matumizi ya huduma rahisi za benki kupitia programu za simu ya mkononi.

Ukuaji huu umechangiwa na ongezeko la watumiaji wa Absa Banking App, ambapo watumiaji hai katika sekta ya benki kwa wateja binafsi na wateja maalumu waliongezeka kwa asilimia 14 hadi kufikia milioni 2.9. Upakuaji mpya wa programu uliongezeka kwa asilimia 94, ukichangiwa na maboresho endelevu, utendaji bora zaidi, na uzoefu rahisi kwa mtumiaji.

Absa inatoa shukrani zake kwa wafanyakazi wake, wateja na wadau wote ambao mchango wao umewezesha kufikiwa kwa mafanikio haya muhimu.

Kuvuka hatua hii si tu kielelezo cha tulipo leo, bali ni ishara ya mwelekeo wetu wa baadaye,” alihitimisha Mbhele.

Dhamira yetu ya ‘Kuiwezesha Afrika ya Kesho Pamoja’ inaonesha kujitolea kwa kina kushirikiana na watu na jamii tunazozihudumia katika kujenga maendeleo. Kila ubunifu, kila ushirikiano na kila mawasiliano na mteja ni sehemu ya simulizi kubwa zaidi, ambapo tunajenga mustakabali jumuishi, imara na wenye fursa nyingi kwa bara la Afrika, hatua moja baada ya nyingine.”

Friday, April 24, 2026

NuLife Advanced Fertility Centre Strengthens Its Position as a Leading Fertility Provider in Tanzania

Dar es Salaam, Tanzania – April 24, 2026 – NuLife Advanced Fertility Centre continues to establish itself as a leading provider of advanced fertility care in Tanzania, delivering world-class reproductive solutions supported by strong clinical outcomes and international expertise.

Over the past four years, the clinic has performed a significant successful number of cycles (OPU +FET), resulting in more than 400 babies delivered through A.R.T with an overall success rate of 65%.

NuLife Advanced Fertility Centre offers a full range of services including IVF, IUI, PRP, and TESA/PESA procedures, alongside advanced genetic testing (PGT-A) and a cryopreservation program. They are one stop solution to all gynecological issues like fibroids, cysts all the way up to mild, moderate and severe endometriosis. They specialize in surgical skills using keyhole surgery.
As part of its commitment to excellence, the clinic partners with internationally renowned fertility expert Dr. Nayana Patel, working alongside NuLife’s own leading specialist, Dr. Madhav. These ongoing collaborations include knowledge transfer, technology transfer and skill set up gradation.

A representative from NuLife Fertility Centre stated: "We are committed to making high-quality fertility care accessible while maintaining international standards, combining advanced technology with compassionate, patient-centered care."
About Nulife Fertility Center

NuLife Fertility Centre is a leading fertility clinic based in Masaki, Dar es Salaam, offering advanced reproductive services including IVF, IUI, genetic testing, and fertility preservation. With a strong track record of success and a commitment to excellence, NuLife delivers personalized care supported by modern technology and experienced medical professionals.

Wednesday, April 22, 2026

BENKI YA ABSA NA THE RUNNERS CLUB WAZINDUA MBIO ZA ABSA DAR CITY MARATHON 2026

 

Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga (kulia), akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi rasmi wa mbio za mwaka huu za Absa Dar City Marathon zinazotarajiwa kutimua vumbi jijini Dar es Salaam, Mei 17 mwaka huu. Katikati ni Makamu wa Rais wa The Runners Club, Bw. Godphrey Mindu, waratibu wa mbio hizo na kushoto ni Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Jesca Nassari, ambao ni mmoja wa wadhamini. Benki ya Absa ni mdhamini mkuu wa tukio mbio hizo.

Benki ya Absa Tanzania kwa kushirikiana na The Runners Club, wamezindua rasmi mbio za Absa Dar City Marathon 2026, zinazotarajiwa kufanyika Mei 17 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Tukio hilo linatarajiwa kuvutia zaidi ya washiriki 5,000 kutoka ndani na nje ya nchi, likilenga kuhamasisha mazoezi ya mwili, mshikamano wa kijamii pamoja na maisha yenye afya.

Mashindano ya mwaka huu yatakuwa na makundi matatu ya mbio; kilomita 21.1 (Nusu Marathon), kilomita 10 na kilomita 5. Usajili tayari umefunguliwa kupitia majukwaa rasmi ya usajili, huku wakimbiaji wa viwango vyote, kuanzia wanariadha wakongwe, wapenda afya, hadi washiriki wa burudani, wakihimizwa kujiandikisha na kushiriki katika sherehe hii ya kipekee jijini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga, alisema:

Katika Absa, tunaamini katika kuleta athari chanya katika jamii tunazozihudumia. Absa Dar City Marathon siyo tu mbio, bali ni jukwaa linalokuza afya, umoja na ustawi wa jamii, tunajivunia kushirikiana na The Runners Club kuandaa tukio hili na tunawahimiza Watanzania wote kukuuenzi mtindo huu wa maisha wenye kujishughulisha kimwili.

Naye Mratibu wa mbio hizo na Makamu wa Rais wa The Runners Club, Godphrey Mindu, aliongeza:

Marathon hii inaakisi ukuaji mkubwa wa utamaduni wa kukimbia nchini Tanzania, tumeona jamii zikija pamoja kupitia mazoezi ya viungo, na tukio hili ni sherehe ya roho hiyo, tunatarajia kuwapokea wakimbiaji wa viwango vyote na kutoa uzoefu wa hali ya juu siku ya mashindano.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam, Felix Donald, alisema:

Matukio kama Absa Dar City Marathon yana mchango mkubwa katika kuvumbua na kukuza vipaji vya riadha huku yakihamasisha afya na nidhamu. Kama chama, tunaunga mkono kikamilifu juhudi zinazokuza mfumo wa riadha na kuhamasisha kizazi kijacho cha wakimbiaji.

Wawakilishi kutoka vilabu mbalimbali vya kukimbia walisisitiza umuhimu wa tukio hilo kwa jamii. Johnson Mbunda “Balozi” kutoka Goba Roads Runners alisema kuwa marathon hiyo “siyo tu mbio, bali ni tukio linalowaunganisha wakimbiaji kutoka kote nchini kukutana, kuwasiliana na kujenga urafiki wa kudumu.” Mwanachama wa Kigamboni Runners alielezea mbio hizo kama “mkusanyiko wa kila mwaka unaotoa fursa ya kuungana tena na marafiki na familia, kukutana na watu wapya na kuiona Dar es Salaam kwa mtazamo wa kipekee.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wanachama wa vilabu mbalimbali ikiwemo Tabata Runners, TOT Runners, Absa Running Club, Salasala Runners na Kigamboni Runners, pamoja na wadhamini wa tukio hilo. Uwepo wao uliashiria kukua kwa utamaduni wa kukimbia na mshikamano mkubwa wa jamii unaoliunga mkono tukio hili.
Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga (wa tatu kutoka kushoto), na Meneja Matukio na Huduma za Jamii wa benki hiyo, Bi. Abigail Lukuvi (kushoto kwake), wakionesha fulana zitakazovaliwa na wakimbiaji wa mbio za mwaka huu za Absa Dar City Marathon katika hafla ya uzinduzi wa maandalizi ya mbio hizo, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kutoka kulia ni Makamu wa Rais wa The Runners Club, Bw. Godphrey Mindu, waandaaji wa mbio hizo na baadhi ya wawakilishi wa kampuni wadhamini. Benki ya Absa ni mdhamini mkuu wa Absa Dar City Marathon.

BENKI YA ABSA KUENDELEZA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA

  

Mtendaji Mkuu wa Benki ya Absa wa Afrika Mshariki, Bw. Saviour Chibiya (wa tatu kutoka kulia), akiwa katika mazungumzo na Bw. Rumisho Shikonyi (wa tatu kutoka kushoto), Meneja Mkazi wa taasisi ya kifedha ya Watu Credit Tanzania, alipofanya ziara katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam jana, akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa pili kutoka kulia), pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo. Mazungumzo yao yalilenga kuimarisha ushirikiano, kufungua fursa mpya, na kuendeleza ukuaji endelevu. Bw. Chibiya kwa sasa yupo Tanzania kwa ziara yake rasmi ya kikazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa tatu kutoka kushoto), akizungumza na Bw. Rumisho Shikonyi (kulia), Meneja Mkazi wa taaisis ya Watu Credit Tanzania, wakati Mtendaji Mkuu wa Benki ya Absa wa Afrika Mashariki, Bw. Saviour Chibiya (wa pili kutoka kushoto), akifanya ziara katika kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Mazungumzo yao yalilenga katika kuimarisha ushirikiano, kufungua fursa mpya, na kuendeleza ukuaji endelevu. Bw. Chibiya kwa sasa yupo Tanzania kwa ziara yake rasmi ya kikazi. Kushoto ni Ofisa Fedha Mkuu wa Absa Bank Tanzania, Bw. Bernard Tesha.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Absa wa Afrika Mashariki, Bw. Saviour Chibiya (kushoto), akimsikiliza kwa makini Bw. Rumisho Shikonyi (kulia), Meneja Mkazi wa taasisi ya Watu Credit Tanzania, wakati wa ziara yake katika taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana. Alifuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Bank Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kusoto kwake), pamoja na viongozi wengine waandamizi wa benki hiyo. Mazungumzo yao yalilenga katika kuimarisha ushirikiano, kufungua fursa mpya, na kuendeleza ukuaji endelevu. Bw. Chibiya kwa sasa yupo Tanzania katika ziara yake rasmi ya kikazi.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Absa wa Afrika Mashariki, Bw. Saviour Chibiya (wa tatu kushoto), Bw. Obedi Laiser (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Bank Tanzania; na Bw. Rumisho Shikonyi (wa nne kutoka kushoto), Meneja Mkazi wa Watu Credit Tanzania, wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na maafisa waandamizi kutoka taasisi zote mbili baada ya ziara ya Bw. Chibiya katika taasisi hiyo ya fedha, jijini Dar es Salaam jana.

Wednesday, April 15, 2026

BENKI YA ABSA TANZANIA YAONGEZA KIWANGO CHA MKOPO BINAFSI NA MUDA WA MAREJESHO KUWAWEZESHA WAFANYAKAZI WA SEKTA BINAFSI NA YA UMMA

Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benkiya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere (katikati), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Jisogeze na Mkopo wa hadi TZS 200m”, inayolenga wafanyakazi wa sekta binafsi na umma, jijini Dar es Salaam leo. Pichani kushoto ni Bw. Aron Luhanga, Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano na kulia ni Bw. Heristraton Genesis, Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi.

Benki ya Absa Tanzania imetangaza maboresho katika bidhaa yake ya Mkopo Binafsi Usio na Dhamana kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na Umma wanaopokea mishahara, hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa mikopo nafuu na yenye masharti nafuu zaidi ikiwa ni sehemu ya dhamira ya benki hiyo ya kuiwezesha Africa ya Kesho, pamoja, hatua Moja baada ya nyingine.

Chini ya maboresho hayo mapya, wafanyakazi wa sekta binafsi na umma sasa wanaweza kupata mikopo hadi shilingi milioni 200 za Kitanzania, kutoka kiwango cha awali cha shilingi milioni 150. Aidha, muda wa marejesho umeongezwa hadi miezi 96 (sawa na miaka 8), huku mkopo huo ukiendelea kutolewa bila hitaji la dhamana yoyote.

Huduma hii inawahusu wateja waliopo tayari benki (ETB) pamoja na wateja wapya (NTB), kwa kuzingatia taratibu za kawaida za tathmini ya uwezo wa mkopo.

Maboresho haya yanafuatia hatua kama hiyo iliyotekelezwa awali kwa wafanyakazi wa sekta ya umma, ambapo Absa iliongeza kiwango cha mkopo hadi shilingi milioni 200, kuongeza muda wa marejesho hadi miaka 10, na kupunguza muda wa kusubiri kuongeza mkopo (top-up) kutoka miezi 6 hadi miezi 3.

Hatua hizi kwa pamoja zinaonyesha dhamira endelevu ya Absa kusaidia wateja wanaopokea mishahara katika sekta mbalimbali katika hatua muhimu za maisha yao ya kifedha.

Akizungumza wakati wa kutangaza maboresho hayo, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere, alisema hatua hiyo imejengwa katika uelewa wa kina wa safari za maisha ya wateja. “Katika Absa, tunaelewa kuwa maisha ya kila mteja ni simulizi, yenye sura tofauti na nyakati muhimu. Iwe uko sekta ya umma au binafsi, jukumu letu ni kuwawezesha wateja kusonga mbele kwa kujiamini. Kwa kuboresha mikopo yetu binafsi isiyo na dhamana, tunawawezesha kusema NDIO kwa maendeleo – kwa sababu stori yao ni ya thamani sana,” alisema Bi. Ndabu.

Bi. Ndabu alisisitiza umuhimu wa unafuu na unyumbufu wa kifedha katika hatua mbalimbali za maisha. “Kuongezwa kwa muda wa marejesho na kiwango cha mkopo kunawapa wateja nafasi ya kusawazisha majukumu ya leo na malengo ya kesho. Kuanzia kuanzisha biashara, kuboresha makazi, kuwekeza katika elimu, kugharamia matibabu hadi kuunganisha madeni, bidhaa hii inawawezesha wateja kujisogeza mbele bila shinikizo lisilo la lazima la kifedha,” aliongeza.

Alibainisha pia kuwa wateja waliopo wanaokidhi vigezo wanaweza kuomba nyongeza ya mkopo au kufanya marekebisho ya mkopo (refinancing), kwa mujibu wa sera za ndani za benki na idhini ya tathmini ya mkopo.

Maboresho haya yanaungwa mkono na kampeni ya wateja ijulikanayo kama “Jisogeze na Mkopo wa hadi TZS 200m”, inayowahamasisha wateja kusonga mbele kwa ujasiri katika safari zao za kifedha.

Wateja wanaweza kuomba mkopo huo kwa kutembelea tawi lolote la Absa, kuzungumza na Afisa Mahusiano au kuwasiliana na vituo vya huduma kwa wateja vya benki hiyo.
Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Heristraton Genesis (kulia), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Jisogeze na Mkopo wa hadi TZS 200m”, inayolenga wafanyakazi wa sekta binafsi na umma, jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Bw. Aron Luhanga, Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano na Bi. Ndabu Swere, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi kutoka benki hiyo
Baadhi ya wakurugenzi na wafanyakazi wa Benki ya Absa, wakifurahia uzinduzi wa kampeni ya 'Jisogeze na Mkopo wa hadi TZS 200m jijini Dar es Salaam leo.

Monday, April 13, 2026

BENKI YA ABSA TANZANIA YAKABIDHI WODI YA WAZAZI ILIYOKARABATIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TEMEKE

   

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Patrick Foya (kushoto), na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dk. Mfaume Kibwana (Katikati), wakifungua pazia kuashiria makabidhiano rasmi ya Wodi ya Wazazi, iliyofanyiwa ukarabati na Benki ya Absa. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo, Temeke, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga.

Benki ya Absa Bank Tanzania leo imekabidhi rasmi wodi iliyokarabatiwa ya Wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kijamii unaoongozwa na wafanyakazi wa benki hiyo, wenye lengo la kuboresha mazingira ya huduma kwa kina mama, watoto pamoja na wahudumu wa afya.

Ukarabati huo umetekelezwa kupitia mpango wa Absa unaojulikana kama “Adopt a Ward”, ambao unaendeshwa na wafanyakazi wenyewe kwa kubaini mahitaji ya jamii, kukusanya rasilimali na kushirikiana na benki katika kuleta mabadiliko chanya yenye tija kwa jamii.

Kazi za ukarabati zilizofanyika katika wodi hiyo ni pamoja na akarabati wa paa na dari, uwekaji wa vigae kwenye kuta za vyoo, ukarabati wa madirisha, kazi za nje za mabomba maalumu ya plastiki (PVC), ukarabati wa mifumo ya umeme, kazi za mabomba ya maji, ufungaji wa milango ya alumini, ufungaji wa viti vya vyoo na sinki pamoja na uchoraji wa majengo.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Patrick Foya, alisema kuwa mpango huo unaonyesha imani ya muda mrefu ya benki kwamba jamii huimarika pale taasisi na watu binafsi wanapowekeza pamoja katika suluhisho za vitendo zinazoboresha maisha.

Katika Absa, tunaamini kuwa ‘Stori yako ina Thamani’, na leo tunakumbushwa kuwa hadithi za kina mama, watoto, familia na wahudumu wa afya zina umuhimu mkubwa. Ukarabati huu ni utekelezaji wa dhana yetu ya ‘Kuwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, Hatua Moja baada ya nyingine’. Pia unaonyesha utamaduni tunaoujenga Absa, ambapo watu wetu wanachukua jukumu la kubaini mahitaji ya jamii, kuhamasisha msaada na kushirikiana na benki kuleta mabadiliko endelevu.

Aliongeza kuwa mradi huo unaakisi ajenda pana ya uwajibikaji wa kijamii na uendelevu ya Absa, kwa kusaidia kuboresha mazingira ya huduma kwa heshima na ustahiki kwa wanawake na watoto, sambamba na kuimarisha mchango wa benki katika ustawi wa jamii.

Huu ni mfano halisi wa namna Absa inavyokuwa nguvu chanya katika jamii. Kwa kuboresha wodi ya Mama na Mtoto, tunawaunga mkono wahudumu wa afya wanaohudumia jamii kila siku, na pia kuboresha uzoefu wa huduma kwa kina mama na watoto. Tunaamini uwekezaji wa pamoja wa aina hii ni muhimu katika kujenga jamii imara na yenye afya.

Mpango huo uliwakutanisha wafanyakazi wa Absa kutoka idara mbalimbali, ukiakisi utamaduni wa ndani wa taasisi hiyo unaowahamasisha wafanyakazi kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo ya jamii, huku benki ikiongeza nguvu katika jitihada zao ili kuongeza athari chanya.

Mfumo huu wa utoaji unaoongozwa na wafanyakazi pamoja na msaada wa taasisi, umeendelea kuwa sehemu ya mkakati mpana wa Benki ya Absa Tanzania katika uwajibikaji kwa jamii, unaojikita katika ushirikiano, ujumuishi na uundaji wa thamani ya muda mrefu kwa jamii.

Hatua hiyo ya makabidhiano pia inaendana na lengo la Absa ya “Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, Hatua Moja baada ya nyingine” pamoja na ahadi yake ya chapa ya “Stori yako ina Thamani”, ambayo ni msingi wa namna benki hiyo inavyotoa thamani kwa wateja, jamii na wadau wake.

Kupitia uboreshaji wa mazingira katika sekta muhimu ya afya, Benkiy a Absa Tanzania inalenga kuchangia katika kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto, huku ikiimarisha umuhimu wa ushirikiano wa pamoja katika kutatua changamoto za jamii.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Patrick Foya (katikati), akikata utepe kuashiria makabidhiano rasmi ya Wodi ya Wazazi ya Hosptali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, iliyofanyiwa ukarabati na Benki ya Absa. Hafla hiyo, ilifanyika hospitalini hapo, Temeke, Dar es Salaam leo. Kulia ni na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Mfaume Kibwana na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga.
Mkuu wa Udhibiti ya Udhibiti Ubora wa, Bw. Hosptali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dk. Selemani Kivoja, akisalimiana na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Patrick Foya (kushoto), huku Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Mfaume Kibwana (kushoto), akiangalia, katika hafla ambayo beni hiyo ilikabidhi jengo la wodi ya wazazi lililokarabatiwa na benki hiyo, katika hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo, Temeke, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Bw. Patrick Foya, pamoja na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa hafla ya makabidhiano ya Wodi ya Wazazi iliyofanyiwa ukarabati na benki hiyo.

Sunday, March 29, 2026

BENKI YA ABSA YAENDELEA KUWAWEZESHA WANAWAKE WAJASIRIMALI KIUCHUMI

Meneja Bidhaa wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Bryton Kimemeta (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanawake wajasiriamali, wanachama wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, katika semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa uwezeshaji wa benki hiyo ikihusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo hayo ni sehemu ya mikakati ya Benki ya Absa ya kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Meneja Msaidizi wa Uhakiki wa Biashara wa Benki ya Absa Tanzania. Bi. Miriam Ngajilo (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanawake wajasiriamali, wanachama wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, katika semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa uwezeshaji wa benki hiyo ikihusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo ya kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la Benki ya Absa la Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, Bw. Hafizur Milon (kushoto), akizungumza kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya taasisi hiyo na Benki ya Absa Tanzania, wakati wa semina ya wanawake wajasiriamali wanachama wa taasisi hiyo kuhusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya Benki ya Absa katika kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la 'Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine', kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Mtaalamu wa Mafunzo wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Hussein Said (kulia), akizungumza na baadhi ya wanawake wajasiriamali, wanachama wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, katika semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa uwezeshaji wa benki hiyo ikihusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo ya kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la Benki ya Absa la Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Mmoja wa wanawake wajasiariamali mwanachama wa Taasisi ya huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, Amina Makongoro akichangia hoja wakati wa semina kuhusu elimu ya kifedha na usimamizi wa biashara wenye tija, iliyoandaliwa na taasisi hiyo ikiwezeshwa na Benki ya Absa Tanzania, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo katika kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la 'Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine', kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Baadhi ya wanawake wajasiriamali wanachama wa Taasisi ya huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, wakisikiliza, wakati Meneja Bidhaa wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Bryton Kimemeta, akizungumza nao wakati wa semina kuhusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, iliyoandaliwa na Taasisi ya ASA Microfinance Tanzania kwa uwezeshaji wa benki hiyo, jijini Dar es Salaam jana. Semina hiyo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo katika kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la 'Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine', kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.

Friday, March 27, 2026

MRADI WA COOKFUND WALETA MAGEUZI YA MATUMIZI YA NISHATI KATIKA TAASISI ZA UMMA

Mshauri Mkuu wa Kiufundi wa UNCDF, Bw. Peter Malika, akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya teknolojia ya upishi salama kwa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam jana. Serikali ya Tanzania, kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Ujumbe wake nchini, na usimamizi wa programu ukifanywa na Mfuko wa Maendeleo wa Mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF), inatekeleza Programu ya CookFund ili kuharakisha mpito wa matumizi ya nishati safi ya kupikia katika kaya na taasisi za umma, hususan mashuleni. Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (wa pili kutoka kulia), alikuwa mgeni rasmi.

Dar es Salaam, Tanzania | Zaidi ya wanafunzi 62,000 kote Tanzania sasa wananufaika na majiko salama na safi zaidi kufuatia usakinishaji wa zaidi ya majiko ya kisasa 170 ya nishati safi ya kupikia katika shule na taasisi za umma zaidi ya 45. Hatua hii muhimu iliadhimishwa katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam, ikionesha mchango wa mpango huu katika kupunguza matumizi ya kuni na mkaa na hivyo kukabiliana na ukataji wa miti.

Mpango huu unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na kutekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kupitia programu ya CookFund.

Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Salome Makamba alisema:

Mapinduzi haya kuelekea matumizi ya nishati safi ya kupikia ni kipaumbele cha kimkakati cha taifa kinachochangia kulinda mazingira, kuboresha afya ya umma na kuongeza ufanisi wa kiuchumi. Kwa kuzipatia shule na taasisi za umma teknolojia za kisasa za kupikia, tunalenga kulinda misitu yetu, kupunguza hewa chafuzi, na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wetu. Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo kupanua upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa kuzingatia Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia (2024–2034).

Jitihada za nishati safi ya kupikia nchini zinaongozwa na Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na wizara na taasisi nyingine za Serikali, ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, pamoja na taasisi nyingine za umma. Hadi sasa, msaada huu kwa taasisi za umma, hususan shule, unalenga taasisi zote zinazohudumia watu zaidi ya 100 kwa wakati mmoja ili kuachana na matumizi ya kuni na mkaa.

Hatua hizi zinaendana na vipaumbele vya kitaifa vya kupunguza ukataji wa miti, kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi, na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za umma. Matumizi ya kuni na mkaa huzalisha chembechembe hatarishi zinazoweza kusababisha magonjwa mbalimbali ya mfumo wa upumuaji kama pumu na saratani ya mapafu.

Kupitia programu ya CookFund, inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya, hatua hizi zinalenga kupunguza matumizi ya nishati za kuni na mkaa kwenda kwenye teknolojia bora na zenye ufanisi zaidi kama majiko yanayotumia mkaa mbadala, majiko ya umeme (electric pressure cookers), biyoethano, majiko banifu, pamoja na gesi. Teknolojia hizi zinatarajiwa kupunguza shinikizo kwa rasilimali za misitu, kuboresha ubora wa hewa jikoni, na kuongeza afya na usalama wa wanafunzi na watumishi. Hadi sasa, taasisi 45 zimeboresha mifumo yao ya upishi, nyingi zikiwa ni shule za msingi na sekondari.

Aidha, kupitia CookFund, UNCDF inatoa msaada wa kifedha na kiufundi kwa makampuni na wajasiriamali wanaokidhi vigezo ili kuongeza usambazaji wa nishati safi ya kupikia. Msaada huu unajumuisha uwekezaji wa mtaji na mtaji wa uendeshaji kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa biashara zinazojihusisha na uzalishaji, uagizaji, usambazaji na uuzaji wa majiko, mafuta na bidhaa au huduma zinazohusiana na nishati safi ya kupikia.

Kwa upande wake, Mkuu wa Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Marc Stalmans, alisema:

Umoja wa Ulaya umejikita kikamilifu katika kuendeleza hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani, na Tanzania siyo tofauti. Mpango huu ni sehemu ya juhudi zetu za kusaidia mpito kuelekea nishati safi. Kupitia msaada wa Umoja wa Ulaya, jamii zinazingatia mbinu endelevu zinazolinda mazingira, huku zikichochea ukuaji wa uchumi, kukuza ajira, na kuboresha upatikanaji wa nishati mashuleni, kwenye biashara pamoja na kaya.

Naye Mshauri Mkuu Maswala Kiufundi wa UNCDF, Bw. Peter Malika, alibainisha kuwa pamoja na msaada uliotolewa kwa taasisi 45 katika wilaya 14 za Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma na Mwanza, programu hiyo imewekeza dola milioni 10.1 katika biashara ndogo na za kati 102.

Nishati safi ya kupikia inapunguza utegemezi wa kuni na mkaa huku ikiboresha usalama, afya na ufanisi wa majiko shuleni,” alisema Bw. Malika. “CookFund inaonesha wazi kuwa teknolojia za kisasa za nishati zinaweza kuleta mageuzi makubwa katika taasisi za umma na kuboresha moja kwa moja mazingira ya kujifunzia kwa maelfu ya wanafunzi.

Kwa ujumla, programu hii imeleta matokeo chanya na yenye mageuzi makubwa, ikichangia uundaji wa ajira 27,005 (za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja), jumla ya biashara 4,933 katika mnyororo wa thamani wa nishati safi ya kupikia, kufikia kaya zaidi ya 482,089, na kupunguza zaidi ya tani 3,911,450 za uzalishaji wa hewa ukaa. Mafanikio haya yanaonesha mchango mkubwa wa programu hii katika maendeleo endelevu, ustawi wa jamii na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, akitoa hotuba yake wakati wa makabidhiano ya vifaa vya teknolojia ya upishi salama kwa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam jana. Serikali ya Tanzania, kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Ujumbe wake nchini, na usimamizi wa programu ukifanywa na Mfuko wa Maendeleo wa Mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF), inatekeleza Programu ya CookFund ili kuharakisha kipindi cha mpito wa matumizi ya nishati safi ya kupikia katika kaya na taasisi za umma, hususan mashuleni.
Mkuu wa Ushirikiano wa Ujumbe wa EU nchini Tanzania, Bw. Marc Stalmans, akihutubia hadhira wakati wa makabidhiano ya vifaa vya teknolojia ya upishi salama kwa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam jana. Serikali ya Tanzania, kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Ujumbe wake nchini, na usimamizi wa programu ukifanywa na Mfuko wa Maendeleo wa Mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF), inatekeleza Programu ya CookFund ili kuharakisha kipindi cha mpito wa matumizi ya nishati safi ya kupikia katika kaya na taasisi za umma, hususan shule. Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (wa tatu kutoka kulia), alikuwa mgeni rasmi.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (kushoto), anapika wali akitumia jiko linalotumia nishati salama ya kupikia, wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya teknolojia ya upishi salama katika Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam jana. Serikali ya Tanzania, kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Ujumbe wake nchini, na kwa usimamizi wa programu kutoka Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuendeleza Mitaji (UNCDF), inatekeleza Mpango wa CookFund ili kuharakisha kipindi cha mpito cha matumizi ya upishi safi katika kaya na taasisi za umma, hususan mashuleni. Kutoka kulia ni Bw. Marc Stalmans, Mkuu wa Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, akiwa pamoja na Mshauri Mkuu wa Kiufundi wa UNCDF, Bw. Peter Malika.

Sunday, March 22, 2026

WAKULIMA KARATU KUNUFAIKA NA MAPINDUZI YA KIDIJITALI KUPITIA MIXX BY YAS

Meneja wa Mahusiano ya Biashara na Serikali wa Mixx by Yas, Suleiman Asilia (wa tatu kushoto), na Meneja wa Kibiashara Kanda ya Kaskazini wa Mixx by Yas, Eric Sosteness (kushoto kwake), pamoja na Kaimu Mkuu wa COPRA Kanda ya Kaskazini, Famia Amiri, wakimkabidhi runinga janja (Smart TV) Mwenyekiti wa ACU, Shedrack Asseri (mwenye koti jeusi), kwa ajili ya urushaji wa moja kwa moja wa minada ya mazao ya kilimo ili kuongeza uwazi na ushiriki wakati wa msimu wa mazao mbalimbali, ikiwemo ufuta.

Arusha - Wakulima wa Wilaya ya Karatu wanatarajiwa kunufaika kwa kiasi kikubwa na upatikanaji bora wa taarifa za masoko pamoja na kuongezeka kwa uwazi katika biashara ya mazao, kufuatia kuanzishwa kwa mpango wa kidijitali unaoongozwa na Mixx by Yas kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya kilimo.

Mpango huo ulizinduliwa rasmi kupitia hafla ya makabidhiano ya runinga janja (Smart TV) iliyotolewa kwa Chama Kikuu cha Ushirika Arusha (ACU) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA). Hatua hii inalenga kuboresha upatikanaji wa taarifa muhimu za masoko kwa wakulima na kuongeza ushiriki wao katika mifumo rasmi ya biashara.

Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa Kibiashara Kanda ya Kaskazini wa Mixx by YasEric Sosteness, alisema kuwa suluhisho za kidijitali zinatoa fursa mpya kwa wakulima kufikia masoko kwa urahisi zaidi.

Kupitia Mixx by Yas, tumejikita kuwawezesha wakulima kwa kuwapatia suluhisho zinazowaleta karibu zaidi na masoko. Upatikanaji wa taarifa za mnada kwa wakati utawasaidia wakulima kufanya maamuzi sahihi na kuongeza kipato chao,” alisema.

Runinga hiyo janja inatarajiwa kuwa chombo muhimu katika kurusha moja kwa moja minada ya mazao ya kilimo. Kupitia teknolojia hiyo, wakulima wa Karatu na maeneo jirani wataweza kufuatilia mwenendo wa bei na shughuli za biashara bila kulazimika kuwepo katika eneo la mnada. Hatua hii inatarajiwa kuongeza uwazi, kupunguza upotoshaji wa taarifa, na kuimarisha ushindani wa haki katika soko.

Kwa upande wake, Meneja wa Mahusiano ya Biashara na Serikali wa Mixx by YasSuleiman Asilia, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na taasisi za umma katika kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa wakulima.

Ushirikiano huu unaonesha jinsi teknolojia na ubia vinavyoweza kufungua fursa mpya kwa wakulima. Lengo letu ni kuhakikisha wakulima wanaunganishwa zaidi, wanapata taarifa sahihi na wanajumuishwa kifedha,” alieleza.

Naye Kaimu Mkuu wa COPRA Kanda ya Kaskazini, Famia Amiri, alibainisha kuwa urushaji wa moja kwa moja wa minada utaongeza uwazi na kujenga imani katika mfumo wa biashara ya mazao, hususan katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea msimu wa ufuta.

Mbali na mpango huo, Mixx by Yas inaendelea kutoa huduma mbalimbali zinazolenga kumwezesha mkulima, ikiwemo Mixx Kilimo inayorahisisha miamala, Afya Mkulima inayolenga ustawi wa wakulima, pamoja na Kilimo Pesa inayowezesha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa urahisi zaidi.

Kwa ujumla, mpango huu unaakisi mwelekeo wa sekta ya kilimo nchini kuelekea matumizi makubwa ya teknolojia katika kuboresha mifumo ya biashara. Kadri suluhisho hizi zinavyozidi kuenea, zinatarajiwa kuongeza tija, kuimarisha kipato cha wakulima, na kuwapa nafasi kubwa zaidi katika uchumi wa kisasa unaozidi kuwa wa kidijitali.

Wednesday, March 18, 2026

BENKI YA ABSA YAJIZATITI KUENDELEA KUWAWEZESHA WANAWAKE

  

Ofisa Mkuu wa Teknolojia wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Emmanuel Mwinuka, akitoa mada katika kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Accelerate Women Summit’ na kufanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Likidhaminiwa na Benki ya Absa, kongamano hilo liliwaleta pamoja viongozi wanawake kujadili namna teknolojia, uongozi na ujumuishwaji vinavyounda mustakabali wa taifa.
Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kulia), akipokea cheti cha shukrani kwa udhamini kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Acceleration Foundation, Bi. Bernice Fernandos, wakati wa Kongamanao la wanawake lililoitwa ‘Accelerate Women Summit’ na kufanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Likidhaminiwa na Benki ya Absa, kongamano hilo liliwaleta pamoja viongozi wanawake kujadili namna teknolojia, uongozi na ujumuishwaji vinavyounda mustakabali wa taifa. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Meneja anayeshughulikia miradi wa Benki ya Absa, Bi. Munira Chambuso, Ofisa Mkuu wa Teknolojia, Bw. Emmanuel Mwinuka, na Bi. Cygrade Othman pia kutoka benki hiyo.
Ofisa Mkuu wa Teknolojia wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Emmanuel Mwinuka (katikati), na Bi. Munira Chambuso (kushoto) kutoka Absa, wakimsikiliza mfanyabiashara na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Dewji, wakati wa Kongamano la wanawake lililoitwa ‘Accelerate Women Forum’ na kufanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Likidhaminiwa na Benki ya Absa, kongamano hilo liliwaleta pamoja viongozi wanawake kujadili namna teknolojia, uongozi na ujumuishwaji vinavyounda mustakabali wa taifa.
Bi. Thamrat Khamis (kushoto), anayeshughulikia akaunti za biashara ndogo na za kati (SME) akizungumza na mmoja wa washiriki wa Kongamano la wanawake lililoitwa ‘Accelerate Women Forum’ na kufanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Ukidhaminiwa na Benki ya Absa, mkutano huo uliwaleta pamoja viongozi wanawake kuchunguza namna teknolojia, uongozi na ujumuishwaji vinavyosukuma mustakabali wa taifa.
Wakishangilia, ni timu ya timu kutoka Benki ya Absa, ikiongozwa na Ofisa Mkuu wa Teknolojia, Bw. Emmanuel Mwinuka (wa pili kushoto), wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya Kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Accelerate Women Forum’ likifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Likidhaminiwa na Benki ya Absa, kongamano hilo, liliwaleta pamoja viongozi wanawake kujadili namna teknolojia, uongozi na ujumuishwaji vinavyounda mustakabali wa taifa.

Monday, March 16, 2026

BENKI YA ABSA TANZANIA YADUMISHA USHIRIKANO NA WATEJA WAKE

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kushoto), Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Alhad Omar, pamoja na wageni wengine wakichukua chakula cha futari katika hafla iliyoandaliwa na benki kwa wateja wake jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Alhad Omar (kulia), akipokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, wakati wa hafla ya futari, iliyoandaliwa na benki kwa wateja wake jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Katikati ni Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa benki hiyo, Bw. Muhsin Kaye.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere (wa tatu kushoto), pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki na wageni wengine, wakichukua chakula cha futari, katika hafla iliyoandaliwa na benki kwa wateja wake jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benkiy a Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, akiwahutubia wateja na wageni waalikwa, katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Alhad Omar, akihutubia baadhi ya wateja na wafanyakazi wa Benkiy a Absa Tanzania, wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Alhad Omar (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Bank Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa pili kushoto), pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa benki hiyo wakipiga picha ya pamoja baada ya hafla ya futari, iliyoandaliwa na benki kwa wateja wake jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Muhsin Kaye (kushoto), akimuaga Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Alhad Omar, huku Mkurugenzi Mtendaji wa benki, Bw. Obedi Laiser, akiangalia, baada ya hafla ya futari iliyoandaliwa na benki kwa wateja wake jijini Dar es Salaam hivi karibuni.